Tuambie Mechi yako Bora zaidi ya soka ambayo umewahi kuishuhudia

Nimekuwa shabiki wa soka kwa muda mrefu sana. Kwa muda wa miaka 20 sasa. Nimeangalia mechi nyingi sana na za kutosha, zaidi ya 1000 hadi leo hii.

Toka enzi za goli la dhahabu hadi leo hii ambapo goli la ugenini limefutwa kwenye mashindano ya Ulaya na technolojia ya VAR inatumika.

Nimeangalia fainali 6 za kombe la dunia, toka 2002 hadi 2022. Nimeangalia zaidi ya fainali 14 za Uefa Champions league. Nimeangalia mechi nyingi sana za mashindano tofauti tofauti na zenye matukio ya kusisimua na matokeo ya kustaajabisha....Jaribu kuwaza,,

Nani amesahau kuhusu usiku wa Liverpool dhidi ya Ac Milan 2005?..Je ile comeback ya Barcelona dhidi ya PSG 2017?...vipi kuhusu usiku wa Drogba pale Allianz Arena 2012?....Bila shaka wote tunakumbuka goli la Iniesta lilivyowapa ubingwa Spain mbele ya Uholanzi pale Soccer city kwa madiba....Na vipi kuhusu ile Acrobatic ya Wayne Rooney dhidi ya Man city dakika za kuelekea mwisho kabisa kwenye mechi muhimu ya kuamua bingwa wa EPL 2010/2011...Mungu amlaze pema Cheikh Tiote anayetukumbusha Comeback ya Newcastle dhidi ya Arsenal game ambayo Newcastle wanatoka nyuma kwa bao 4 na kufanya matokeo kuwa 4 kwa 4...vip kuhusu Madrid dhidi ya City UCL mwaka jana?

Hakika kuna mechi nyingi sana ambazo tumezishuhudia na kuzifurahia. Na ambazo zilituacha na kumbukumbu nzuri sana mioyoni mwetu. Lakini pamoja na hayo, kuna mechi moja ambayo kwangu mimi nimeiweka katika kilele cha ubora. Ndiyo, ni Mechi Bora zaidi ya soka ambayo nimewahi kuishuhudia. Unataka kuifahamu?

Usipate tabu, rudisha kumbukumbu zako hadi Jioni ya Tarehe 18.12.2022 pale Qatar...ARGENTINA vs FRANCE....Dakika 120 za dhahabu. Ni mechi kubwa iliyoamuliwa na wachezaji wakubwa katika hatua kubwa ya mshindano makubwa zaidi ya soka duniani.

Kwangu mimi Argentina Vs France ndio mechi yangu bora zaidi ya soka niliyowahi kuishuhudia toka nimeanza kuangalia soka....

Tuambie kwa upande wako, ipi mechi bora kwako!!!
uefa 1998 man u vs bayen bonge la mechi mpaka 90 man u ashakula moja. 90 hyohyo man u anasawazisha. dk za nyongeza ya 92 man u anapiga la 2 kupitia kona ya beckam golin yuko shumaika kwa upande wa man u na upande wa bayan yuko oliver khan hyo mechi sitakaa nisahau.kwa kifupi kikosi cha man u ni dwhite york na pacha wake andy cole, jap stam beki kisiki roy kean mtata kila wakikutana patrick viera wa aseno ligi ya england lazima wazichape sababu wote ni watata.alafu kuna beckham, tedy sherigam,scoles, ole guna sosha, gigs, philip nevo na ndugu yake gary nevo.roy kean,nick but, henning berg na wengine kibao
 
Ile mechi Messi anawapata Real Madrid huku kang'ata plasta mdomoni then anakuja kuwaonyesha jezi yake namba 10
 
...Kassim Manara akiweka mpira ndani ya miguu yake hata mkija 5hamchukui ule mpira,.....George Masatu anafuta magoli kwenye msitari....ohoooo Tanzania tulipotea wapi kama nchi?

Marehemu Gibson Sembuli anapiga mashuti uzito mara 3 ya yale ya Salvatory Edward...

Abeid Mziba akinyanyuka juu kuufuata mpira wa kichwa, watazamaji nasi tunanyanyuka kushangilia mpira unaoelekea kimiani...
 
Galatasaray vs Real Madrid

Tarehe 3 April 2001, zinakutana Gala na Madrid mechi ya mkondo wa kwanza wa robo fainali ya UCL ndani ya Ali Sami Yen, Instanbul...

Hii mechi ilikuwa sio ya kumtuma mtoto dukani kwani ilikuwa imesheheni mastaa kwa kila timu, Gala wakiwa wanaongozwa na mtukutu wa Romania fundi kabisa wa guu la mavi Gheorge Hagi...

