Maulana Al Tayeb!
Asalaam Alaykum, Al Akhiy.
Wallahi,ndo nachungulia hapa kiduchu naona zile "Zah'ma Wa Min'karadas" ndo zimeshaanza!ahaaa!!
Naona unavyoshusha mipini yako kwa utaratibu!ahahaa!!
Ahsanta.
Ndugu yangu, mbona tena unaleta khadith za kitoto na kutaka kuiharibu hii thread...jaribu kujitofautisha na hao mbumbumbu wengine!
Mbona hata Waislam unaowataja/unaowashutumu nao pia wanalalama pita kiasi yakuwa hizo mitaa/Barabara takriban zoote wamepewa maluuni wengine tu wasiokua hata na history,asili au hata kujitolea muhanga na hilo jiji au nchi/Taifa letu!?
Unafahamu yakuwa mitaa michache mno hapo D'Salaam hiyo mnayodai ati ina majina ya Waislam; ilipewa majina hayo baada ya msukosuko na lawama nyingi toka kwa Waislam na wapenda haki wengineo hapo nchini!? Hii ilikua khasa kipindi cha Alhaj Hassan Mwinyi na Kitwana Kondo.
Ikumbukwe zaidi,yakuwa hao unaowaona ati ni Waislam... asilan hawakupewa majina ya hiyo mitaa sababu ya Uislam wao...hasha abadan!
Hao walikua ndo Vinara,Wanaharakati,Wafadhili na Wahenga wakuu wa kupigania ukombozi/harakati za kutupatia huo "Uhuru" wetu.
Zaidi ya hilo,takriban woote kati yao hiyo D'salaam/Mzizima ni kwao au ni kwenye asili yao...kwa hiyo hawakuwa ati ni wageni hapo kama wengineo wengi tu!...
Hata hivyo wengi mno kati yao wamesahaulika kwa makusudi kwenye hiyo "Official History" ya nchi hiyo kama alivyoitaka yule Nyerere!
Nafikri pia unashuhudia hata leo wakijaribu kutajwa kiduchu tu humu mitandaoni-Jf na kwingineko,basi hutokea Wajaaluta kadhaa kuwakashifu hao Mashujaa wetu,Wanaharakati na Wakombozi wa huo "Uhuru" wetu!?
Nakhis ni uzuri ifike wakti baadhi ya jamaa zetu wengi mpunguze jazba na mihemuko ya kidini japo kiduchu na kuzipisha hizo Ilm na busara zenu kufanza shugulize japo thuluthi...na hii ni kwa faida yetu soote na Taifa letu changa!
D'salaam,ni mmojawapo wa mikoa michache saana kama sio pekee hapo Tanganyika usokua na ubaguzi kwa watu woote...embu kachungulie huko mikoani kuna mitaa mingapi yenye majina ya watu wenye asili au kutoka D'salaam/Mzizima!?
Nyerere alichukua ile ilokua Independence Avenue nafikiri ndo akaipa jina la yule Mmakonde Terrorist wake...ambae bila ya shaka kama angalikuwapo mpaka leo basi wale washenzi/Politicians wa Western World labda nae pia wangemwita pale Dan Hague/The Hague akajibu charges - Crimes against humanity!? Kwi! Kwi! Kwi!
Kuna wakti nilitoa maoni na sababu/history kiduchu humu Jf,kupinga yule mpuuzi Mwai Kibaki kupewa jina la mmoja wa mitaa/barabara zetu maarufu hapo Mzizima/D'Salaam...matokeo yake nilishambuliwa vibaya mno tena bila hata ya mantik yoyote ile!?
Ahsanta sana.
Mwanasiasa umkanye huyu panya buku atakuharibia kanyageni.
Kila mtu ana dark side hata wewe pia mkuu, kuna mambo ambayo hutamani tuyajue lakinipo siku tutayajua..ni jambo la muda tu na nafasi, vile vil eunaweza kutumia jina la kambona kwa watoto wako, ni nafasi nzuri kumuenzi sio lazima kila mtu apewe mtaa ndio mchango wake ukubalikeNaendelea kusoma kitabu cha The Dark Side of Nyerere.Kitabu hiki kilipigwa marufuku Nchini.Lakini iliniongezea kiu kukisoma
Hadi Muda Huu Kambona amesahaulika kwenye Historia.Ipo siku atarudi kwenye Historia ya Nchi hii.
