Tuacheni unafiki, Le Mutuz alikuwa ni mtu wa ovyo na mfano mbovu kwa vijana

Tuacheni unafiki, Le Mutuz alikuwa ni mtu wa ovyo na mfano mbovu kwa vijana

Ni sawa tu kwao kwa sababu hata wewe ni mtu wa kisasi, jiulize kama huna kisasi iweje mpaka leo unaongeleaga tu mambo ya mtu ambaye hayupo duniani kitambo tu sasa tena kwa matusi ya ajabu tu
Ndio nimekuambia andaa matusi kabisa ww na wenzako ya kulipiza kisasi. Kifo changu mke wangu atakitangaza hapa jukwaani. Kuna jingine boss kwa msaada zaidi?
 
Kila mtu aliyeko kwenye mtandao ni lazima awe na maisha ya kuigwa na watu wote? Wewe ni mzee wa miaka mingapi?
Kwanza tujue kwamba siyo kila mtu anakuwa na followers,mfano mimi ukiniuliza ni nani na nani wananifuatilia nitakwambia sina sababu sina hulka au vyovyote ya ku-share ninayoyafanya ila kwa status ya Le Mutuz huyo alikuwa na watu wanamfuatilia so kwa vyovyote wapo watakaoona ni sahihi kwao kuiga baadhi ya matendo yake kumbe siyo.

Haya mambo ya kutosema ukweli kuwahusu marehemu way back yalizitesa sana jamii zetu,ilikuwa mtu kafa kwa ukimwi na anaonekana kabisa umemuuwa ukimwi risala inasema amekufa kwa homa ya manjano,lazima kama jamii tukubali madhaifu ya marehemu wetu halafu watu waambiwe hili lilikuwa sahihi hili halikuwa sahihi.

Hata mimi siku nikifa yatakuwa haya haya muhimu nitengeneze mapema kile ninachotaka kisemwe siku sipo na huyu ndipo alipofeli
 
Ndio nimekuambia andaa matusi kabisa ww na wenzako ya kulipiza kisasi. Kifo changu mke wangu atakitangaza hapa jukwaani. Kuna jingine boss kwa msaada zaidi?
🤣🤣🤣

Acha mbwembwe Mkuu, umejuaje kama utatangulia wewe, kwa nini isiwe mke
 
Mtoa post sio muongo?hasengenyi? halewi? hatukani? hategei kazini? anawaheshimu watu wote?

Wengi humu tunaonaga vibanzi vya wenzetu while sie tuna maboriti...

Le Mutuz ye aliamua kutokuwa mnafiki, aliishi maisha yake, hakuwa omba omba....sasa maisha yake yanakuathirije?

Mind yo business...The Man is gone, kama ulikua haumpendi shauri yako, hakuna anayependwa na wote!

Tuache unafiki....
 
Nenda William ,nasikitika kuwa uliishi maisha ya furaha na amani ili walio nyuma na wanaokutizama wajue una furaha kumbe ulikuwa mwingi wa msongo wa mawazo .

Nenda William ambayo hukuyasema kipindi chako yenye huzuni sitayaweka wazi ukiwa hujitambui tena .

Zaidi nitakukumbuka kwa kuumaliza mgogoro wangu na profesa Anangisye , sikutegemea kuwa ipo siku nitakaa meza moja tena na huyu profesa .

Nenda Wiliam , ulikuwa shujaa sana wakati sisi wa rika lako tukiwa wahuni kwa uficho wewe ulionesha wazi maana ndiyo ilikuwa furaha ya moyo wako .

Nenda Wiliam , mimi mshikaji wako na nduguyo nitakukumbuka kwa mengi mazuri yasiyomithirika ukizingatia tulikuwa na watu wa kaliba moja japo mimi sikuwa muwazi kiasi chako .

Nenda Wiliam, Ni njia yetu sote.[emoji24][emoji24]
 
Kwanza, ninapenda kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, washikaji na wanaJF walioguswa na kifo cha William Malecella. Mungu awape faraja katika kipindi hichi kigumu cha majonzi.

Sasa, twende moja kwa moia kwenye mada, kupitia mada hii, bila kuficha wala kumumunya maneno, William Malecela (Le mutuz) alijulikana na kufahamika zaidi kama mtu wa ovyo kwa sifa hizi (sifa ambazo alikuwa akijivunia nazo hadharani mitandaoni na mitaani);

1. Mpenda sifa popote.
2. Mpenda pombe.
3. Mpenda umalaya.
4. Mpenda maisha ya kujirusha na kuponda raha.
5. Mpenda kujipendekeza kwa watu maarufu (chawa)

Le Mutuz japokuwa alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 50, akijaliwa kuwa na watoto, akipambana kwa namna mbalimbali kutafuta kipato, huku akitokea kwenye familia ya mzee Malecela yenye heshima kubwa sana kisiasa na kijamii ndani na nje ya Tanzania, lakini mienendo na tabia za Le mutuz zilikuwa zenye kutia aibu na kinyaa, akiishi kama kijana aliyepevuka juzi, aliyekosa malezi yoyote ya kijamii na kidini.

Japokuwa hayo yalikuwa ni maisha yake binafsi (sio busara sana kuyahukumu) lakini ni vyema kusema ukweli na kuweka angalizo muhimu kwa vijana ambao ndio wamejaa mtandaoni kuwa makini na kukwepa kuiga au kujifunza kupitia maisha binafsi ya Le mutuz ambayo yalijaa anasa na uchafu mwingi.

