DOKEZO Tuhuma za mauaji kwa mmiliki wa kampuni ya KOPAGAS, Andron Mendez

DOKEZO Tuhuma za mauaji kwa mmiliki wa kampuni ya KOPAGAS, Andron Mendez

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ndiyo maana hawa jamaa wa MGas huduma imekuwa mbovu sana, kuishiwa gas walikuwa wanakuletea kabla haijakata sasa hivi inakata ndiyo wanaoleta,

Wateja kibao wanataka huduma ila vifaa hawana.

Kifupi ufanisi umepungua
Si amemwaga damu ya asiyekua na hatia!!!
Kampuni itafunga virago Kabla Mende hajahukumiwa.
Polisi wa Tanzania wako vizuri, wanakula pesa yako wee, mwisho wa siku wanakutelekeza.
Ngoja polisi waneemeke kwanza.
 
Wengi huwa nawashauri kuwa shika bunduki tu kama ni sehemu ya kazi yako. Lakini vijana wana miliki bunduki kama alama ya mafanikio, nguvu na umaarufu.

Maishani mwangu sijamuona aliyemiliki bunduki ikamsaidia wakati "Wazee Wa Kazi" wamefika kuchukua chao.

Wengi wanaishia ku- misuse kama vile lililompata Ramadhan Ditopile Mzuzuri pale Njia Panda ya Kawe.

Kama Andron angekwenda bila bunduki pengine angemzaba kibao huyo mlinzi, kisha kugundua kuwa aliyempiga kibao siyo mlengwà, angemuomba samahani na kumpa hata Tsh Elfu 50 kufuta machozi.
Mbali na chuki zako juu ya JPM, leo umenena hoja nzuri sana Chifu [emoji120]
 
Hii kesi niliisikia sikia siku za nyuma hapa, kuna dada mwansheria naona ndiye anaifuatilia kumbe kesi ndio hii daaah hapo mambo ni mazito sana. Kwa sababu mkurugenzi anaonekana kabisa katenda makosa.
 
Mkuu, kifungu cha 114 cha Penal Code, Cap 16 R.E 2022 kina sub-section 4 na paragraph kibao, kwa usahihi wa kuzuia 'upotoshaji' niambie specific kifungu husika kwa ukamilifu.

Kifungu namba 114 (1) (d)

(d) while a judicial proceeding is pending, publishes, prints or makes use of any speech or writing, misrepresenting the proceeding, or capable of prejudicing any person in favour of
or against any parties to the proceeding, or calculated to lower the authority of any person before whom that proceeding is being had or taken.

Adhabu ya kosa hilo hapo juu iko katika kifungu namba 114(1) (k)
 
Mkuu jamaa anachanganya kujadili mwenendo wa kesi iliyopo mahakamani na kujadili tukio ambalo tayari lina kesi mahakamani, hivyo ni vitu viwili tofauti. Hakuna kosa la jinai kwa mtu kujadili tukio ambalo tayari lina kesi mahakamani. Kwa mtazamo wa jamaa basi hata mawakili na wateja wao wanapojipanga kwa ajili ya kutoa ushahidi wanakuwa wanatenda kosa la jinai, maana wanajadili kesi iliyopo mahakamani.

Kifungu alichotaja kinaeleza kuhusu uchapaji wa mwenendo pasipo ruhusa ya mahakama, kuonyesha dharau kwa mahakama, kuzuia utendaji kazi wa mahakama, kumsema shahidi kwa nia ya kumharibia hadhi kwenye kesi nk..hakuna kinapozuia kujadili matukio yaliyopelekea kesi kama hivi tunavyojadili

Kujadili kesi iliyopo mahakamani unajua madhara yake?
 
Ndo madhara ya kuamini nguvu za giza katika maisha ya utafutaji. Kama sio mara ya kwanza basi uwatoa kafara
 
Hapo wasambaa watapewa pesa watakaa kushoto. Kesi itaisha. Ukiona tajiri jela jua kakosana na mamlaka.
Kosa la zumarid ni kutokuwa na connection kama wafanyavyo wamimina mafuta.
 
Kwenye tuko lenywewe mke wake hakuwepo. Inasemekana alikuwa baada ya tukio, ila gari ndio iliondoka na huo mwili. Anyways, jamaa alijaribu mpaka kubadilisha namba ya gari, akajaribu na kuuza hilo gari; too bad.

Pombe na Bunduki sio combination nzuri
Pombe na bunduki havina tatizo.
Tatizo ni kichwa cha mmiliki wa hiyo combination.
Watu tuna hiyo combination mwaka wa 30 huu na marafiki zetu wa karibu hawajawahi kuona hiyo manati ya mzungu wala kujua kama tunazimiliki.

Narudia tena, pombe sio mbaya, tatizo ni kichwa cha mnywaji pombe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kifungu namba 114 (1) (d)

(d) while a judicial proceeding is pending, publishes, prints or makes use of any speech or writing, misrepresenting the proceeding, or capable of prejudicing any person in favour of
or against any parties to the proceeding, or calculated to lower the authority of any person before whom that proceeding is being had or taken.

Adhabu ya kosa hilo hapo juu iko katika kifungu namba 114(1) (k)
Tafsiri ya hiki kifungu kinaelezea mambo yasiyotakiwa kufanywa yanayoathiri mwenendo wa kesi (judicial proceeding), sasa mfsno mimi nikisema Sabaya alimpiga mfanyabiashara makofi, nayasema hayo kwa kuwa nilikuwepo eneo la tukio, ila napoyasemea sio mahakamani na wala mimi sio miongoni mwa mashahidi mahakamani, na ninaisema hiyo sio kwa kuangalia mahakamani kumerekodiwa nini, ninakuwa ninaathiri vipi kesi hiyo?? Wapi nazuiwa kuzungumza hivyo?
 
Back
Top Bottom