Tuhuma za JWTZ kupiga raia huko Kawe: Tunaomba Waziri wa Ulinzi ajitokezee kukemea, kulaani, na kukataza jeshi kujichukulia sheria mkononi

Tuhuma za JWTZ kupiga raia huko Kawe: Tunaomba Waziri wa Ulinzi ajitokezee kukemea, kulaani, na kukataza jeshi kujichukulia sheria mkononi

Mtoa maada umeandika ujinga pia waao changia. Hawafikiri vizur. Hakuna sababu yeyote inayo kupa haki ya kuu.huo ni uasi
Nimeandika ujinga kivipi mkuu na wakati umeshasema hao sojaz wenyewe hawafikirii vizuri?
 
Sasa sio kibali cha kuua raia inchi inaongozwa kwa sheria...inabidi kuwe tofauti ya JWTZ na Hamas
Kweli mkuu, nchi ina sheria, nchi ina mahakama na wanasheria wa kusimamia sheria.

Hivyo hao sojaz walitakiwa wafuate sheria, badala ya kupiga watu hovyo na kujichukulia sheria mkononi.
 
Kweli mkuu, nchi ina sheria, nchi ina mahakama na wanasheria wa kusimamia sheria.

Hivyo hao sojaz walitakiwa wafuate sheria, badala ya kupiga watu hovyo na kujichukulia sheria mkononi.
Afrika siyo sehemu ya kuendekeza saaana kufuata Sheria.....Ni kipigo tuu....Sasa wewe mwanao mnyime kipigo ufuate sheria.

Raia za Afrika wakati mwingine wanaelewa kwa kipigo
 
Kweli mkuu, nchi ina sheria, nchi ina mahakama na wanasheria wa kusimamia sheria.

Hivyo hao sojaz walitakiwa wafuate sheria, badala ya kupiga watu hovyo na kujichukulia sheria mkononi.
That's murderous at highest order....anyway utashangaa wamepandisha vyeo kesho ...tunaongozwa na lichama chakavu
 
Sahau kama kuna waziri au hata Rais wa nchi anayeweza kujitokeza hadharani akalikemea jeshi. Siyo Tanzania tu, dunia nzima.

Sana watakaa chini na wakuu wa jeshi, yamalizwe kidiplomasia. Usiwe na wasiwasi.
Kikwete alikemea na alifanikiwa kumaliza uhuni huu.
Magufuli alikuta jeshi lenye nidhamu akaendeleza alipo achia Mwamba Kikwete.
Tunayasikia sasa yanajirudia mambo ya awamu ya Mkapa kurudi miaka ya nyuma.
 
Afrika siyo sehemu ya kuendekeza saaana kufuata Sheria.....Ni kipigo tuu....Sasa wewe mwanao mnyime kipigo ufuate sheria.

Raia za Afrika wakati mwingine wanaelewa kwa kipigo
Tatizo wanapiga watu ambao hawakuwepo na wengine hawafahamu kilichotokea.
 
Kikwete alikemea na alifanikiwa kumaliza uhuni huu.
Magufuli alikuta jeshi lenye nidhamu akaendeleza alipo achia Mwamba Kikwete.
Tunayasikia sasa yanajirudia mambo ya awamu ya Mkapa kurudi miaka ya nyuma.
Hata Husein Mwinyi aliweza kusimamia nidhamu kwa jeshi enzi zake alipokuwa waziri wa ulinzi.
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Ndugu wanaJF wenzangu, nafikiri wengi wetu hapa JF tumesikia, tumesoma na wengine kuona kile kinachosemekana kufanywa na jeshi letu, ambalo tumelipa jina la "Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Jeshi hilo tulilipa jina hilo kwa kuamini kwamba, jeshi hilo limeundwa kwa ajili ya kumlinda, na kumpigania mwananchi wa Tanzania.

Lakini pia liliundwa kwa ajili ya kuilinda mipaka ya Tanzania, pamoja na viongozi wa Tanzania akiwemo raisi wa nchi (ambae ni amiri jeshi wao mkuu) mawaziri, wakuu wa mikoa na viongozi wengine mbali mbali. Hilo ndio lilikuwa lengo la kuundwa kwa jeshi hilo, lkn pia kupewa jina hilo (JWTZ)

Sasa inashangaza sana jeshi ambalo lingewalinda na kuwapigania wananchi, ndio linageuka kuwa jeshi la kuwapiga hovyo wananchi, kuwatesa wananchi na hata wengine kuwauwa wananchi bila sababu za msingi.

Yes tunajua kwamba kila binadamu ana mapungufu yake, hivyo wapo wananchi wanaofanya makosa, au mambo mabaya kwa jeshi letu. Lakini kuna sheria na mahakama ambavyo vinaweza kutumika kuwaadhifu wale wanaofanya mambo mabaya kwa jeshi letu, na sio jeshi hilo kukimbilia tu kujichukulia sheria mkononi mpaka kupelekea maafa kama yaliotokea Kawe na kwengineko.

Malalamiko ya wananchi au raia dhidi ya jeshi hayakuanza leo, ila cha kushangaza badala ya kumalizwa kwa njia ya amani, ndio yanazidi kuongezeka kwa njia za kuchochewa na jeshi hilo hilo lililopewa dhamana ya kutulinda.

Kwa kilichotokea juzi huko Kawe, nafikiri viongozi wengi wa kiserikali wanalifahamu, lkn kwa vile pengine sio wahusika wakuu wa maswala ya kiusalama ndio maana hawahitaji kuliingilia swala hili.

Hivyo sisi wananchi tunamuomba waziri husika wa ulinzi mama yetu Stergomena Tax, pamoja na waziri wa mambo ya ndani brother Masauni waingilie kati swala hili kwa kuonya, kulaani na kutolea maelezo swala husika.

Msingoje mpaka raisi aje kulizungumzia mwenyewe, na wakati nyinyi kama mawaziri mmepewa dhamana ya kutulinda.

Kwa niaba ya wananchi wanyonge, ni mimi mpigania haki zao Mr Dudumizi wa somewhere in Kawe.
Pole sana,
Nimesikitishwa sana na taarrifa hizi, nimefedheheshwa sana na askari wetu kwa hatua walizochukua dhidi ya raia huko kawe.
Naomba utulivu na subiira kidogo ili kujiridhisha na hatimae, niwahakikishie, hatua kali stahiki za kijeshi zitachukuliwa dhidi ya wote watakao thibitika kushiriki aibu hii...
 
We dogo, acha kuleta utani kwenye mambo serious basi
 
Back
Top Bottom