Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

mhn!Makubwa.
 
Siandiki kama Msukuma wala Mbena naadika kama Mtanzania niliyo na historia ya hao watu.
Neno "NYIE" halina maana kuwa kila mtu akitoa mchango wake wa kifikira ni
'MSUKUMA".
Hawa jamaa kusema ukweli walionewa sana.

1.Vyama vyao VIKUU vya USHIRIKA vilihakikishwa kuwa vimekufa ili kusiwe na elements ya kuwaunganisha
.
2'MAJARIBIO9 experiments} za UJAMAA zilianzia kwa hawa jamaa maana hawakuwa na la kufanya.

3.MAJARIBIO{ EXPERIMENTS} za UJAMAA hazikufanyika
BUKOBA/KAGERA, Ama Mikoa kama KILIMANJARO.Jiulize ni KWA NINI??????

Ni kweli hawa ni wati wa kuhurumia sana!!
Japokuwa TATIZO lao nao walipenda Ngombe sana.
Na kama nasema uongo unaweza kuni challenge
 
kumbe walewale sa tutegemee nini?? ndomana nyerere nasikia alikataaga makabila yenye watu wengu kushika nchi
 
Mayalla umesahau pia kuwa Wasukuma ndio kabila linloongoza kwa kuharibu manzigira kukata miti ovyo, kuingiza mifugo kwenye hifadhi za taifa na reserve pia hawachimbi vyoo.
Wasukuma ni kweli ni waharibifu wa mazingira aisee. Ila wamasai wanaongiza kwa kuchungia ng'ombe kwenye hifadhi za taifa wala siyo wasukuma. Msukuma hana uwezo wa kupambana na simba ila masai anao. Anachungia Ngorongoro national park na simba akisikia kengele ya ng'ombe anatimua mbio mwenyewe. Jamaa ni noma sana hao.
 
Tusipokuwa makini hii nchi tutakuja kugawana vipande. Maana wasukuma wakishanogewa wanaweza wasiachie madaraka moja kwa moja. Na hivi wako wengi kama kataifa kao wenyewe huko kanda ya ziwa.
 
kumbe walewale sa tutegemee nini?? ndomana nyerere nasikia alikataaga makabila yenye watu wengu kushika nchi
Ni kweli, hata mleta mada kasema "tatizo ni kabila lenye watu wengi", na kweli ni tatizo. Tena endapo watauendeleza ukabila, basi ni wasukuma hadi kiyama. Labda nchi imegeke. Na dalili ziko huko mbeleni kwa utaratibu huu wa "kiwanja cha kimataifa cha ndege chato", na bandari.
 
Wasukuma halisi ni kabila la watu watii sana na wanyenyekevu, wanaishi communal life mpaka kesho, they are not selfish, they're selfless hadi leo hadi kesho, vijijini wanakula sahani moja. Land ilikuwa ya wote the entire community hivyo it was easy kukubaliana na kila wazo la Mwalimu Nyerere after all, Wasukuma sio very industrious, pamoja na utajiri mkubwa wa n'gombe, hawakujijenga kisasa, vijumba vya hovyo hovyo, na hawana mazao ya kudumu hivyo it was easy ku abandon kila kitu na kuhamia kijiji cha ujamaa, sisi kwetu tuliisha jenga nyumba ya block ya bati, tukagoma kuhama, tukatengwa, babu alipochomoka, Bibi akahamia mjini kwa wanae tukahama bushi jumla.

Wachagga na Wahaya, ni selfish tribes, kila mtu anapakuliwa chakula sahani yake au bakuli lake hivyo no sharing. Kule hakuna communal land, kila ukoo na kihamba chake, na kufuatia zao la kahawa ndio the biggest cash crop, wale ni industrious, hivyo waliendelea wakajenga nyumba za maana, hivyo walikubali kuanzisha vijiji vya ujamaa Kwa lazima lakini walimgomea Mwalimu kuhama, kata kata, na kiukweli enzi za Mwalimu, Wachagga na Wahaya waliisoma sana number.

P
 
Mkuu Karne hiii unakuwa na guts za ku spell Ukabira kwenye mind na kuutafsiri kwenye ink. Good luck japo huwa nasoma posts zako
 
Ni kweli mwalimu amesomesha wachagga namba mbaya kabisa! Lakini sikubaliani kusema eti nyie wasukuma mkila chakula wenyewe kwa wenyewe ndiyo siyo ukabila. Huo pengine ni utamaduni tu, hata uchggani upo. Mbona watu wana "ria mbege", chubuku moja inapitishwa kila mtu anakunywa? Mbona hata wakichinja ng'ombe ama mbuzi, nyama zinawekwa kati na ndizi watu wanapiga?

Mkuu hauna taarifa za kutosha, pengine ni kwasababu ya ubinafsi hutaki kufahamu. Ama umekuwa "blindsided due to bias", kwahiyo vya wengine either huvioni, na hata ukiviona, hauoni kwamba ni bora nk.
 
Mkuu Roman, kwanza sorry and don't be offended, kabla ya ujio wa wakoloni, Wachagga pia walikuwa communal, hiyo ya Ku "ria hapo kidogo mbee' ndio kidogo iliyobakia, the spirit ya accumulation of capital is inside Wachagga wengi, na ndio maana wanaijua hela na ndio wanaongoza kwa maendeleo and fixed assets lakini kubali kataa, tribals preferential ipo kwenye ofisi zote top boss ni Mchagga au Muhaya na usitake kupinga tukafumua humu makaburi.
 
