Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!



Wenye macho wameona, wenye masikio walisikia!

Hainahaja ya kutaka kulaumu mkwezi wakati nazi imeliwa na mwezi!
 
Wasukuma jamaa yenu kawaharibia sana
Mlichokosea ni kumsifia muda wote ni kama mtt mkorofi anasemelewa kwa mamake anasifiwa badala akandiwe mbele za watu halafu asifiwe nyumban nyie mnasifia hadharani ujinga kwa kweli hamuaminiki na hamtakaa muaminike nchi hiii
 
Influence ya wasukuma iko wapi wakati ni watu wasio na elimu
Wasomi wangap ngazi za juu ni wasukuma ..?
Hii miaka mitano mmefanikiwa kubebana lakini nakwambia kwa vile hamko competent anguko Leni ni kubwa sana wahaya hawahitaji kubebwa tayari wamejipambanua wako vizuri kichwani
Nakwambia wasukuma ukabila mlioanzisha mtaona mwisho wake
 

Wanaokulinda ni wasukuma, Mara, kanda ya Ziwa, wahehe pia hawaogopi kufa, kazi ngumu.

Sehemu nyingi hatarishi wapo hapo.

Usalama Rais ni nani, Jeshini, Polisi nani ndio wengi? Ambao hawaogopi kazi ngumu.

Mwadui Goldmine, Mgogoro wa Barrick Gold(tupate mgao mkubwa pesa zitumike kwenye elimu, afya, hospitali, miundombinu Tanzania nzima).

Serengeti ipo pale karibu. Ndio mbuga bora kabisa duniani.

Kubadilisha sheria za madini tuwe na share za kutosha kwenye madini yote 16% sasa ilikuwa sifuri na seat on the high ,top table, pia economic benefit, (zilikusanywa ngapi ukiondoa gharama zako tugawane 50/50.) Kiufupi hakupata chocchote cha maana kwa miaka toka uhuru. Mzee akakomaa.

Ni mfano Duniani. Tujue kila kinachofanyika kwenye bodi.

Utatusaidia sana ni blueprint utatumika kwa mikataba yote inayokuja.

Sato, Sangara, dagaa nimewaona wamejaa kwenye Supermarket za Ulaya. Hadi Kahawa, Chai.

Ngombe ni wa pili Africa, Mbuzi na Kondoo hatuko mbali kuongoza. Hawa Ngombe wanachungwa kienyeji, kitaalamu tunaweza kuwa wa kwanza Duniani.

Kilimo pamba, mchele, mahindi, maharage yamejaa tele.

Ongea na Mmasai, Msukuma wape mbinu za kisasa za kufuga serikali itapata mapato, nyama maziwa ya kutosha. Watoto wako watapata elimu, afya nzuri bure.

Kuna watu wanataka sera za majimbo bila aibu. Wasukuma wanataka ku -share walichonacho kwa nchi nzima.

TRA, CRDB, BOT tumeona matokeo yake ukimpa uongozi mtu fulani, kwenye Taifa itakuwaje.

Kununua kiwanja ni shida, ukifungua duka maeneo fulani ni issue, hata ukifungua hutapata wateja. Kisa ukabila. Kama hauendi kila mwaka kusalimia ni issue.

Usukumani hakuna hizo issue.
 
Mkuu naelewa sana kuwa Wasukuma kwa kawaida ni watu poa sana.
Msukuma ni mtu gentle na mstaarabu kwa kadri ninavyo wafahami, maana tumeoleana huku mitaani.
Asante kwa hili kuhusu Wasukuma.
Lakini kumbuka SUKUMA GANG ni pseudonym ya wafuasi wa Mwendazake.
Siyo siri hata hivyo kwamba Mwendazake aliteua 0ver 80% ya viongozi wake toka Lake Zone, na ndio maana ya asili ya hiyo Sukuma Gsng.
Kwanza sii kweli JPM aliteua 80% kutoka Lake Zone, ukweli ni kuwa Lake Zone acconts for 40% of Tanzania population, hivyo kwenye kila uteuzi wa nafasi 10, nafasi 4 zilipaswa kutoka kanda hii as a derserving positions and not prefential treatment.

