Tujifunze kitu kwa misiba ya vigogo hawa na idadi ya watoto

😀😀 Mzee naona inatoka budget maalumu kabisa ya mavazi ya msibani, watu wanapigilia aisee full ma makeup kama Ile misiba ya kwenye movie za marekani
Msiba wa matajiri itifaki inazingatiwa, siyo kwetu uswahilini, niliwahi kwenda musoma nikakuta wanautamaduni wa kushangaza, kuna ule muda msibani watu huwa wanatulia kimya hawalii sasa akiingia ndugu mpya vilio ndo vinachochewa kinyama wanalia Balaa, baada ya nusu saa wanatulia akiingia tena mgeni mwingine mayowe yanaanza.

Ikaenda hadi yule mtu akazikwa sasa imeshapita wiki kama 3 mtaa mzima tumesahau msiba si akafika ndugu alietoka safari ya mbali hicho kilio walicholia nilijua wamepata msiba mwingine kumbe ndo staili ya kumpokea mgeni msibani full fujo.
 
Mkuu niliwahi kusema matajiri wakubwa TANZANIA hawana msaada wa moja kwa moja kwa jamii nikatukanwa na kuambiwa nitafute vyangu.
 
Sawa, kwahyo hata kama unafanya kazi kiwandani unalipwa kwa siku elfu7 hata ukizaa watoto 10 sawa tuu ausio
Kwani anakuja kukuomba msaada wa kulea watoto wake?

Huyo huyo unayemuona ana kazi ya kijinga na familia kubwa bado anawalea vizuri kabisa huku akiwasaidia wazazi na ndugu wengine pia.
 
Hakuna somo la kujifunza kupitia hao marehemu .

Mfano huyo Ndugulile alishindwa hata kuacha legacy yoyote

Huyo mwingine the same

Ukiachana na kujilimbikizia Mali we have nothing to learn from them.
 
Kwa mtazamo wa karibu hao watoto hakuna mwenye uelekeo wa kuja kuwa jambazi ama kahaba , ila kwa mwaju ndala ndefu unaona kabisa hapa kuna mmoja atakuja vunja nyumba ya mtu siku za usoni🤔
 
Kwa mtazamo wa karibu hao watoto hakuna mwenye uelekeo wa kuja kuwa jambazi ama kahaba , ila kwa mwaju ndala ndefu unaona kabisa hapa kuna mmoja atakuja vunja nyumba ya mtu siku za usoni🤔
Shida hawa watu hawaelewi? Yani unasema kuzaa hakuna shida halafu mtu Hana yeye tuu hajiwezi, watoto watalelewa na Nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…