Tufanye nini na hizi clip zinazopotosha Historia ya Tanzania?

... Mzee, fasihi ulisomea wapi wewe?
 
Hapo kwanza ncheke. Mzee unalalamika kukosewa adabu kuitwa Mudi kifupi cha Mohammed huku wewe ukiwa ni bingwa wa kufupisha majina ya watu humu.

Mfano tu hapo Lukubuzo unayemlalamikia umemwita Luku.. ni ni unatakataa na nini unafanya?
Tai...
Nimefupisha Luku.

Yeye kama anataka kufupisha inatakiwa aandike "Moh" si Mudi.

Umefanya haraka kucheka.
Umefanya haraka sana kunijibu.

Kabla hujaandika unatakiwa kusoma kwa utulivu uelewe ndipo unajibu.

Kama ni swali la mtihani umekosea.
Ushapoteza alama.

Kama usaili wa kazi...
 
WEKA HIYO CLIP HAPA. ILI ISIONEKANE MANENO MANENO YA KILA SIKU. WEKA CLIP HAPA IJADILIWE.
 
... Mzee, fasihi ulisomea wapi wewe?
Dudus,
Sidhani kama ni fasihi peke yake.
Nimepita na madrasa.

Madrasa wanafunza mengi sana kwa mtindo tofauti na shule.

Huwezekana sababu ni hiyo.
Kwa nini umeniuliza?
 
So issue hapa ni kuwa Kuna Dini nyingine haijatajwa? Hivi ikitokea mimi nimeandaa Documentary nikasema team kubwa Yanga. Nyie wa Simba mnakuwa mmeondoshwa au mnaanza kukosa kitu gani katika maisha? Maana malalamiko mengine tusionekane tu tuna asili ya kulalamika. Hii Wakristo wakijitaja inawakosesha nini Waislamu? Hawataenda Mbinguni? Dini yao itafutika?
 
Mtu ukiwa na roho ya ulalamishi mwishowe unadharaulika tu maana unalalamika hata visivyo na maana. Hiyo documentary imetaja watu maarufu ambao wengine hata siwafahamu. But siwezi anzisha uzi kulalamika. SIYO DOCUMENTARY YA SERIKALI. SIYO RASMI. BUT SIONI CHA KULALAMIKA KILA WAKATI. MALALAMIKO YAMEKUWA MENGI SANA MPAKA SASA MTU UNADHARAULIKA.
 
Yaani Babu yangu mzee Mohammed kwa udini wewe huwezekani na bahati mbaya umeshazeeka hata kushaurika ni ngumu.

Mungu akusaidie utambue thamani ya watu kupitia utu wao na sio dini maana hakuna namna unaweza shauriwa kwa umri wako huo.
Dp...
Kwa umri wangu wa miaka 71 wewe ni mwanangu.

Kikwetu mimi nikikuchukua kama mjukuu nitakuwa nimekupandisha daraja ya kuweza hata kunikalia kichwani.

Kwa ajili hii basi una haki ya hata kunifanya mimi babu yako kichekesho.

Huu utangulizi nia yake ni kukuweka mahali pako kama mwana ili uwe na adabu kwangu.

Ikipatikana adabu tutafanya mjadala wenye tija.

Udini kuandika "corrective political history ya Tanganyika?"

Au kwako hii ni dini?

Swali la umri halina uhusiano na historia ya uandishi wangu kwani nimeanza kuandika nikiwa kijana na walitokea watu kupingana na mimi.

Naamini tumeelewana.
Angalia picha hiyo katika makala yangu katika New African (London):


 
Na hujakosoa kuwa lugha kuu Kiarabu kimo. Badala ya Kiswahili na Kiingereza. Maana ndiyo Lugha zenye wazungumzaji wengi. Hilo hukuona kuwa ni kosa. Ile video nadhani wametengeneza makusudi kupima uelewa wa watu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mtu...
Inawezekana huoni mambo nionavyo.
Kweli wewe huoni tatizo katika hiyo clip.

Mimi na wengine wengi tumeona tatizo katika clip hiyo.

Watu wamepishana katika ufahamu.
Mimi sijalalamika.

Rejea niliyoandika.
 
Mtu...
Kawaida yangu ni huwa siandiki kila kitu.

Hupenda kuandika kile ninachokiona muhimu.

Unisamehe kwa hili.
 
Siku zote history huandikwa na wanaotawala hakuna historia sahihi asilimia 100%
Sidhani Kila mtu aliyepigania uhuru amendikwa kwenye kitabu cha historia na cha msingi watanganyika kwa umoja wao ndio waliodai Uhuru haijalishi sana dini.
Sasa kwa Nini unataka kubinafisisha hii history iwe ya waislam peke Yao?
 
We niwa kupuuzwa. Waislam walikuwa taasisi ipi iliyotaifishwa na serikali? Taasis zilitaifishwa ni za kanisa. Mkapa aliwapa waislamu chuo cha TANESCO Morogoro bure kabisa ndio chuo kikuu pekee cha waislamu. Waislamu hawana uwezo hata wa kujenga chuo chao. Niambie zaidi ya kile chuo kikuu chenu qameongeza nini. Hata kufungua tawi Dsm wameshindwa. Ni watu wavivu, walalamishi, wa kupenda kupendelewa.
 
Mtu...
Kawaida yangu ni huwa siandiki kila kitu.

Hupenda kuandika kile ninachokiona muhimu.

Unisamehe kwa hili.
Mudi, nilikupa tu mfano wa makosa makubwa mengi katika hiyo makala. But mi sijaona la kuhangaika nalo. Mi kuna mambo nasema hayana haja ya kuumiza kichwa na kulalamika lalamika kila wakati.
 
Gambo...
Una hakika kuwa ''siku zote'' historia inaandikwa na wanaotawala?

Zipo historia na ni nyingi ambazo zimeandikwa na watu huru.

Huwezi kuandika ''kila mtu'' lakini wapo ambao wakiachwa watu watauliza.

Unaweza kuandika historia ya TANU bila kumtaja Sheikh Hassan bin Ameir?

Sijabinafsisha historia ya TANU kuwa ya Waislam peke yao.
Waislam walifutwa katika historia ya uhuru.

Mimi nimewarejesha.

Nimewarejesha si Waislam tu bali na wengine ambao na wao pia walifutwa.

Mfano wa Denis Phomgeah, Dome Okochi Budohi, Clement Mtamila, Dr. Michael Lugazia, Dr, Vedasto Kyaruzi, Dr. Luciano Tsere kwa kuwataja wachache.

Haya ndiyo yaliyofanya kitabu hiki kivutie wasomaji wengi.


Dr. Luciano Tsere


Denis Phombeah

 
Eti!? Huyu Kleist asili yake ni wapi!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…