Acha nichambue kwa ufupi tabia za marehemu ulizoorodhesha:-
1. Mpenda sifa popote.
Hii ni hulka ya kila binadamu kwa wakati wake na nafasi yake kwa hiyo hoja yako hapa haina mashiko
2. Mpenda pombe.
Le Mutuz hakuwa mlevi wa pombe na sijawahi kumuona akinywa pombe naye pia alishasema mara nyingi kuwa hatumii pombe wala sigara
3. Mpenda umalaya.
Le Mutuz hakuwa malaya kama unavyofikiria ila alikuwa na hulka ya kujirusha na wanawake, kupiga picha n.k ila sio kuwalala. Alikuwa na wanawake lakini kwa level ya kumuita malaya.
4. Mpenda maisha ya kujirusha na kuponda raha.
Hii tabia alikuwa nayo na naichukulia kama tabia za watu wengine tu wanavyopenda kuride pikipiki, kuendesha magari, kujenga majumba mazuri n.k. No offense at all.
5. Mpenda kujipendekeza kwa watu maarufu (chawa)
Hii tabia alikuwa nayo lakini sio kosa kujipendekeza kwa mtu ikiwa huvunji sheria.
Yote kwa yote marehemu hasemwi vibaya, tuache apumzike.