Ni wazi ana mfadhaiko, wasi wasi na majuto makali sana hasa baada ya wanaojaribu kutetea ufisadi wake ndani ya chadema kukosa ushawishi na hoja zenye mashiko za kumsafisha na tuhuma hizo za ufisadi. Ni wazi anajiona na anahisi ana hatia, na hana tena nguvu na uhalali wa kuendelea kua kiongozi wa kitaifa wa chadema.
Mbaya zaidi,
makundi yaliyojipanga vizuri sana kumlipua kwa vielelezo na ushahidi usio na shaka dhidi ya ufisadi wake ndani ya chama kwenye mkutano wa baraza kuu la chadema taifa September 15,2026, yanampa kiwewe zaidi.
Lakini pia viongozi wanzake wa kitaifa kujitenga nae na kujaribu kumkwepa kisirisiri kuna muumiza kichwa zaidi mtuhumiwa huyo wa ufisadi wa pesa za chadema kwa manufaa yake binafsi na ya familia yake.
Kama mdau wa jf jukwaa la siasa, unadhani ni kitu gani kingine kimefanya kiongozi huyo anaetuhumiwa kwa ufisadi chadema kupunguza uropokaji na kua mnyonge sana?🐒
Mungu Ibariki Tanzania