Mbavu ya kushoto ya Madrid akiwepo Roberto Carlos kwa mara ya kwanza kushuhudia anakimbizwa muda wote wa mechi pamoja ya kwamba alikuwa ni moja ya mabeki wenye kasi sana lakini alikutana na ustaadh Hakan Sas winga moja teleza na kilichovutia zaidi kwa muonekano wote walikuwa kama wanafanan hivi...

Hadi HT, Gala alikuwa ashakufa bao mbili mtungi, hapo Madrid wakinua wanalipa kisasi cha kuchapwa Super Cup...

Kipindi cha pili kilipoanza tu Gala walipiga mbungi moja hatari sana, wakaanza kwa kuchomoa goli la kwanza kupitia penati ya Umit Davala, Sas akitupia la pili, na striker mmoja hatari sana Mario Jardel mtaalamu wa mipira ya vichwa akiweka kambani bao la tatu na mwisho wa siku game ikaisha kwa Madrid kufa 3 - 2...

Line ups za siku hiyo...

Screenshot_20240214_201847_Chrome.jpg
 
International level : Argentina Vs France, 2022 worpd cup final.

Club level: Bayern Munich Vs Atletico Madrid 2016 UEFA nusu fainali ya pili pale Allianz Arena, baada ya mechi ya kwanza kuisha kwa ushindi wa moja bila kwa Atletico. Wakarudiana pale Allianz Arena, Pep Guardiola akaweka pembbeni mpira wa kihispaniola, akawaacha akina Frank Ribery wapige ule msako wa kijerumani.

Upande wa pili, Diego Simeone alienda na mission moja tu, kupaki bus. Hili ndicho kipindi ambacho Atletico Madrid walikua na defense bora zaidi duniani.

Ulipigwa mpira mwingi sana. Ilikua ni pressure kuanzia dakika ya kwanza, hadi ya mwisho. Bayern walishinda 2-1, ila wakatolewa kwa aggregate.

NB: Comeback ya Barcelona Vs PSG, ilikua ni total domination. Barca iliwazidia PSG kila kitu, ndio maana siioni kama ni mechi bora.
Hiyo game Atletico walipigwa msako kwa hatari upande wa kushoto Douglas Costa alimtesa sana Juanfran lakini yule dingi alizuia Costa hakupiga hata cross za maana.
 
Nimekuwa shabiki wa soka kwa muda mrefu sana. Kwa muda wa miaka 20 sasa. Nimeangalia mechi nyingi sana na za kutosha, zaidi ya 1000 hadi leo hii.

Toka enzi za goli la dhahabu hadi leo hii ambapo goli la ugenini limefutwa kwenye mashindano ya Ulaya na technolojia ya VAR inatumika.

Nimeangalia fainali 6 za kombe la dunia, toka 2002 hadi 2022. Nimeangalia zaidi ya fainali 14 za Uefa Champions league. Nimeangalia mechi nyingi sana za mashindano tofauti tofauti na zenye matukio ya kusisimua na matokeo ya kustaajabisha....Jaribu kuwaza,,

Nani amesahau kuhusu usiku wa Liverpool dhidi ya Ac Milan 2005?..Je ile comeback ya Barcelona dhidi ya PSG 2017?...vipi kuhusu usiku wa Drogba pale Allianz Arena 2012?....Bila shaka wote tunakumbuka goli la Iniesta lilivyowapa ubingwa Spain mbele ya Uholanzi pale Soccer city kwa madiba....Na vipi kuhusu ile Acrobatic ya Wayne Rooney dhidi ya Man city dakika za kuelekea mwisho kabisa kwenye mechi muhimu ya kuamua bingwa wa EPL 2010/2011...Mungu amlaze pema Cheikh Tiote anayetukumbusha Comeback ya Newcastle dhidi ya Arsenal game ambayo Newcastle wanatoka nyuma kwa bao 4 na kufanya matokeo kuwa 4 kwa 4...vip kuhusu Madrid dhidi ya City UCL mwaka jana?

Hakika kuna mechi nyingi sana ambazo tumezishuhudia na kuzifurahia. Na ambazo zilituacha na kumbukumbu nzuri sana mioyoni mwetu. Lakini pamoja na hayo, kuna mechi moja ambayo kwangu mimi nimeiweka katika kilele cha ubora. Ndiyo, ni Mechi Bora zaidi ya soka ambayo nimewahi kuishuhudia. Unataka kuifahamu?

Usipate tabu, rudisha kumbukumbu zako hadi Jioni ya Tarehe 18.12.2022 pale Qatar...ARGENTINA vs FRANCE....Dakika 120 za dhahabu. Ni mechi kubwa iliyoamuliwa na wachezaji wakubwa katika hatua kubwa ya mshindano makubwa zaidi ya soka duniani.

Kwangu mimi Argentina Vs France ndio mechi yangu bora zaidi ya soka niliyowahi kuishuhudia toka nimeanza kuangalia soka....

