Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Haya makabila makubwa huwa na matatizo ya kuwa na kiburi cha chini chini pindi kiongozi alieko madarakani ni ndugu yao. Wakati sokoine alikuwa waziri mkuu wamasai walikiwa na kiburi cha chinichini, hata kipindi cha lowasa nako walikuwa na shida ingawa ilikuwa mda mfupi Kabila la nyerere lilikuwa kimya, na la mwichi, mkapa na jk pia. Lakini alipoingia jpm, masifa ya kichini chini, ukanda nao ulianza, kitu ambacho ilikuwa inapigiwa vita na ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais huyu anaiangamiza hii nchi,anaichafua nchi hii,anakiuka haki za binaadamu kwa kiwango kikubwa kuliko Rais yoyote katika historia ya nchi ni mkabila,mdini,ni Rais wa visasi kwa wapinzani wake wa kisiasa,anaingiza nchi hii katika umasikini mkubwa,Ni Rais ambaye upeo wake wa kufahamu uhalisia,uko mbali sana na ustaarabu wa binaadamu,nakupa mfano mdogo tu anaachilia kila kona ya Dar/Tanga watu kuvunjiwa nyumba zao,ati sababu wanajenga mabondeni,ukitizama sehemu hizo zote ni ngome za upinzani,hivyo mbona hatusikii mwanza ,shinyanga,Geita,chato nk watu kuvunjiwa wanaojenga mabondeni?na katika sehemu hizi kuna sehemu nyingi watu wamejenga mabondeni,tena tuna ushahidi mkubwa wa haya tunayoyasema,asilimia kubwa ya serikali yake anachukua jamaa zake,hajapatapo kutokea rais wa namna hii Tanzania,anatetea uvunjifu wa sheria,kwenye veti,katiba,sheria zabunge,usalama wa raia nk,raia wanauwawa kila leo bill hatia,ukisema unawekwa ndani,tujiulize tukienda namna hii tutafika?.
 

Kaza buti tu uteuzi bado unaendelea
 
Kwa msisitizo, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila mbaya bali ukabila mzuri wa upendo, ushirikiano, kula pamoja, kupenda wengi etc etc

P
 
Mkuu Pascal hii nadharia ya ukabila inataka kuoteshwa na watu wenye hila tu. Mimi pia ni msukuma lakini hakuna hata chembe ya ukabila kwa wasukuma hatubagui watu kwa kabila zao au dini zao.
Wasukuma wameenea karibu kila sehemu ya Tanzania na wanaishi na wenyeji wa maeneo husika bila shida.
Kama kuna hoja nyingine isemwe lakini siyo hii inayoibuliwa na watu wenye mitazamo mithili ya mkia wa sungura.
Tusijifiche kwenye chaka la ukabila kwa chuki binafsi kama kuna hoja za msingi tuzitoe lakini la ukabila kwa wasukuma hapana labda kama tumeamua kuwapaka mavi tulioyanya sisi wenyewe kisha tuseme wamejinyea.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
 
Mwanzoni akiingia madarakani walileta hoja kuwa sio Msukuma na kumbambikizia makabila wanayoyajua wao.

Watu hawa hawa leo hii wamehama na kuibuka na hoja kuwa ni mkabila.

Hoja zote hizi zinaletwa na watu wenye chembe chemba na waliojawa na uchoyo( selfish) wa kiasili ya huko makwao watokako.

Tusisahau kuwa miongo kadhaa iliyopita jamii zetu ndizo zilikuwa mstari wa mbele kuwadharau Wasukuma na kuwaona ni jamii isiyo na fursa.

Wengi wetu tuneishi huko kwa hawa Watanzania wenzetu na kutajirikia huko bila jata kubaguliwa nao, hata niandikapo hivi sasa kungali na Watanzania wa jamii mbalimbali kutoka kila pande za nchi wako huko kqa hawa wenzetu waki/mkinufaika na fursa mbali mbali na kuoeleka mkate mikoani mwenu mkiwaacha hawa mnaowadharau wakibaki na umasikini.

Ni vyema sasa tukawaelimisha vijana wa leo mkajua athari za kudandia na kusambaza uchonganishi mnaotumwa na wanasiasa wenye kengo la kuigawa nchi kwa masilahi yao binafsi.

