Tuache Ufyatu: Mtu Hawi Gaidi kwa Kuitwa Gaidi

Tuache Ufyatu: Mtu Hawi Gaidi kwa Kuitwa Gaidi

Kwa mashitaka hayo unatakiwa uthibitishe katoa fedha kwa ajili ya ugaidi. Unaona inavyokuwa ngumu
Ugumu unatoka wapi?
Dereva wake si ametapika kila kitu
Hiyo concept note ya kuandika maboresho ya ofisi ni kwa ofisi ipi ilioboreshwa?
Tusubiri kesi ianze
 
Ni kweli haki lazima ionekane itendeke lakini tumeona watu walioshitakiwa kwa kosa hili wakikaa ndani kwa takriban miaka minane na mwisho DPP kusema hataki kuendelea na kesi. Mimi nadhani tufike mahali mahakama iwe inazitupitilia mbali kesi zinazochukua zaidi ya mwezi mmoja kuanza kusikilizwa kwa kisingizio chochote kile na kuamuru mshitakiwa alipwe fidia.

Amandla...
Katiba mpya itakayoondoa ujinga wa watu kujipa umungu mtu yahitajika.
 
Ugumu unatoka wapi?
Dereva wake si ametapika kila kitu
Hiyo concept note ya kuandika maboresho ya ofisi ni kwa ofisi ipi ilioboreshwa?
Tusubiri kesi ianze
Sawa tunasubiri, kama ilivyokuwa wakati wa IGP Mahita.
 
Alishapokea na nje…. Zile asingepata
Aliypiga cm kwamwezake ni nani kwamba njoo uchukue hela zenu zipo tu ,ninan utampigiaje aje achukue hela aliyechukua tayari nje

Nje ,wapi ,nje chooni ,ya nyumba

Nambie outskirt ipi
 
Uwe unakumbuka kwamba huko huko mahakani tena ni hiyo mahakama ya kisutu na ni hakimu huyo huyo simba aliyewatia hatiani akina mbowe kwa ushahidi wa kutengenezwa. Kwahiyo Kama nia ni kutaka Mbowe akae mahabusu muda mrefu na kupewa hukumu ya ushahidi wa kutengeneza hadi aje atoke mahakama kuu ni kwamba lengo la kumuonea litakuwa limetekelezwa.

Kwahiyo CDM watakuwa wajinga kukaa na kutegemea Kuna haki yoyote itatendeka kwe kesi inayosikilizwa na hakimu Simba. Hivyo waachwe CDM wapige kelele huenda Rais atasikia kilio cha wananchi
 


Unaweza kumuita mtu chechote kile; lakini kumuita mtu tu kitu hakimfanyi mtu kuwa kitu kile. Ni kweli kwamba kuna majina mwingine ukimuita mtu unamvunjia heshima, hadhi, na utu wake mbele ya jamii. Kwa mfano, mtu ameachana na mke wake au mume wake lakini kwa sababu ya machungu ya kuachana anaenda na kumtangaza kuwa "yule alikuwa malaya" au "alikuwa mlevi" n.k Sasa watu wengine wanaweza kweli kuamini na wao wanaweza kueneza habari hizo kuwa "yule alikuwa malaya". Hata ukimuuliza alijuaje atasema "jamaa yake walioachana" ndio alimuambia.

Kwenye siasa hili nalo ni kweli. Kuna mambo unaweza kumuita mpinzani wako wa kisiasa ili kumvunjia heshima, hadhi, na utu. Na wakati mwingine unaweza kumuita kitu ili kumharibia nafasi zake za kisiasa. Sote tunajua jinsi gani jina aliloitwa Dkt. Salim A. Salim lilivyomvurugia nafasi yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano 1995. Na tumeona mbinu hii ikitumiwa karibu na pande zote za kisiasa nchini - unaweza kuwaita watu "wachochezi" au "mafisadi" au unaweza kumuita mtu jina lolote.

Hata hivyo, linapokuja suala la kisheria - ambalo ni tofauti na la kisiasa - ukimuita mtu jina na mkaenda mahakamani basi suala huko ni ushahidi na uzito wa ushahidi huo (preponderance of evidence). Ndio maana kuna kesi za kumtangaza mtu vibaya au kumzushia ubaya (libel and defamation). Dkt. Salim huyo huyo aliwahi kushinda mamilioni ya hela dhidi ya gazeti la The East African miaka kadhaa nyuma kutokana na makala yao moja hivi.