P
 
Kwa maoni yangu, nadhani Wasukuma ni one of the most accommodative tribes. Mtu kutoka kabila lolote unaweza ku settle usukumani na ukakubalika bila kubaguliwa angalia hata wabunge wa Mwanza, Kiwia ni Mchagga aligombea Mwanza akapata, sasa wewe mtu wa kabila jingine kagombee ubunge Moshi au Bukoba!.
Kiukweli kwenye ukabila Wasukuma mnatuonea.
P
 

watu wasio na ukabila Tanzania hapa ni watu wapwani tu....kuanzia pwani ya Dar es salaam kwa wazaramo mpaka pwani ya kusini kwa wandengereko na wamakonde.. ila makabila yote ya watanzania ukiondoa hao yamejaa ukabila tena hasa haya makubwa Wachaga, wasukumu, wahaya na wanyakyusa..

Na tusipokuwa makini na kuacha baadhi ya philosopy za Mwalimu Nyerere huko mbele hii nchi inaweza kugawika vipande vipande kwa sababu ya ukabila...

Tuliza kichwa fanya proper research bila ushabiki utaamini maneno yangu...ukabila unafichwa na unafiki ila ukiingia deep utauona ukabila tena mbaya sana....
 
1. Je wasukuma ni wengi kuliko watanzania wa makabila mengine kwa ujumla?
2. Sisi tulio kwenye ground tunaona picha ingine, but it is very scary.
 
Nimeishi Mwanza nimeona
Mtu asikudanganye hizo ni chuki za watu binafsi wasukuma hawana ubinafsi wala ukabila
Ukiona mmoja mwenye tabia hiyo ni yeye kama yeye lakini ukweli ndio huo
Njoo Moshi ndio utaelewa Kuna watu Wana Roho mbaya
 
Mkuu hiyo 80% ni nafasi za juu za uongozi.
Kuna wakati tulikuwa na mawaziri 7 hadi 10 kutoka Lake Zone peke yake, achilia mbali na kundi la akina Dotto na huko Idara za Sheria.
 
"Statistics are like bikinis. What they reveal is suggestive, but what they conceal is vital"(Aaron Levenstein)

Asante mkuu Pascal Mayalla Kwa hii takwimu. Umenibariki.
 
Wa

Waislam ni 60% ,mko tayari kila teuzi 10 , 6 wawe waislam. ???

Mkitoka kwenye ukabila mtakwenda kwenye udini ili tu chama kishike hatamu kwa katiba inayotoa mianya ya upendeleo.
 
Ukabila m-baya! Na ukabila mzuri! Upi unafaa.
 
no wonder zamani mliitwa mang'ombe, kwasababu uelewa wenu huwa mdogo sana. you shouldn't even dared to argue like that.
 
Wa


Waislam ni 60% ,mko tayari kila teuzi 10 , 6 wawe waislam. ???

Mkitoka kwenye ukabila mtakwenda kwenye udini ili tu chama kishike hatamu kwa katiba inayotoa mianya ya upendeleo.
aliyekwambia wapo 60% amekudanganya sana. ukiondoa zanzibar, wao ni 45 au 40, therest ni wapagani wa kisukuma na wagalatia.
 
Kila kabila lina ukabila - ukabila ni hali/tendency ya kujipendelea kama mnaongea lugha moja au mnatoka sehemu moja - hiki kitu kiko ndani mwetu wote. Sehemu ambazo kuna mwingiliano mkubwa wa watu ukabila ni mdogo maana watu wanakuwa exposed kwa watu kutoka sehemu zingine na hivyo sehemu fulani ya prejudice waliyonayo inapungua na sehemu ambazo hazina mwingiliano mkubwa wa watu, kuna tendency zaidi ya kuonyesha ukabila/upendeleo wa watu wa kabila, lugha, sehemu unakotoka. Sisi wote tuna elements za ukabila. Mimi natoka Ukerewe (UK), nikikutana na Wakerewe au watu wa kutoka Ukerewe nita'feel' more comfortable kuongea au kuwa nao siyo kwa sababu napenda kufanya hivyo, ila kwa sababu najikuta navutwa kufanya hivyo kwa sababu tu tunaongea lugha moja au tunatoka sehemu moja. Wanaofanya bidii 'to overcome this tendency' wanafanikiwa sana (hawa ndio tunaosema hawana ukabila), wasiofanya hivyo unawatawala (hawa ndio tunaosema wana ukabila).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…