Tuendako hali inatisha. Sasa maharage yanakimbilia kilo moja elfu 4 (4,000)

Kilimo ni biashara.
Ndio ni biashara kama biashara zengine ambazo bei ikiwa kubwa watu husema ila wewe biashara ikiguswa uñawaambia wengine nao wawe wakulima.
 
Ndio ni biashara kama biashara zengine ambazo bei ikiwa kubwa watu husema ila wewe biashara ikiguswa uñawaambia wengine nao wawe wakulima.
Watu kusema sio tatizo maana tunasema kila wakati. Ila kushinikiza serikali ishushe bei ni tatizo.
 
Kwahiyo mkuu ulitakaje kwamba watu wasiseme kwamba gharama za chakula kupanda? Kwamba unaona watu hawataki kuona wakulima mkiwa matajiri sasa hivi?
 
Kwahiyo mkuu ulitakaje kwamba watu wasiseme kwamba gharama za chakula kupanda? Kwamba unaona watu hawataki kuona wakulima mkiwa matajiri sasa hivi?
Watu waseme tu ila wasiishinikize serikali ishushe bei. Walalamike kama wanavyolalamika wakilipa ada huko private school, wakinunua mabati, wakilipia matibabu private hosp n.k
 
Kula kitu kingine mkuu si lazima maharage.

Kwanza ulaji wa mara kwa mara wa hayo mazao makabu kunaleta udumuvu, mengi hiwa na sumu kuvu na madawa ya uhifadhi nafaka.
Mimi nashangaa kama maharage kilo ni 4000 si ununue nyama nusu kilo ni 4000 pia? Mbona huko mjini mnaendelea kupiga bia kama kawaida?? [emoji12] [emoji12]
 
Watu kusema sio tatizo maana tunasema kila wakati. Ila kushinikiza serikali ishushe bei ni tatizo.
Nani kashinikiza humu zaidi wewe ukiona uzi wenye kulalamika bei za chakula kuwa juu unaona kama watu hawataki nyie wakulima mjengo maghorofa kwamba mnaona wanawabania ndio maana unakuja na kauli za kuwaambia wengine nao wakalime.
 
Watu waseme tu ila wasiishinikize serikali ishushe bei. Walalamike kama wanavyolalamika wakilipa ada huko private school, wakinunua mabati, wakilipia matibabu private hosp n.k
Kote huko watu hulalamika na hutoa mapendekezo nini kifanyike ila mkiguswa nyie ndio mnakuja na kauli za kuwataka watu wote wawe wakulima.
 
Nani kashinikiza humu zaidi wewe ukiona uzi wenye kulalamika bei za chakula kuwa juu unaona kama watu hawataki nyie wakulima mjengo maghorofa kwamba mnaona wanawabania ndio maana unakuja na kauli za kuwaambia wengine nao wakalime.
Kwani unalalamika ili nn kitokee?
 
Tafuta pesa acha malalamiko, hela huna wewe peke yako usiwajumuishe na wengine ili kujifariji, umaskini huchochea dhambi.
 
Kote huko watu hulalamika na hutoa mapendekezo nini kifanyike ila mkiguswa nyie ndio mnakuja na kauli za kuwataka watu wote wawe wakulima.
Wenye njaa sababu ya kutaka mwingine anyang'anywe ili washibe huwa hawalalamiki ila wanashinikiza.

Unataka kudanganya kuwa aliye na njaa sababu mkulima kagoma kumlisha na aliyekosa ela ya kulipa ada private school wote wanalalamika? Hapana, kuna mmoja anashinikiza sababu hana option zaidi ya huyo mkulima kunyang'anywa apewe ale ashibe. Huyu mwenzake wa private school atalalamika yakimshinda atapeleka government.
 
Kazi ya kilimo Ni sawa na kuwa Mwalimu unabidi kujitoa Sana malipo atalipa Mungu.
Hapa sijaelewa. kilimo kinacho toa mavuno yanayo weza kutoa Cha kula chakaya, nakubakisha chakuuza , ni kilimo biashara.
Kilimo hicho kinaitaji pesa kati kahatua zifuatazo;
A: Kukodi shamba
B:kulima kwa tractor 🚜 au kwa ng'ombe
C : Kununua mbegu
D:kupanda
E: mbolea za kipandia
F😛arizi
G:mbolea za kukuzia
H:dawa zawadudu
l:kuvuna
J: kusafirisha kupereka mavuno Sokoni.
Hatua zote hizi, ikirukwa moja nikilio kwa mkulima.

Kumbuka wakulima wengi hawana mitaji .
Ili kuendesha shughuli hizo hadi kufikia mavuno wamekopa Tena Mikopo umiza
Inavyo tokea sababu yoyote yakuwakwamisha kupata Bei, ujue ni maandalizi ya kuwakataza kulima msim unao fuata. Wakati Bei ya mpunga na mahindi imepromoka ,hakuna alie jiangaisha na mkulima.
Mbolea zikapanda watu wa kaka kimya . Ile kuja kushituka wanarusu soko la nje tayali tulisha cherewa.
Mvua Nazo zikakata.
Kumbuka huu ukame , hauko Nchini mwetu TU, uko Somalia , sudani kusini na vipande vya Kenya. Kwa Khali hiyo mkulima atafanyaje?
Kazi ya kilimo Ni sawa na kuwa Mwalimu unabidi kujitoa Sana malipo atalipa Mungu.
 
BEI IMEKUWA NZURI KWELI HAKIKA KILIMO SASA NI DILI TWENDENI TUKALIME TUJE KUFAIDI BEI HII NZURI AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA.
N. B, badala ya kukiwahi kilimo, tufaidi tunalalama.
Wala usilime,tafuta mtaji msimu wa mavuno nunua kama umepagawa

Kipindi kama hiki unauza kwa bei uitakayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…