Tuambie kwa upande wako, ipi mechi bora kwako!!!
Ooh!!! kama ulikuwepo mkuu... Mechi ya fainali kati ya Ufaransa na Argentina ilikuwa ya kukata na shoka... Huku Mbape-the wonder kid, kule Lionel Messi8 the infinity unaweza kumwita hivyo kama unataka-mchawi wa mpira wa miguu yaani duniani na hata mbinguni... "the rest is history".
 
Hii mechi ya fainali kwakweli ilikuwa nzuri sema iliamuliwa na Kolo Mwani aliyekosa goli ye na kipa. Ubora na quality ya mechi iliishia pale.

Unaikumbuka Brazil na Germany fainal. De Lima anampiga Oliver Khan 2 na kumstaafisha international football
 
Nimekuwa shabiki wa soka kwa muda mrefu sana. Kwa muda wa miaka 20 sasa. Nimeangalia mechi nyingi sana na za kutosha, zaidi ya 1000 hadi leo hii.

Toka enzi za goli la dhahabu hadi leo hii ambapo goli la ugenini limefutwa kwenye mashindano ya Ulaya na technolojia ya VAR inatumika.

Nimeangalia fainali 6 za kombe la dunia, toka 2002 hadi 2022. Nimeangalia zaidi ya fainali 14 za Uefa Champions league. Nimeangalia mechi nyingi sana za mashindano tofauti tofauti na zenye matukio ya kusisimua na matokeo ya kustaajabisha....Jaribu kuwaza,,

Nani amesahau kuhusu usiku wa Liverpool dhidi ya Ac Milan 2005?..Je ile comeback ya Barcelona dhidi ya PSG 2017?...vipi kuhusu usiku wa Drogba pale Allianz Arena 2012?....Bila shaka wote tunakumbuka goli la Iniesta lilivyowapa ubingwa Spain mbele ya Uholanzi pale Soccer city kwa madiba....Na vipi kuhusu ile Acrobatic ya Wayne Rooney dhidi ya Man city dakika za kuelekea mwisho kabisa kwenye mechi muhimu ya kuamua bingwa wa EPL 2010/2011...Mungu amlaze pema Cheikh Tiote anayetukumbusha Comeback ya Newcastle dhidi ya Arsenal game ambayo Newcastle wanatoka nyuma kwa bao 4 na kufanya matokeo kuwa 4 kwa 4...vip kuhusu Madrid dhidi ya City UCL mwaka jana?

Hakika kuna mechi nyingi sana ambazo tumezishuhudia na kuzifurahia. Na ambazo zilituacha na kumbukumbu nzuri sana mioyoni mwetu. Lakini pamoja na hayo, kuna mechi moja ambayo kwangu mimi nimeiweka katika kilele cha ubora. Ndiyo, ni Mechi Bora zaidi ya soka ambayo nimewahi kuishuhudia. Unataka kuifahamu?

Usipate tabu, rudisha kumbukumbu zako hadi Jioni ya Tarehe 18.12.2022 pale Qatar...ARGENTINA vs FRANCE....Dakika 120 za dhahabu. Ni mechi kubwa iliyoamuliwa na wachezaji wakubwa katika hatua kubwa ya mshindano makubwa zaidi ya soka duniani.

Kwangu mimi Argentina Vs France ndio mechi yangu bora zaidi ya soka niliyowahi kuishuhudia toka nimeanza kuangalia soka....

Tuambie kwa upande wako, ipi mechi bora kwako!!!
Nikurudishe nyuma kdogo.je, unaikumbuka fainali ya uefa kati ya man u na bayen munich? Tafuta watu wakusimulie ndo utajua ni bonge la mechi enzi za refa kipara colina anatoa kadi huku anakuchekea hyo ilikuwa 1998
 
Brazil vs Italy 1970 in Mexico hii nilishuhudia uwanjani mwenyewe and was my first World cup to attend jamani hii mechi pele kafanya kazi ,sijawah kuona balaa lile tena ,
Brazil alikuwa na watu dah miaka imekwenda.
Rip Pele
 
Uholanzi vs brazil world cup semi final 1998. Mechi kali na Nusu fainali kali sanaaaa iliisha kwa goli 1 - 1 ikaenda penalty
 
Real madrid vs bayer leverkusen UCL final 2002 zizou anapiga bonge la goal
Italy vs German nusu final gemu inaisha iraly 2 german 0 extra time. Sikumbuki kama refa alipuliza filimbi kumaliza huu mpira. Baada ya Delpiero kupiga goli la pili dakika za mwisho kabisa wachezaji wa ujerumani walilala uwanjani kwa maumivu na wengiine wakatoka wenyewe uwanjani. Yaani italy walikuwa na nguvu ya extra time utafikiri walikula viagra. Goli la kwanza alipiga Fabio Groso jezi no 3. Naikumbuka sana hii game japo sikuwa na team hapo
 
Back
Top Bottom