Tuhuma za JWTZ kupiga raia huko Kawe: Tunaomba Waziri wa Ulinzi ajitokezee kukemea, kulaani, na kukataza jeshi kujichukulia sheria mkononi

😀😂😂😂

Hakika wewe unafaa kupewa nafasi aliyonayo waziri wetu wa ulinzi leo.
Ingawa umeigiza, lkn umeonesha uthubutu wa uongozi kupitia kauli yako.
 
Cha mkunjo ndio nini?
 
Mbaya zaidi wanalipa kisasi kwa kila aliyeko mbele yao, ina maana hata wangekutana na dingi yako anatoka misele wangekata funua tu. 🤣 🤣 🤣
Just imagine wakikuta mzee anatoka kutafuta riziki ya watoto wake wanakula ugoko.

Wakikuta bibi katoka feli kununua samaki ili akakaange auze kwa ajili ya kujipatia riziki ya kusomesha watoto na wajuu zake jamaa wanaondoka na ndoo ya samaki huku bibi akishushiwa kipigo cha mbwa mwizi.

Afu linatokea jitu kuwatetea hawa wavunja sheria.
 
Ni heri wachukuliwa hatua Hata kijeshi , ikiwezekana waachishwe kazi mana wamekosa nidhamu na wako above the law, kwa walichokifanya inaweza chochea kwa chuki mtaani na kuwindana
Kweli mkuu, na sio wahusika kuchukuliwa hatua tu, bali pia wawaombe radhi waathirika wote wa tukio lile kwa kipigo na unyama waliowafanyia.
 
Kaeni.kimya acheni kuchochea msivyojua,haya mambo humalizwa kimya kimya bila kelele za media!!

Msifikiri Kila jambo huwa ni la kisiasa eti lazima watu wasikie!!

Tutulie!
Kwahiyo mfano mzazi wako au wewe mwenyewe ungekuwa unatoka zako town haujui hili wala lile unashuka tu kwenye basi unakumbana na jamaa wanaanza kukupiga huku na kule bila sababu wala kukuuliza chochote ungekaa kimya et kwa sababu hili sio swala la kisiasa?

Kila binadamu nchini au duniani ana haki zake za kuishi kwa amani na usalama. Haiwezekani mtu haujui kilichotokea na wala haukuwepo eneo la tukio, ghafla tu unavamiwa na kuanza kupigwa hovyo kichwani miguuni na sehem zingine mbali mbali za mwili bila kuulizwa chochote. Na hata ukiulizwa kama jambo haulijua na haukuwepo kwenye eneo la tukio, humjui muuaji wala alieuwawa unafikiri utajibu nini?
 
Hiyo kambi ya kawe ihamishwe iende Mbali na makazi ya watu!
Ndio msaada pekee!

Saikolojia ya wanajeshi sio sawa kwa raia!

Huo unaouona na hiyo Hali waliyonayo ndio inatufanya tuwe na amani hadi leo mkuu!!

Hao jamaa watengewe makazi yao nje ya mji kabisa!!

State of mind ya mjeda ni tofauti sana na hiyo uliyonayo!
Hivyo tu na Tena kama wamefiwa na mtu wao ndio kabisaa nawashauri Wana kawe wahamie huku mikoani kwa muda!!
 
Daaah anyway mwamba ninamfahamu hakuwa na makuu likizo alikuwa Singida Manyoni, kwao ni Jirani na Makazi yangu ya zamani.

Pumzika Afisa , ukweli wa Jambo anaujua Mungu tu.

Yanayosemwa huku kuwa yalikuwa mabishano ya mpira eti?
Hapana mkuu sababu iliyosababisha kifo chake haikuwa mpira, bali ni kaubabe fulani, si unajua jeshi ni jeshi tu hata awe mpole vipi, lkn anakuwa na karoho fulan ka tofauti ni sisi raia wa kawaida.

Afisa alikuwa ameenda mtaa fulan kupoza koo na familia yake. Sasa akawa amepaki gari yake vibaya (ameziba njia kiaina), huku akiongea na simu kabla ya kushuka.

Wakati huo kuna dogo alikuwa anatoka zake huko na bajaj yake akakuta afisa amepaki gari mazingira mabaya, ikabidi dogo amfuate ofisa amwambie asogeze gari yake kidogo pembeni ili yeye apite kwenda kwenye mambo yake.

Ofisa alipoambiwa vile akaona ni dharau kwa dogo tena raia wa kawaida kumfundisha yeye namna ya kupaki. Akaanza kumwambia dogo kama ana haraka zake basi ageuze akatafute njia nyingine ya kupita, majibizano ya hapa na pale yakaanza. Afisa akamchapa dogo makofi ya haja. Dogo nae kutokana na maumivu, pamoja na hasira ya kufedheheshwa mbele ya watu kwa kupigwa vibao ndo akachomoa cha mkunjo na kumshambulia afisa kisha kutokomea kabla ya kukamatwa.
 
Afrika siyo sehemu ya kuendekeza saaana kufuata Sheria.....Ni kipigo tuu....Sasa wewe mwanao mnyime kipigo ufuate sheria.

Raia za Afrika wakati mwingine wanaelewa kwa kipigo
Usingeandika huu ujinga wako kama hao wajinga wangevamia kwenu ,wakaanza kumpa kisago baba yako na mama yako na kuwajeruhi na wewe wakakupasua bila kosa lolote mlilofanya .
Unaandika huu upuuzi kwa vile sio wewe uliyekutwa na hili .
Jaribu kutumia akili badala ya makalio kabla ya kuandika comment
 
Ushauri uliotoa ni mzuri sana mkuu. Lakini nafikiri ni vigumu mno kuhamisha kambi. Maana hii kambi ni ya muda mrefu sana.

Asilimia kubwa ya raia wameukuta kambi ya jeshi. Lkn pia ugomvi umetokea nje au mbali ya kambi. Hivyo sababu ya tukio sio watu kuishi karibu na kambi, bali ni kale kaubabe fulan ka kijeshi jeshi kama ulivyosema saikolojia ya hawa jamaa.

Nafikiri sasa ni muda wa serikali kuzuia watu kununua viwanja na kujenga maeneo yalio karibu na kambi za jeshi. Lkn pia serikali isichoke kuendelea kuwafundisha nidhamu, upendo na mshikamano kati ya raia na jeshi. Najua na wao ni watu, hivyo wapo ambao watakuwa wanaguswa na kile wanachofundishwa na kukizingatia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…