Tuchambue kwa upana Part 1 ya interview ya Jesca Magufuli na Millard Ayo

Tuchambue kwa upana Part 1 ya interview ya Jesca Magufuli na Millard Ayo

Kwan wewe una ndugu wangapi waliopata 4 ila wanasoma vyuo sasa?
Mbona sio maarufu.
Kwanza kabisa umeuliza kwa nini huyo Dada ni maarufu kuliko ndugu zake wengine,
Mimi nimekujibu kuwa sababu ni hiyo skendo ndio ilipelekea.
UMaarufu wake ulianzia hapo.

Sijasema skendo ni ya kweli au lah.

Halafu sina ndugu ambae alipata div 4 na yuko chuo kwa sasa.
 
Ushabiki wa kisiasa pembeni, nafikiri mahojiano haya yametupa taarifa nyingi mpya za maisha binafsi na ya kifamilia ya Hayati Magufuli ambazo zilikua hazifahamiki hapo kabla.

Kipi umejifunza kuhusu hayati Magufuli na familia yake kupitia hii interview?

View attachment 3319560

Binafsi kwa mara ya kwanza nimejua kuhusu;
  • Namna alivyozingatia tamaduni na miiko ya familia kama watoto wake kuja kumsalimia kila siku asubuhi saa kumi na mbili - hata alipokua ikulu.

  • Historia ya jina la Magufuli na kwamba halikua jina halisi la ukoo wao na lilitokana na babu yake aliyekua akicheza ngoma na makufuli 🔒🔓🔐.

  • Picha za vipindi mbalimbali vya maisha yake na mkewe mama Janet, kutotumia vilevi kama pombe na kurudi nyumbani saa kumi na mbili jioni ili kuwa na muda na familia yake. Kuna la kujifunza hapa kwa vijana ambao mmeoa au bado hamjaoa.

  • Sikujua kama mazingira tatanishi ya kifo chake yalileta sintofahamu kwa familia yake pia, baadhi ya watoto na ndugu hawakupata taarifa za msiba mpaka walipoona mitandaoni.

  • Hakua baba wa kudekeza watoto wala kupenda kuwalimbikizia mali. Watoto wake kupewa zawadi za magari ya kawaida kama Toyota Raum na IST hata alipokua Raisi ambaye anamudu kifedha kuwanunulia magari ya kifahari.

  • Hobbies - hata alipokua Raisi, kwenye muda wake binafsi aliendelea kufanya vitu binafsi vya kumfurahisha kama ufugaji wa ng’ombe na kuvua samaki, I hope tunalibeba hilo kama funzo pia.

Tupia yako uliyookota kwenye Part 1 ya interview hii.

Cc:
Aaliyyah , bonjov , makutupora , Half american , To yeye , Poor Brain , ledada
Hakua baba wa kudekeza watoto wala kupenda kuwalimbikizia mali. Watoto wake kupewa zawadi za magari ya kawaida kama Toyota Raum na IST hata alipokua Raisi ambaye anamudu kifedha kuwanunulia magari ya kifahari.
Hapa kwenye magari weeh,apa nimemnyooshea Mikono 😂😂kama huyu jesca anavoshangaa alipewa IST akitegemea atakutana labdah na Discovery,Benz kama Mzee au Land cruiser...ila Mzee aliamini katika falsafa moja ili ufike juu unatakiwa kuanzia chini na hiki ni kitu kizuri Sana tofauti na kuanzia juu ukija chini unaweza Dhani Dunia imekutenga
 
Hata hizo Certificate na Diploma sijaona, maana kamaliza 2011, 2012 anaomba bachelor UDOM.

ndo maana wadau wakahoji inawezekanaje hii, tazama vizuri hapo ktk uzi husika.
Matokeo ni ya 2011 na chuo kamaliza 2019 maan yake alianza 2016. Kwa hiyo sio kwel kwamba alimaliza form 4 halafa akaenda degree moja kwa moja!!
 
Kama kamaliza Chuo kikuu 2019 maana yake alikua na miaka 2 nyuma ya kusubiri kusafisha cheti au kusoma certificate, diploma then degree, la sivyo ingekua 2011 form 4, 2012 na 14 advance then 14 hadi 17 degree. Kuna elimu amechukua alipopumzika sidhani kama kuna namna ilifanyika.
 
Ni maarufu kwa sababu ya skendo ya kupata division 4 "O" level" na kuingia UDOM kusoma.
Hapana, umaarufu aliupata baada ya ku disco UDOM, halafu ujanja ujanja ukafanyika akabaki. Ikiwa baba yake aliwaita wale watoto wa diploma “Vilaza” hawafai kuwepo UDOM wahamishwe vya kati.

Kama alipata division 0 O-level sina hakika.

WaTz mnasahau haraka sana.
 
Baada ya kupata 4 olevel alirudia mtiani then akasoma QT (4&5 mwaka mmoja) then akaingia chuo.
 
Matokeo ni ya 2011 na chuo kamaliza 2019 maan yake alianza 2016. Kwa hiyo sio kwel kwamba alimaliza form 4 halafa akaenda degree moja kwa moja!!
2019 ni masters ndo kamaliza.
 
Lengo siyo kusifia, soma vizuri nyuzi mkuu.

Unaweza kusema mabaya pia uliyoyaona kwenye hayo mahojiano.
Nasema hivyo kwa sababu watu huwa mbaka wanaomba ufufuke eti aje aone kinachoendelea Tz, Sasa huoni kuwa ni tatizo?
Kwa nini wamtumainie mtu mfu? Je kwani Mungu wa kumtumainia hayupo?
 
Ushabiki wa kisiasa pembeni, nafikiri mahojiano haya yametupa taarifa nyingi mpya za maisha binafsi na ya kifamilia ya Hayati Magufuli ambazo zilikua hazifahamiki hapo kabla.

Kipi umejifunza kuhusu hayati Magufuli na familia yake kupitia hii interview?

View attachment 3319560

Binafsi kwa mara ya kwanza nimejua kuhusu;
  • Namna alivyozingatia tamaduni na miiko ya familia kama watoto wake kuja kumsalimia kila siku asubuhi saa kumi na mbili - hata alipokua ikulu.

  • Historia ya jina la Magufuli na kwamba halikua jina halisi la ukoo wao na lilitokana na babu yake aliyekua akicheza ngoma na makufuli 🔒🔓🔐.

  • Picha za vipindi mbalimbali vya maisha yake na mkewe mama Janet, kutotumia vilevi kama pombe na kurudi nyumbani saa kumi na mbili jioni ili kuwa na muda na familia yake. Kuna la kujifunza hapa kwa vijana ambao mmeoa au bado hamjaoa.

  • Sikujua kama mazingira tatanishi ya kifo chake yalileta sintofahamu kwa familia yake pia, baadhi ya watoto na ndugu hawakupata taarifa za msiba mpaka walipoona mitandaoni.

  • Hakua baba wa kudekeza watoto wala kupenda kuwalimbikizia mali. Watoto wake kupewa zawadi za magari ya kawaida kama Toyota Raum na IST hata alipokua Raisi ambaye anamudu kifedha kuwanunulia magari ya kifahari.

  • Hobbies - hata alipokua Raisi, kwenye muda wake binafsi aliendelea kufanya vitu binafsi vya kumfurahisha kama ufugaji wa ng’ombe na kuvua samaki, I hope tunalibeba hilo kama funzo pia.

Tupia yako uliyookota kwenye Part 1 ya interview hii.

Cc:
Aaliyyah , bonjov , makutupora , Half american , To yeye , Poor Brain , ledada
The dark side to such interviews will never be told
 
Back
Top Bottom