Nilitegemea Barack Obama Road iwe Kambona Road au Shanty Town Moshi iwe Oscar Kambona Streat.Osterbay iitwe Oscar Kambona Streat.Taifa haliwezi kurithi maadui wa mtu mmoja.Ni ujinga na Uzuzu.Ni laana.Tutende haki
Wewe inaonekana ni mgeni humu ndani.Sikilizeni nyinyi vijana wa juzi halafu wavivu wa kusoma, kwa taarifa yenu nyerere ni mkosefu wa fadhila na mzee mshenzi hajawahi kutokea na hatatokea mzandiki kama yeye..wafuatao ndo walimkaribisha nyerere ndani ya mji huu na ndio wenye mchango mkubwa katika kuleta uhuru, abdulwahid sykes, aziz dossa, ally sykes, hassan bin ameir, john rupia,mshume kiate, suleiman takadiri, bibi titi mohammed, na kwa ufupi waislam ndo walichangia sana, na nyerere alikiri hilo wakati anawaaga wazee wa dsm mwaka 85, watu hata hamujui hotuba aliyotoa siku hiyo kazi yenu kuropoka tu...wazandiki nyie...nyere aliwatenga wote hao kwa ukosefu wa fadhila zaidi aliwatia kizuizini...kwa kuwasaidia nendeni mkasome kitabu cha mohammed said "maisha na nyakati za abdulwahid sykes" mtafaidika...
Hahahaaaaaaha..hahaaa haaa haaaa Mabikira wanatudhalilisha!!!!
Acha uongo eti alikuja kutubu weka ushahidi, kina Bibi Titi ndiyo waliomsaidia Nyerere na kumpokea TANU mpaka kuwa rais wa Tanganyika.
Hizo ni chuki za Nyerere kwa wenzake waliopigania nao uhuru kina Kambona.
Kama Kambona alikuwa anataka kumpindua Nyerere si angeweza kufanya hivyo wakati wanajeshi wameasi na Kambona alikuwa waziri wa ulinzi ndiyo aliyekwenda kumficha Nyerere huko Kigamboni.
Tatizo lenu ninyi waislam, mkishindwa hoja mnakua na vioja! Maneno meeeengi, facts zero, utendaji zero! Cheki mukulu JK, Mwinyi....tunawapuuza tu shwaain..
Ndugu yangu huyo Alhaj Mwinyi, kama umeamua kumuona kama ni Muislam tu na sio Rais wako Mstaafu wa Awamu ya Pili...basi una kazi kubwa mno ndani ya ubongo wako!?
Huyo Rais Mwinyi,si ndo alokuja kukutoeni tongotongo za macho na kukufundisheni kuvaa viatu vya maana badala ya kuvaa mipira michakavu ya motokari aka "makatambuga"...au mara hii mmeshasahau!? Kwi! Kwi! Kwi!
Huyo Mkristo mwenzio/mwenzenu unayemsifia Nyerere aka "Mwalimu";si alikuacheni mnatembea makende nje na wengine mkila nyasi kama kondoo na nchi nzima ilikua hoi bin taabani!?
Huo upuuzi woote wa hao Viongozi wachafu,mafisadi na wazandiki ambao ninyi Chadema/Wakristo mnalalamika humu mitandaoni-Jf kila kukicha kama vifaranga vya kuku...hujui yakuwa hiyo ndo mojawapo ya legacy ya yule Mkristo mwenzenu Nyerere!?
Unawezaje kuwalinganisha Marais wa nchi/pahala tena kwa kutumia vigezo vya kidini...khalaf ndo unajiita ati umesoma wewe!?
Kuna mengi ningekwambia/ningekufunza lakini nina shughuli za maana zimenibana hapa kiduchu....
Hizo myth zenu za kipuuzi/za kizamani mlizokua mnadanganywa na kubebwa na yule Nyerere zitakufikisheni pabaya...huna uwezo,nia,mbinu wala dhamira ya kuwadharau Waislam/Uislam...hizo nyakati ni zilipendwa!
Acha ujuvi na makhanatha ya kwenye keyboard!!
Kasome ujifunze...na pia punguza mihemuko na dharau/chuki za kidini!
Ahsanta.
Nyerere alikuwa smart sana kuliko hawa mujahedeen , many times over......niliwahi waambia Nyerere alikuwa njia, ubongo na kila kitu kwa Tanganyaika na Tanzania.
Bibi Titi alikuwa chakula mjini km wengine..ila Nyerere alimhitaji sana kuwakusanya akina mama wa Kiislam..ndio maana hadi leo wanawake wajingawajinga wapo kwa vile mama zao wajingawajinga walipata nafasi za bure na kuwarithisha.....Nyerere aliona bora kuwachapa viboko kuliko waachia hawa magaidi wakajenge kambi ya shida.
Hata haoa kina sykes sijui na nani....Nyerere aliwawatibulia ugaidi wao km Israeli anavyochelewesha Iran kupata silaja kwa kuweka uchafu ktk vinu , kuweka virusu ktk computer na kugereverse issue ilimradi basi.Ili wawe busy na ushirikina wakidhani wamelogwa.
Nyerere kuna mara alitumia mchawi mpe mtoto ,,,,,mara nyingine aliwatokea ghfla na kuwachapa maswali wasiyotegemea hadi wakapoteza mistari wanayomzeshwa kwa ajili ya ubishi km wanavyokariri ya Biblia wakshidnane na wakristu...
