Tuhuma za JWTZ kupiga raia huko Kawe: Tunaomba Waziri wa Ulinzi ajitokezee kukemea, kulaani, na kukataza jeshi kujichukulia sheria mkononi

Mtoa maada umeandika ujinga pia waao changia. Hawafikiri vizur. Hakuna sababu yeyote inayo kupa haki ya kuu.huo ni uasi
Nimeandika ujinga kivipi mkuu na wakati umeshasema hao sojaz wenyewe hawafikirii vizuri?
 
Sasa sio kibali cha kuua raia inchi inaongozwa kwa sheria...inabidi kuwe tofauti ya JWTZ na Hamas
Kweli mkuu, nchi ina sheria, nchi ina mahakama na wanasheria wa kusimamia sheria.

Hivyo hao sojaz walitakiwa wafuate sheria, badala ya kupiga watu hovyo na kujichukulia sheria mkononi.
 
Kweli mkuu, nchi ina sheria, nchi ina mahakama na wanasheria wa kusimamia sheria.

Hivyo hao sojaz walitakiwa wafuate sheria, badala ya kupiga watu hovyo na kujichukulia sheria mkononi.
Afrika siyo sehemu ya kuendekeza saaana kufuata Sheria.....Ni kipigo tuu....Sasa wewe mwanao mnyime kipigo ufuate sheria.

Raia za Afrika wakati mwingine wanaelewa kwa kipigo
 
Kweli mkuu, nchi ina sheria, nchi ina mahakama na wanasheria wa kusimamia sheria.

Hivyo hao sojaz walitakiwa wafuate sheria, badala ya kupiga watu hovyo na kujichukulia sheria mkononi.
That's murderous at highest order....anyway utashangaa wamepandisha vyeo kesho ...tunaongozwa na lichama chakavu
 
Sahau kama kuna waziri au hata Rais wa nchi anayeweza kujitokeza hadharani akalikemea jeshi. Siyo Tanzania tu, dunia nzima.

Sana watakaa chini na wakuu wa jeshi, yamalizwe kidiplomasia. Usiwe na wasiwasi.
Kikwete alikemea na alifanikiwa kumaliza uhuni huu.
Magufuli alikuta jeshi lenye nidhamu akaendeleza alipo achia Mwamba Kikwete.
Tunayasikia sasa yanajirudia mambo ya awamu ya Mkapa kurudi miaka ya nyuma.
 
Afrika siyo sehemu ya kuendekeza saaana kufuata Sheria.....Ni kipigo tuu....Sasa wewe mwanao mnyime kipigo ufuate sheria.

Raia za Afrika wakati mwingine wanaelewa kwa kipigo
Tatizo wanapiga watu ambao hawakuwepo na wengine hawafahamu kilichotokea.
 
Kikwete alikemea na alifanikiwa kumaliza uhuni huu.
Magufuli alikuta jeshi lenye nidhamu akaendeleza alipo achia Mwamba Kikwete.
Tunayasikia sasa yanajirudia mambo ya awamu ya Mkapa kurudi miaka ya nyuma.
Hata Husein Mwinyi aliweza kusimamia nidhamu kwa jeshi enzi zake alipokuwa waziri wa ulinzi.
 
Pole sana,
Nimesikitishwa sana na taarrifa hizi, nimefedheheshwa sana na askari wetu kwa hatua walizochukua dhidi ya raia huko kawe.
Naomba utulivu na subiira kidogo ili kujiridhisha na hatimae, niwahakikishie, hatua kali stahiki za kijeshi zitachukuliwa dhidi ya wote watakao thibitika kushiriki aibu hii...
 
We dogo, acha kuleta utani kwenye mambo serious basi
 
Askari wa Jeshi la Wananchi waheshimu Raia kwani ndio walipaji wa mishahara yao, hali kdhalika Wananchi wawaheshimu Askari wa Jeshi LETU la Wananchi kwani ndio walinzi wetu wa Mipaka na HESHIMA ya TAIFA letu.
Naunga mkono hoja hii kila mmoja asimame kwenye nafasi yake.

Hakuna nafsi inapenda kuonewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…