Tuhuma za Madawa ya Kulevya: Kamishna Jenerali wa DCEA akosoa utaratibu alioutumia Makonda

Swala la kuwataja washukiwa ni kinyume na kanuni za kimaadili, ila ukweli wa kuhusika kwa waliotajwa nalo ni jingine.
Marekani na baadhi ya nchi za dunia ya kwanza kama wanavyojiita wao, uwataja washukiwa wote wanao shiriki biashara za madawa ya kulevya, bila hata kufikishwa mahakamani. Mahakama haipo kukutuhumu, bali unaweza kupewa tuhuma kisha mahakama ndo itaamua kama tuhuma hizo ni kweli au si kweli.

Kwa sheria zote za jinai Tanzania wanaofikishwa mahakamani uwa ni watuhumiwa si wakosaji. Watakuwa wakosaji mara mahakama inapothibitisha. Ni mara ngapi majambazi wamekamatwa kwa kushukiwa kufanya tukio la ujambazi?

Au ni mara ngapi watu wamekamatwa kwa kushukiwa tu kuuwa?

Uwezi subiri umshike mfanya biashara wa madawa kwa kumkuta na madawa. Huyu kamishina anatetea baadhi ya vigogo maarufu wafanyao hiyo biashara. Kwa mwendo huu tusahau vita dhidi ya madawa ya kulevya. Ni ubabaishaji tu! Hata Rais mwenyewe yupo kimya simsikii kakemea au kuongelea.
 
Makonda kipindi hiki cha Kamishna Lyimo sijui kama atadhubutu kuchezea hii mamlaka inayotusaidia kudhibiti mawada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…