UKWELI USEMWE KIKAMILIFU.
Huu uzi wako ukifika kesho salama shukuru Mungu.
 
Kwanza tujue kwamba siyo kila mtu anakuwa na followers,mfano mimi ukiniuliza ni nani na nani wananifuatilia nitakwambia sina sababu sina hulka au vyovyote ya ku-share ninayoyafanya ila kwa status ya Le Mutuz huyo alikuwa na watu wanamfuatilia so kwa vyovyote wapo watakaoona ni sahihi kwao kuiga baadhi ya matendo yake kumbe siyo.

Haya mambo ya kutosema ukweli kuwahusu marehemu way back yalitesa sana jamii zetu,ilikuwa mtu kafa kwa ukimwi na anaonekana kabisa umemuuwa ukimwi risala inasema amekufa kwa homa ya manjano,lazima kama jamii tukubali madhaifu ya marehemu wetu halafu watu waambiwe hili lilikuwa sahihi hili halikuwa sahihi.

Hata mimi siku nikifa yatakuwa haya haya muhimu nitengeneze mapema kile ninachotaka kisemwe siku sipo.
Was he a public figure?

Usahihi wa jambo kuhusiana na maisha private ya mtu unapimwa kwa kutumia vigezo gani?

Alikuwa na madaraka yoyote ambayo yali impact maisha yako in one way or another?

If anything, labda alikuja kujulikana zaidi kutokana na status ya mzee wake. Lakini hakutumia hilo kufanya ufisadi.
 
Utamaduni wa kutukana marehemu unaimarishwa kwa kisingizio cha uwazi na demokrasia, haya twendelee. Mtu Akifa duniani kote tunatafakari mazuri yake, mabaya tunamwachia Mungu wake, Ila sasa tunatafakari mabaya yake, mazuri tunamwachia Mungu

Biblia inasema ukiwapo wema wowote, sifa nzuri yoyote, tuyatafakari hayo, lakini mtu anatafuta ubaya wowote, sifa mbaya yoyote, ndio anaitafakari, tena ya marehemu, huo ni ushetani
 
🤣🤣🤣

Acha mbwembwe Mkuu, umejuaje kama utatangulia wewe, kwa nini isiwe mke
Ni kweli ww unaweza kutangulia, lakini hakuna uwezekano wa mimi kuwatangulia nyie sukuma gang wote. Hivyo jipangeni kifo kikinikuta mlipize kisasi, maana najua ni kwa kiwango gani ninawaumiza wafuasi wa dhalimu.
 
Alikuwa wa ovyo Kwa vigezo vya nani?
Kwa vigezo vyako binafsi?
Au Kwa imani yako ?

Why tunapenda Ku judge watu Kwa kupitia vigezo vyetu ambavyo sio universal??

Umalaya unaweza thibitisha?au picha za Instagram na warembo ndo uthibitisho?
Pombe?lini ulimuona akinywa? Au picha Akiwa wavuvi ndo ushahidi wako??

Why mnapenda kuishi kinafiki?kujifanya watu wema Kwa nje huku mna madhambi ya kutisha Kwa Siri huku mnahukumu watu Kwa picha za mitandaoni?
Wewe usifanye hujui wakati kila kitu kiko wazi. Kwa zaidi ya 99% ya watu wamemjua marehemu kupitia mitandao, na kote huko marehemu aliona sifa na fahari kujitambulisha kama mpenda sifa, umalaya, ulevi, kuponda starehe na uchawa. Mtu wa namna hiyo, anawezaje kusemwa tofauti na hivyo?
 
Kwanza, ninapenda kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, washikaji na wanaJF walioguswa na kifo cha William Malecella. Mungu awape faraja katika kipindi hichi kigumu cha majonzi.

Sasa, twende moja kwa moia kwenye mada, kupitia mada hii, bila kuficha wala kumumunya maneno, William Malecela (Le mutuz) alijulikana na kufahamika zaidi kama mtu wa ovyo kwa sifa hizi (sifa ambazo alikuwa akijivunia nazo hadharani mitandaoni na mitaani);

1. Mpenda sifa popote.
2. Mpenda pombe.
3. Mpenda umalaya.
4. Mpenda maisha ya kujirusha na kuponda raha.
5. Mpenda kujipendekeza kwa watu maarufu (chawa)

Le Mutuz japokuwa alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 50, akijaliwa kuwa na watoto, akipambana kwa namna mbalimbali kutafuta kipato, huku akitokea kwenye familia ya mzee Malecela yenye heshima kubwa sana kisiasa na kijamii ndani na nje ya Tanzania, lakini mienendo na tabia za Le mutuz zilikuwa zenye kutia aibu na kinyaa, akiishi kama kijana aliyepevuka juzi, aliyekosa malezi yoyote ya kijamii na kidini.

Japokuwa hayo yalikuwa ni maisha yake binafsi (sio busara sana kuyahukumu) lakini ni vyema kusema ukweli na kuweka angalizo muhimu kwa vijana ambao ndio wamejaa mtandaoni kuwa makini na kukwepa kuiga au kujifunza kupitia maisha binafsi ya Le mutuz ambayo yalijaa anasa na uchafu mwingi.

UKWELI USEMWE KIKAMILIFU.

Tusipangiane namna ya kuishi please

Lakini pia kuna sheria ya namna ya kushi
Kama kuna sheria alivunja sawa alaumiwe

Uzee usikie tu ukikufika utajuta
 
Back
Top Bottom