Mimi ni msukuma sihitaji kutetea wasukuma hata kidogo natamani watu waseme wale walioenda usukuma nadhani ushuhuda wao utakuwa na nguvu kuliko utetezi wangu. Niliwahi tu kumwambia rafiki yangu kuwa Mungu acha aitwe Mungu maana hili kabila kama lingepewa karma ya ndugunazation wakivyo wengi wangeleta machafuko. Allhamudillah mola akaepusha. Hakuna cha Mwadila ofisin wala ginehe nkoi. Ila kama ipo ni ya mtu mmoja mmoja maana ubaya hauna kwao
 
Ukabila upo kwa makabila mengi tu mkuu. Niwekee hizo links hapa unazodai ni makaburi utafukua, weka hapa.

Shida kubwa ni assimilation! Hata hayo makabila ya wachagga na wahaya, kama waliajiri watu ambao wanasikilizana, kikubwa kinachangiwa na assimilation. Mfano kuna baadhi ya makabila yako hivyo hayawezi ku assimilate ama kujichanganya. Nimeshuhudia sana hili. Bado ile identity ya utaifa inafunikwa na ukabila. Mtu utakuta yuko happy kufanya kazi na mtu wa kabila lake kwasababu wanaelewana zaidi, ama wanakula the same food, wanaogea the same language, na tamaduni zao hawaziachi nk.

Utakuta msukuma ameishi uchaggani akifanya vibarua nk, lakini piga ua, hawezi kula ndizi, atasema siyo chakula, na hiyo ni stereotype. Ndizi ni chakula bora sana. Yeye amekariri ugali nk.

Hayo mambo na hizo tabia, ni visababishi vikubwa vilivyopelekea sisi kutawaliwa na mzungu. Mzungu yeye kwa kujichanganya! Utakuta anaongea hadi kimasai na rubega kapiga!
 
Maandishi yako yanakaukweli, Mimi nina zaidi ya mwaka uhayani lakini sijawahi wala kutamani kuonja senene, naona ni wadudu. Inakuwaje nile wadudu? Ila wengi wanaisifu chakula hiki, sisi kwetu nyama hasa ya ngombe na mbuzi ndiyo kila kitu.
 
Maandishi yako yanakaukweli, Mimi nina zaidi ya mwaka uhayani lakini sijawahi wala kutamani kuonja senene, naona ni wadudu. Inakuwaje nile wadudu? Ila wengi wanaisifu chakula hiki, sisi kwetu nyama hasa ya ngombe na mbuzi ndiyo kila kitu.
Naunga mkono hoja, hata mimi sijaweza kabila kula senene, tatizo ni psychological na connotation kuwa senene ni chakula cha Kihaya, kwa vile mimi sio Mhaya, then siwezi kula senene. Huu pia ni ubaguzi wa kikabila, kwa sababu hao senene sijawahi hata kuwajaribu nikashindwa, ile thinking tuu ni wadudu, siwezi kula, lakini mimi huyo huyo, nimeletewa prone nikajaribu, na ninawala!.
P.
 
Hili la ukabila wa Wasukuma, nimelizungumza hapa.
P.
 
Karibu mitaa hii
P
 
Soma bandiko hili
Sisi sio wakabila bana.
P
 
Mkuu Digiti Elfu, kwanza samahani kukujibia huku, kwa sababu ni kawaida yangu, nikipandusha baadhi ya mada, huwa sichangii lolote wala kujibu hoja yoyote zaidi ya kutoa likes tuu, lakini objectivity ya mchango wako, umenigusa.

Mimi sio mkabila, na Wasukuma sio wakabila na hawajawahi kuwa wakabila, kwa vile Tanzania tumeisha ongozwa na marais wa makabila matano tofauti, na kila kabila lina strenghs zake na weaknesses zake, kuna ubaya kusifia strenghts za kabila fulani kama uchapakazi bila kuonekana mkabila?.

Tumepata rais chapa ng'ombe anapiga kazi kama maksai, mtu hadi analala na mafaili chumbani, kuna ubaya kumsifia bila kuonekana mkabila?.
P
 

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa Wasukuma hawana ubagusi tangu zamani. Nakumbuka enzi zetu za Middle school ile miaka ya sitini(kuwa specific 1963) tulifundishwa darasani kuwa idadi ya Wa Tanganyika(population in Tanganyika) ilikuwa million 9 kati ya hao Wasukuma walikuwa million tatu(three million)(from this figure current Wasukuma lazima wawe at least 20 million) na upande wa nchi ya Zanzibar population ilikuwa laki tatu(three hundred thousand) Wachagga na Wahaya wastani kila moja laki 6!!!! Ila waliosoma kuliko wote ni Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa! Sababu - wamissionari waniingia sehemu hizo na kujenga mashule na Mahosipital. Waarabu walisisitiza zaidi ujenzi wa misikiti! Ukweli ndiyo huo! Pili Wachagga/Pare na Wahaya wengi walisoma Uganda na Kenya wakati sekondari zilikuwa chache Tanganyika - Sarafu ilikuwa ni moja Africa Mashariki. Ukiona Wahaya, Wanyakyusa na Wachagga/Pare maofisini siyo kwa upendeleo ila ni shule!!! I stand to be corrected ila kwa sasa sekondari ziko kila kata!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…