Tuelimishane hapa kuhusu hii bahati na sibu ya BIKO

Tuelimishane hapa kuhusu hii bahati na sibu ya BIKO

UKWELI KUHUSU BIKO.....
naitwa geophrey ni mkazi wa arusha siku ya jana nime cheza BIKO jumla ya laki na 70 ,watu wengi tuna amini tuna weza kushinda ma milioni ya pesa 50m hadi 100m,Katika kucheza biko nime jifunza kitu sijui kama ni mawazo yangu.

Huu mchezo mwanzo una kuvutia mwanzoni ili uendelee kucheza kwa mfano kwa siku ya jana nilianza na elf 10 sikushinda nika cheza tena elf 10 nikashinda elf 20 nikacheza elf 20 tena nikashinda elf 50 lakin swali langu kubwa ili kushinda hzo m50 au m100 ina kuaje maana nme kuwa mtumwa nina ndoto za kushinda na nina nafasi 171 katika dro ya j5 na j2
Ulicheza elfu 10, ukala elf 20!
Ukacheza elfu 20, ukala elfu 50!
Kumbe ni rahisi hivooo, basi cheza milion 50, upate milioni 100.
 
Aisee kwa jinsi ambavyo huwa naiona tamu hela yangu sijawahi kujaribu kitu chochote kinachoitwa bahati nasibu. Sababu wanufaika ni wachache kuliko wanaopata hasara na hasara zenyewe walio wengi hawajui kama wanapata hasara kwa kutokana na kudanganywa katika kushinda vihela kidogo ambavyo vimekuwa ushawishi mkubwa wa kumfanya mtu azidi kushawishika.
 
Mkuu mbona haujasema ukweli kuhusu BIKO kama kichwa cha habari kinavyojinasibu?
 
[emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]ndio maana ikaitwa bahati nasibu,ukikosa jua huna bahati.
 
Jumatano na Jumapili Biko humtoa mshindi mmoja, hawa walianza kutoa milioni 10 au 20 hivi kwa kila Jumapili na walipoona faida inazuka haraka wakaweka mara mbili kwa wiki moja na walipoona faida inakuwa kubwa ili kuhamasisha zaidi wakawa wanatoa 50 katikati ya wiki(J5) na mwishoni(J2).
Walipoona kuna faida zaidi na kuna kaushindani kidogo na Tatu mzuka sasa wanatoa one hundred milions.
Anayecheza mpaka laki kwa week au kwa siku namwonea huruma au namwona mjinga.
Bahati nasibu yoyote kabla hujamwaga fedha zako ni vyema ujue mambo haya;
1.Wewe una % za kushinda kwa kila option moja.
2.Je, ni upi muundo wa bahati nasibu unayoicheza? je, ni ya kulana ninyi kwa ninyi au kuna uwezekano mwenye bahati nasibu nayeye akaliwa/akapata hasara? n.k
3.Soma historia ya washindi na uangalie mahali wanakoishi na uangalie kipato chao kabla ya ushindi. Unakuta house girl anashinda na vihela vya kubana kwenye mboga why upoteze malaki?
Huu mchezo ni vyema uwe unacheza angalau mara 2 tu kwa wiki na ucheze kwa dau dogo maana probability za ushindi haziko wazi.
NB:Biko, Tatumzuka n.k wanarusha matangazo ya kawaida na ya live haya yote wanalipia, wao si wajinga. Wanavuna mliions of money na mabaki ndiyo humpa mmoja au watatu.
Karibu Tatumzuka, ni kugumu ila unaibiwa kwa uhalali zaidi maana hata % za kushinda na kushindwa waweza kuzikokotoa.
 
MBONA HAKUNA HATA MMOJA ANAYESEMA AMESHAJENGA TAYARI NYUMBA.
 
si mcha mungu hawa jammaa wanatangaza matangazo meeengi lakini jinsi mshindi anavyopatikana kuna kama na utata kausiri kidogo,kusema watoe washindi mia hamsini ni kuepuka upangaji matokeo.si rahisi kupanga watu 150 kwa muda mchache
au tena wajaribu hiyo milioni 150 wawagawie watu 300 laki tano tano hapo watoe majina ya washindi 300 na namba zao za simu hakika watakua wamejitangaza,lkn wao kutothubutu hili mimi hunitia mashaka sana michezo hii hp bongo,mfano mzuri shinda nyumba ya Shigongo..matangazo mengi na muda mrefu lkn ht siku draw inafanyika hujui ni wapi,lini na wakati gani!
 
Hata maisha ni kama biko,kuna anaetusua leo,kuna wa kesho n.k...bahati nasibu zipo,ni imani yako na zali lako...!!
 
Unapenda kutelezaa?nenda Shamba mkuu..hamna short cut ktk life... Hiyo lak na 70 nngekuwa na mitetea yng 17
 
Back
Top Bottom