Ndugu yangu, mbona tena unaleta khadith za kitoto na kutaka kuiharibu hii thread...jaribu kujitofautisha na hao mbumbumbu wengine!
Mbona hata Waislam unaowataja/unaowashutumu nao pia wanalalama pita kiasi yakuwa hizo mitaa/Barabara takriban zoote wamepewa maluuni wengine tu wasiokua hata na history,asili au hata kujitolea muhanga na hilo jiji au nchi/Taifa letu!?
Unafahamu yakuwa mitaa michache mno hapo D'Salaam hiyo mnayodai ati ina majina ya Waislam; ilipewa majina hayo baada ya msukosuko na lawama nyingi toka kwa Waislam na wapenda haki wengineo hapo nchini!? Hii ilikua khasa kipindi cha Alhaj Hassan Mwinyi na Kitwana Kondo.
Ikumbukwe zaidi,yakuwa hao unaowaona ati ni Waislam... asilan hawakupewa majina ya hiyo mitaa sababu ya Uislam wao...hasha abadan!
Hao walikua ndo Vinara,Wanaharakati,Wafadhili na Wahenga wakuu wa kupigania ukombozi/harakati za kutupatia huo "Uhuru" wetu.
Zaidi ya hilo,takriban woote kati yao hiyo D'salaam/Mzizima ni kwao au ni kwenye asili yao...kwa hiyo hawakuwa ati ni wageni hapo kama wengineo wengi tu!...
Hata hivyo wengi mno kati yao wamesahaulika kwa makusudi kwenye hiyo "Official History" ya nchi hiyo kama alivyoitaka yule Nyerere!
Nafikri pia unashuhudia hata leo wakijaribu kutajwa kiduchu tu humu mitandaoni-Jf na kwingineko,basi hutokea Wajaaluta kadhaa kuwakashifu hao Mashujaa wetu,Wanaharakati na Wakombozi wa huo "Uhuru" wetu!?
Nakhis ni uzuri ifike wakti baadhi ya jamaa zetu wengi mpunguze jazba na mihemuko ya kidini japo kiduchu na kuzipisha hizo Ilm na busara zenu kufanza shugulize japo thuluthi...na hii ni kwa faida yetu soote na Taifa letu changa!
D'salaam,ni mmojawapo wa mikoa michache saana kama sio pekee hapo Tanganyika usokua na ubaguzi kwa watu woote...embu kachungulie huko mikoani kuna mitaa mingapi yenye majina ya watu wenye asili au kutoka D'salaam/Mzizima!?
Nyerere alichukua ile ilokua Independence Avenue nafikiri ndo akaipa jina la yule Mmakonde Terrorist wake...ambae bila ya shaka kama angalikuwapo mpaka leo basi wale washenzi/Politicians wa Western World labda nae pia wangemwita pale Dan Hague/The Hague akajibu charges - Crimes against humanity!? Kwi! Kwi! Kwi!
Kuna wakti nilitoa maoni na sababu/history kiduchu humu Jf,kupinga yule mpuuzi Mwai Kibaki kupewa jina la mmoja wa mitaa/barabara zetu maarufu hapo Mzizima/D'Salaam...matokeo yake nilishambuliwa vibaya mno tena bila hata ya mantik yoyote ile!?
Ahsanta sana.
Mimi nadhani mnapotosha watu sana nyie,harakati za uhuru zilikuwa karibu kila mahari Tanganyika,isipokuwa Dar palikuwa ni kitovu cha harakati hizo,na sababu zipo nyingi sana,na kwa upande wa Dar zilianza kama harakati za Kidini,waislamu ambao ni wengi kwa kipindi na ndio wenye mji wao hawakupendezwa na utawala wa wageni,hivyo basi kila baada ya swala za jion walikusanyika na kupiga story kuhusu tawala hizo na nyingi ya history hizo ni namna gani wataondoa maudhi ya mtawala wa kigeni.
Harakati hizo ziligeuka na kutoka kwenye dini na kuingia kwenye siasa na hili lilikuwa vuguvugu la kila mahari kipindi hicho.
Bahati mbaya sana,kisiasa Mzizima bado haikuwa na watu wenye weredi,hivyo suala la kutafuta watu weredi lilifanyika.
Na uhuru ukapatikana.
Bahati mbaya sana kwa nyie wadini hamtaki kukubali ukweli kwamba vuguvugu za kiislamu ndizo hasa zilileta mambo mabaya sana baada ya uhuru kwa wale waliokuwa na tamaa zao baada ya uhuru,baadhi ya watu hawakukubali kamwe kutokupata vyeo,ingawa ni ukweli ulio wazi Mwl halijumuisha baraza lake la kwanza la mawaziri na watu ambao hawakuwahi kuuona mlango wa shule hii yote kupunguza vurugu,na hali imekuwa hi to mpaka Leo.
Conclusion,ni ukweli mchungu lakin kama Mwl angekuwa na roho za watawala kama wengine Kipindi like Bibi Titi asingeishi na kufika tamati ya maisha yake peacefully.Na ni wazi hulka za binadamu tunatofautiana hivyo basi kutokutamani hata uone maiti ya mtu aliyetaka kukuua kwa ushaid ulio wazi ni jambo linaloweza mtokea mtu yeyote.
Kifupi haya mambo yapo wazi,vitabu vya Mohamed Said ni upande mmoja,na ukumbuke Kuna conflict of interest kwenye vitabu vyake,sababu Ana unasaba na wakina Sykes and likes,na upande wa pili unasema hili.
Hivyo basi nadhani tufike mahari tumeze ukweli mchungu kwamba kwa waislamu ambao ni wengi nchi hii na harakati zao za kidini zilisababisha harakati za kisiasa na uhuru kupatikana,then after ukosefu wao wa elimu hawakuweza kushika nafasi mbambali baada ya uhuru,na Kisha kuanzisha vuguvugu za chini chini zilizoungwa mkono na wachache wagalatia wenye tamaa za madaraka kipindi kile,na kudhibitiwa na mwalimu,limekuwa ni donda sugu kwa kila kizazi cha kiislsmu kilichofuata kila wanaposimuliana na kureview mapito yale,wanahisi walidhulumiwa kitu,na lawama zao zote ni kwa Nyerere na sasa limezuka hilo la mfumo Kristo,kuwakumbusha tu waislamu ,Nyerere hakuwa na kosa lolote,ni nyinyi kosa lenu wenyewe,by 1961,nchi inapata uhuru wenye degree ni watu 12 tu kwenye taifa la watu milion tisa na wote ni wagalatia,mlitaka afanyeje?Go on forget the past my dears.