Wananchi hawana imani tena na upinzani, wamechoshwa na stori na porojo na kusingizia rushwa mara kwa mara sababu ambazo hazina mashiko kwenye mahitaji na changamoti zao za kila siku.
Hali iyo imebainisha na imedhihirisha kwamba upinzani hawana mipango, hoja, sera, nia wala mikakati mbadala ya kuwaletea wanainchi maendeleo, ispokua kubuni tuhuma za uongo, uzushi na za kusadikika, ambazo zimewafanya wanainchi kutowaamini tena wapinzani wala kuwatilia maanani kwamba eti wana uwezo au nia ya kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii, kisiasa na kiuchumi, kumbe wana chuki binafsi tu, dhidi ya baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali, kitu ambacho hakina faida yoyote kwa waTanzania.
Mfano mzuri ni kutoka kwa watu wa maana sana wa Itigi, kumpuuza kiongozi wa upinzani aliejaribu kuanza kuwahadithia stori ya tuhuma za kusadikika ambazo sio shida za watu wa Itigi....
waTanzania wanataka maji, afya , elimu, umeme, barabara nzuri, masoko ya bidhaa na huduma, lakini pia wanataka pembejeo za kisasa za kilimo, uvuvi na ufugaji.
WaTanzania wanataka ulinzi na usalama wao na mali zao. wanahitaji amani na utulivu wanapofanya kazi na majukumu yao ya kila siku kujipatia riziki.
WaTanzania hawahitaji wala hawana haja na mlolongo wa tuhuma za kusadikika, za kubuni na za kupika uongo zinazochochewa na chuki binafsi, hasira na ghadabu za kukataliwa na wanainchi kila mkutano wa hadhara au uchaguzi.
Ni Faraja ya kipekee sana, kuona waTanzania wameanza kuacha kupoteza muda wao kwenda kuskiza stori na porojo ambazo hazina, na haijawahi kuleta matokeo wala uelekeo wa kumsaidia mwananchi, bali kinachooneka ni chuki binafsi, wivu na kukosa hoja, dira na uelekeo wa pamoja....
Ukata wa pesa za kufanyia mikutano ya hadhara, na pesa kwaajili ya kampeni za uchaguzi, zinawavuruga zaidi, na kunazidisha kudharauliwa na kupuuzwa zaidi na wananchi wanapofanya mikutano yao iliyozorota sana 🐒
Mungu Ibariki Tanzania..