Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Wewe ndiye mkabila, acha kududanganya.
Ukisema Kanda ya Ziwa unamaanisha nini?
Ungeanza kututajia hiyo Mikoa halafu utuambie wakazi wake kwa kulinganisha na Kanda nyingine ungesaidia sana.

Lakini swali la muhimu sana kwenye uongozi lazima utambue kila mtu anafanya kazi na mtu anayeweza kumsaidia kwenye kazi zake. Hakuna Kiongozi mjinga atafurahia kuteua mtu ili kuwaridhisha watu fulani wakati huyo mteuliwa yupo tu kama pambo. Wakati wa kutafuta kura hawatakusaidia chochote.
 
mkuu umesahau na wengine wanaotoka kanda ya ziwa.... makamu wa rais Bi Samia, Waziri mkuu Majaliwa, Spika wa Bunge Bw Ndugai, Gavana wa BOT Prof Luoga,
Na hata wizara nyeti kama fedha,mali asili na utalii, ujenzi na uchukuzi wote wanatoka kanda ya ziwa.
 
ongeza na hawa
1. waziri wa elimu
2. naibu waziri wa uchukuzi
3. waziri wa ardhi
4. mwenyekiti wa parole
 


Ila Ungeleta Hilo baraza la mawaziri kwanza
 
ungejikita kwenye hoja ya ile safu nyeti aliyoitoa kwamba yote ni kanda ya ziwa...
hakusema ni asilimia 100.
Mimi namuongezea kwa nia njema tu kwamba muidhinisha fedha yaani katibu mkuu wizara ya fedha ni mpwa.wangu..
 
Huo unaoufanya wewe ndiyo ukabila. Nyerere huyo huyo alisema hatuchagui viongozi kwa kuwa tu wanatoka wapi au nduvu wa nani. Wanachaguliwa wenye uwezo na waadilifu hata kama wote wangetoka Tera au Mbokomu. Nadhani utakuwa umenielewa. Ni kwamba, huwezi ukaweka mtu mwizi kwa sababu tu anatoka sehemu fulani.
 
Mh!! Unajitahidi, unajitahidi sana
 
Mimi hua jambo lolote linalofanywa na CCM hua naliacha kama lilivyo mana linafanywa kimkakati wa kushinda uchaguzi tuu. Mana mambo mengi yanayofanywa na CCM ukiyaangalia kwa harakaharaka utaona yapo nje ya kukuza na kustawisha umoja na demokrasia nchini.

Ninachojaribu kuangalia ni kuwa ni Chama gani kitafanya tofauti na CCM? Jibu ni Hakuna ,hata vile vinavyojifanya kuwa ni vyama vya kidemokrasaia na usawa ,ni maneno ya mdomoni tu?

Tatizo hilo ulilolitaja kama linakuwepo kwenye nchi au Chama basi Mara nyingi linatokana na hulka ya ubinafsi. Na wale wanaoteuliwa kwa misingi hiyo wanafafanya kazi sio kwa misingi ya kulijenga taifa Bali kumjenga mtu aliyewapendelea na matokeo yake mwishowe yanakua ni kumshinikiza mtu asitoke madarakani ,mana wanajua akitoka atakuja mwingine na kuteua watu wake na kuwaweka pembeni. Hakuna anayependa kukaa pembeni.

Wale wachache wanaotokana na umbali wa eneo linalozungumziwa wanafanyakazi kwa kujipendekeza ili waonekane nao wapopamoja lakini kiukweli wanakua ni watu dhaifu na wanaokosa nguvu mana wanakua kama sehemu ya mazoezi ya kutoa na kuweka ili kukamilisha mzunguko.

Uzuri ni kuwa Taifa letu bado hatujafikia mahali pa kubaguana mana tumechangamana sana kwa makabila yote. Hakuna tena kabila lisilochanganyika na lingine ama kimakazi au kuoana.
Tanzania bado ni moja na tunaendelea kuudumisha umoja wetu.
 
Enzi za Rais Nyerere kuna mikoa iliokuwa na nguvu kazi ya kutosha kwa wingi lakini ilipita zaidi ya miaka 20 bila Mwl.Nyerere kuteua hata waziri mdogo wa kuchovya.
 
Tanzania ipo kwenye kipindi kigumu sana kuliko nyakati zote zilizopita
Kwa mafisdi, wazembe (kupe), na wasiokuwa wabunifu! FANYA KAZI HAKUNA KILICHOBADILIKA NI MAWAZO YAKO TU. Kama ulizoea kula vya kunyonga safari hii lazima uchije ili ule. Hakuna kula kibudu.
 
Kwa mafisdi, wazembe (kupe), na wasiokuwa wabunifu! FANYA KAZI HAKUNA KILICHOBADILIKA NI MAWAZO YAKO TU. Kama ulizoea kula vya kunyonga safari hii lazima uchije ili ule. Hakuna kula kibudu.
Wewe kilaza huwezi kuelewa maana unaishi kwa shemeji yako unakula na kulala
 

Mbona Kuanzia Awamu ya Kwanza walijazana Watu wa Kwetu Mkoani Mara sehemu nyingi, Awamu ya Pili walijazana Watu wengi wa Zanzibar na kule Kilwa pamoja na Rufiji kidogo, ya Tatu waliifurahia Watu wa Mtwara, Songea bila kuwasahau ' Mashemeji ' wa Kilimanjaro na ya Nne ilijaza Watu wengi wa Pwani, Dar es Salaam na Zanzibar bila kuwasahau ' Mashemeji ' wa Lindi ila hizo zote hujazisema / hujazigusia hapa lakini ' umewashwawashwa ' mno na hii ya Awamu ya Tano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…