Tujifunze kitu kwa misiba ya vigogo hawa na idadi ya watoto

Mkuu ukitambuka kuwa kifo ni sehemu ya maisha yetu huna haja ya kulia, kinachotuliza sisi masikini ni huduma, baba alikuwa ndio muhimili mkubwa wa familia, ametutoka je! Ni nani ataihudumia familia? Hapo kulia na kujigaragaza kunapoanza.
 
Mtu maskini akizaa mtoto anaongeza maskini mwingine duniani na kuipa serikali gharama kubwa sana ya kuhudumia umaskini wa kizazi chake.
Ni gharama ipi ambayo unaweza sema serikali za nchi za Africa zinaingia kwa ajili ya wananchi.

Maana serikali inaendeshwa kwa fedha za kodi zinazokusanywa toka kwa wananchi na wengi ni hao maskini.

Hao matajiri ndio wakwepaji kodi wakubwa na mpaka wanaajiri watu wa kuwashauri namna ya kukwepa kodi.
 
Ndio mkuu, huku mitaani watoto wamejaa tele wamekosa malezi
Ndandeki.
Mgawanyo wa majukumu wa kionezi sana huo. Yaan wengine ndiye wawe na haki ya kutiana na kuacha off-springs zao, huku wengine jukumu lao liwe kujenga uchumi na kulea hao wengine bila ya wao kuacha off-springs zao.
 
Usijidanganye..
.hao ni watoto waliojulikana,huko mitaaani anaeweza kuwa na watoto,Kuna mtu ndani ya ndoa alikuwa na watoto 2.kumbe inje ya ndoa anawatoto 4.
Usinambie nilijuaje!😂,
 
Mie nitachukua mfano wa tajiri namba moja duniani na wala sio wanasiasa.

Elon kafyatua 12 na anakwambia anaongezea
 
Hao ni wazembe tu, usilinganishe, je hana watoto wa pembeni?, sasa akina Jaffo mwenye wake wanne utasemaje, wewe zaa tu kila mtu ana mipango yake bwana
 
Ni gharama ipi ambayo unaweza sema serikali za nchi za Africa zinaingia kwa ajili ya wananchi.
Mikopo ya kugharimia maisha ya wananchi wengi maskini na matajiri wachache wakwepa kodi.

Hii ni gharama kubwa kwa serikali inayo zalisha madeni makubwa kwa serikali za Afrika.
Maana serikali inaendeshwa kwa fedha za kodi zinazokusanywa toka kwa wananchi na wengi ni hao maskini.
Serikali nyingi za Afrika zina endeshwa kwa mikopo na misaada ya wazungu.

Kwanza kwa Afrika watu wengi ni wakwepa kodi. Kwanzia maskini hadi matajiri.
.

Hao matajiri ndio wakwepaji kodi wakubwa na mpaka wanaajiri watu wa kuwashauri namna ya kukwepa kodi.
Afrika kila mtu ni mkwepa kodi.

Ni vile hao maskini hawajapata nafasi ya kuingia serikalini kupiga.

Ila mentality za waafrika wengi zimekaa kiwizi wizi.
 
Hii ndio shida ya Mwafrika. ..ubnafisi na Ulafi.

Wazungu wana hela sana. Wakishatimiza mahitaji yao muhumu pesa zinazobali wanatuletea Wafrika washenzi, miradi hii inayosaidia Wamama na Watoto na rai ni mingi
1. Malaria
2.TB
3.HiV
4. Afya ya Mama na Mtoto
5.Ukoma

Zote hizi ni pesa za wazungu wenye huruma kwa Binadamu wenzao.

Huku kwetu ni ufahari usio na faida yoyote hata kujenga kisima cha maji mtaani maskini wakapata maji hawajengi.

1.Magari ya kidahari
2.Nyumba za kifahari
3.Ardhi za kifahari
4. Ubaltasar mwingi

Mwisho wanakufa bila legasi yoyote waliyoacha
 
Mikopo na misaada ni uzembe wetu na hao tuliowapa dhamana.

Nchi Kama Singapore inategemea bandari zake na imetoboa.

Sisi tunachokosa ni uzalendo tu ila tuna kila kitu na bado maskini.
 
Binafsi huwa ni mwendo wa kufyatua, ilimradi Nina uwezo wa kuwalisha, kuwavisha na mazingira wezeshi kwaajili ya maisha Yao ya baadae nk... Huwa sijali chochote kile kisemwacho, watoto ni fahari kwangu. Nawafundisha wanangu kuhusu ubinadamu, wajue Kuna Leo na kesho kwenye maisha haya, wakipata wasiache kusaidia wenye tabu na shida, huu ndo wosia wangu kwao.
 
Jk,Mwinyi mzee,JkNyerere,Masabuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…