Sasa Mbowe amedaiwa kuwa ni "Ghaidi" na jeshi la polisi. Kwa vile hili ni suala la mahakamani na la kisheria basi ni jukumu la mleta mashtaka kuleta ushahidi usio na shaka wa ughaidi huo. Na ili kitu kiwe ushahidi ni lazima kikidhi matakwa ya kisheria. Kusema tu "tuna ushahidi" hakufanyi ushahidi huo kukubalika mahakamani. Ni kwa sababu hiyo binafsi nasubiria kuona hicho kinachoitwa "ushahidi" hasa utakaposimama na kuhojiwa na upande wa utetezi na kupimwa kwa mwanga wa sheria kuona kama unaweza kumtia mtu hatiani.

Nje ya hapo, inawezekana hili la "ughaidi" linatumika tu tena kisiasa kama nilivyoelezea hapo juu. Kinachotakiwa kufanyika siyo tu kutaka kesi ifutwe au iondolewe bali iachwe iendelee mahakamani ili ushahidi uletwe, vieleleze viletwe ili kwa mara moja na daima uamuzi wa mahakama utolewe juu ya tuhuma hizi. CHADEMA wasitake tu viongozi wao waachiliwe pasipo masharti bali watake haki itendeke na kesi iharakishwe.

Kwani, kumuita mtu ughaidi hakumfanyi kuwa ghaidi bali ushahidi usio na shaka (siyo wa kupika) unaoweza kumtia hatiani mtu katika mahakama yoyote iliyo huru.

Haki Itendeke na Ionekane Inatendeka na Imetendeka kama inavyotakiwa kutendeka bila kuteteleka.

MMM
Nani atawaamini hawa.
 
Akili zimeanza kurudi sio?

we jamaa aisee

enzi za Magu you never questioned anythinh

your integrity is waaay down the ashes

You him to act according to your whims and then akili yake ndo itakuwepo. Against you. Hana akili. So tuambie Wewe Ni mungu au dubwana la sayari Mpya. You own the truth.
 
Mwendazake alifanya vibaya hadi shetani akamkana lakini hukuona.

Tuache sisi tuliozoea kwa kuuliza,kukaripia na hata kupiga kelele bila kujali dini ya mtu au kabila lake.

MMK,THE BIG SHOW Ritz Baba yenu mmoja wajomba tofauti.

Alifanya vibaya kwa job description ya Nani. Wakati anaomba Kura alisema atafanya Nini? Wewe unampima kwa vigezo gani? Nicampoop.
 
Inajulikana miaka yote jeshi la polisi linaitumikia CCM, unapoona hati ya mashtaka imeanza kubadilishwa unajua wazi ni muendelezo wa michezo yao miovu wanayowafanyia wapinzani kila mara CCM ipowekwa kwenye wakati mgumu.

Sirro awe makini sana, kama ushahidi watakaouwasilisha mahakamani usipojitosheleza kuishawishi mahakama atatakiwa kujiuzulu nafasi yake ya IGP, kwasababu ataonekana kuwaonea Chadema (Mbowe) na hii itaondoa imani ya watanzania kwake.
Kwa hiyo kila kesi ambayo mahakama inatupilia mbali kwa ushahidi usiojitosheleza basi IGP anatakiwa kujiuzulu? Acha emotions
 
Mbowe sio mwanasisasa wa kwanza kupewa kesi ya ugaidi.
Rwakatare aliwahi kupewa kesi ya Ugaid na alishinda .
Mbowe hiii kesi yake imekaa kimkakati kumnyamazisha asidai katiba mpya.
Huenda ikachukua muda mrefu kuisha ili mama afanye kazi bila shinikizo au hadi atakapotaka mwnyewe kuleta katiba mpya.
Mbowe anawezekana akafungwa badae akakata rufaa ndo akaachiwa
Jambo la kusubiri na kuona.
 
I see you got my dick in your mouth!

Nani mwingine zaidi yangu aliyemchana Magufuli humu?

Nikuwekee orodha toka 2015 mpaka 2021 ya mada za mimi kumchana Magufuli?

Stupid brainless dunce.
Mkuu kuna wakati ulipotea na kupoteza mwelekeo, kubali kukosolewa

Zamani Inilikukubali lakini ukaboa
Ulishabikia lissu kupigwa risasi
 
Back
Top Bottom