Wilderness Voice
JF-Expert Member
- May 19, 2016
- 921
- 1,649
Marekani na baadhi ya nchi za dunia ya kwanza kama wanavyojiita wao, uwataja washukiwa wote wanao shiriki biashara za madawa ya kulevya, bila hata kufikishwa mahakamani. Mahakama haipo kukutuhumu, bali unaweza kupewa tuhuma kisha mahakama ndo itaamua kama tuhuma hizo ni kweli au si kweli.Swala la kuwataja washukiwa ni kinyume na kanuni za kimaadili, ila ukweli wa kuhusika kwa waliotajwa nalo ni jingine.
Kwa sheria zote za jinai Tanzania wanaofikishwa mahakamani uwa ni watuhumiwa si wakosaji. Watakuwa wakosaji mara mahakama inapothibitisha. Ni mara ngapi majambazi wamekamatwa kwa kushukiwa kufanya tukio la ujambazi?
Au ni mara ngapi watu wamekamatwa kwa kushukiwa tu kuuwa?
Uwezi subiri umshike mfanya biashara wa madawa kwa kumkuta na madawa. Huyu kamishina anatetea baadhi ya vigogo maarufu wafanyao hiyo biashara. Kwa mwendo huu tusahau vita dhidi ya madawa ya kulevya. Ni ubabaishaji tu! Hata Rais mwenyewe yupo kimya simsikii kakemea au kuongelea.