Jueni ya kwamba haya mnayoyafanya yatapelekea tufike kubaya na ndiko wanaowatuma wanakotaka tufike na muda huo familia zao zitakuwa London za kwenu tu ndiobzitaingia kwenye vurugu hizo
 
Kuna watu umewaruka fasta ukamrukia waziri mkuu
 
Mkuu wala hatufiki pabaya wasubiri 2020 watawajua wasukuma kuwa ni wasukuma. Kwa taarifa yao tu. Mkoa wa Katavi 1/3 ni wasukuma, Morogoro 1/4 ni wasukuma wilaya ya Bahi 1/3 ni wasukuma, wilaya ya manyoni 1/3 ni wasukuma wilaya ya bunda 1/4 ni wasukuma.ukijumlisha tabora, shinyanga, geita na Simiyu . Hiyo population si mchezo kisiasa msichezee namba kisiasa.
 
Karne ya 21 mnazungumza makabila? Mnataka kutuingiza kwenye karne ya 21 huku mmepanda basi la makabila. Ni aibu. Kama ishu ni wingi kwanini mnasubiri mpaka mpate uongozi wa nchi ndiyo mpeleke maendeleo kwenu tu? Dhambi ya ubaguzi ni hasa wa know kabila ni hatari kuliko ugonjwa wa kuficha. It's matter of time. Kuna kabila waliwahi kusema wao wameshika nafasi nyeti sababu wana akili sana, wengine wakasema wao wamesoma sana. Na sasa ninyi mnakuja na dhana ya wingi. Endeleeni kipanda hiyo mbegu ipo siku mtakuwa chakula cha wale walio wachache. Weka akiba.
 
Wasukuma hawana ukabila labda unasema jamaa wale wa kabila iliyojaaTRA utafikiri walisomea kufanya kazi TRA rais endeleaa kuwatoa hapo wakatumike na taasisi zingine za umma
 
Kwa msisitizo, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila mbaya bali ukabila mzuri wa upendo, ushirikiano, kula pamoja, kupenda wengi etc etc

P
Hakuna kitu. Tabia ya mtu inajulikana akiwa na madaraka na fedha.

Pia binadamu huyazungumza yale yaliyoujaza moyo wake!

Eti ukabila mzuri wa kushirikiana, ama ndo tuuite ukabila kwenye kipeo cha pili?

Btw ukabila wa kushirikiana bado hamjafikia, Kwani mumeunda coalition kama kule Kenya?

Otherwise, hakuna ukabila wenye upendo na ushirikiano na makabila mengine.

Tafuta njia nyingine ya kumtetea if kigezo ni msukuma mwenzio.
 
HILI NENO UKABILA NI MOJA YA SABABU KUBWA INAYOSABABISHA MATAIFA MENGI YASIENDELEE NA HATA KUPIGANA WAO KWA WAO KWA SABABU YA NENO HILI ,UKABILA,, MUNGU TUONGOZE TUSIINGIE KWENYE DHAMBI HII..
 
Wasukuma sio wakabila,kama wangemua kufanya mambo ya Kenya tungekuwa na raisi msukuma au myamwezi kwa vipindi vyote tokea uhuru.
Pammoja na wingi wao na utajiri wao wa kilimo,mifugo,na madini hawa siwatu wa kuchokoza kabisa.
 
RIP Baba wa Taifa.


 
Wasukuma sio wakabila,kama wangemua kufanya mambo ya Kenya tungekuwa na raisi msukuma au myamwezi kwa vipindi vyote tokea uhuru.
Pammoja na wingi wao na utajiri wao wa kilimo,mifugo,na madini hawa siwatu wa kuchokoza kabisa.
Haitokei hivi hivi tu hata kama wasukuma ni wengi. Kwasababu si lazima apitishwe na chama? Kumbuka mgombea binafsi bado haikubaliwi kikatiba.

Sasa wewe unadhani muda wote huo ni kwasababu walikuwa hawataki au walishikiwa chini na sera za mwalimu kuhusu makabila makubwa? Kwa miaka yote toka uhuru , unadhani hawa kuwepo ndani ya ccm wenye uwezo wa kuongoza nchi?

Think think. Usitafute easy solution out!
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…