Huyo ni bibi titi na kawawa wake, ambao ndio best ktk waislama waliokuwa wanataka Tanganyika waislam waliokuwa wanataka uhuru.....sijui itakuweje wengine ambao ndio waliofikia weka mashrti ,bila hivyo wasingeingia kuongeza idadi aliyotaka nyerere ili kuweza wakabili UN kuwapa watanganyika uhuru wao.
Leo hii wapo busy kuwa sijui uislam , sijui sykes, sijui nini na nini.........Hawa uazao wa binamu nyama ya hamu ....hawana ubongo wa kuchagua pande sahihi wa ya historia kitu chohcote duniani..Watapiga kelele san aila wakikaa watakubaliana na mimi.
Ndugu yangu, mbona tena unaleta khadith za kitoto na kutaka kuiharibu hii thread...jaribu kujitofautisha na hao mbumbumbu wengine!
Mbona hata Waislam unaowataja/unaowashutumu nao pia wanalalama pita kiasi yakuwa hizo mitaa/Barabara takriban zoote wamepewa maluuni wengine tu wasiokua hata na history,asili au hata kujitolea muhanga na hilo jiji au nchi/Taifa letu!?
Unafahamu yakuwa mitaa michache mno hapo D'Salaam hiyo mnayodai ati ina majina ya Waislam; ilipewa majina hayo baada ya msukosuko na lawama nyingi toka kwa Waislam na wapenda haki wengineo hapo nchini!? Hii ilikua khasa kipindi cha Alhaj Hassan Mwinyi na Kitwana Kondo.
Ikumbukwe zaidi,yakuwa hao unaowaona ati ni Waislam... asilan hawakupewa majina ya hiyo mitaa sababu ya Uislam wao...hasha abadan!
Hao walikua ndo Vinara,Wanaharakati,Wafadhili na Wahenga wakuu wa kupigania ukombozi/harakati za kutupatia huo "Uhuru" wetu.
Zaidi ya hilo,takriban woote kati yao hiyo D'salaam/Mzizima ni kwao au ni kwenye asili yao...kwa hiyo hawakuwa ati ni wageni hapo kama wengineo wengi tu!...
Hata hivyo wengi mno kati yao wamesahaulika kwa makusudi kwenye hiyo "Official History" ya nchi hiyo kama alivyoitaka yule Nyerere!
Nafikri pia unashuhudia hata leo wakijaribu kutajwa kiduchu tu humu mitandaoni-Jf na kwingineko,basi hutokea Wajaaluta kadhaa kuwakashifu hao Mashujaa wetu,Wanaharakati na Wakombozi wa huo "Uhuru" wetu!?
Nakhis ni uzuri ifike wakti baadhi ya jamaa zetu wengi mpunguze jazba na mihemuko ya kidini japo kiduchu na kuzipisha hizo Ilm na busara zenu kufanza shugulize japo thuluthi...na hii ni kwa faida yetu soote na Taifa letu changa!
D'salaam,ni mmojawapo wa mikoa michache saana kama sio pekee hapo Tanganyika usokua na ubaguzi kwa watu woote...embu kachungulie huko mikoani kuna mitaa mingapi yenye majina ya watu wenye asili au kutoka D'salaam/Mzizima!?
Nyerere alichukua ile ilokua Independence Avenue nafikiri ndo akaipa jina la yule Mmakonde Terrorist wake...ambae bila ya shaka kama angalikuwapo mpaka leo basi wale washenzi/Politicians wa Western World labda nae pia wangemwita pale Dan Hague/The Hague akajibu charges - Crimes against humanity!? Kwi! Kwi! Kwi!
Kuna wakti nilitoa maoni na sababu/history kiduchu humu Jf,kupinga yule mpuuzi Mwai Kibaki kupewa jina la mmoja wa mitaa/barabara zetu maarufu hapo Mzizima/D'Salaam...matokeo yake nilishambuliwa vibaya mno tena bila hata ya mantik yoyote ile!?
Ahsanta sana.
kambona hakuwa muislamu na barabara za dar Es Salaam nyingi ziligawiwa kwa kufuatia dini ya mtu. kama wangefuata ukweli mtu kama Lupia angepewa barabara ya msimbazi!!
Mkuu we kweli mdini namna mnavyomchamba huyo bwana Nalli kuhusu maraisi Mwinyi na Jk,then unageuka na kumchamba Mwl Nyerere,hakika unanipa funzo moja ni ngumu sana kuiondoa imani ya mtu hata kwa mambo yalio wazi kabisa.Haya bana lakini usisahau kupeleka watoto shule,hasa za wagalatia watapata kitu pengine cha kuwasaidia.Msalimie Mohamed Said.Mapambano bado tunayaendeleza.
Nakumbuka those days tunakimbia mchakamchaka kwa kuimba Kambona ameolewa olewa olewa olewaaa, ameolewa kwa kuogopa, azimio azimioo la Arushaa, alafu inaendelea Kambona aah aah Kambona aolewa wapi aah aah huko ulaya....to be continuedAmini kapinga ngoma Gadafi kaimba wimbo maiti nayo yasema Aa! aacha Tanzania utaitambua
Maiti siyo mwingine ni Amini,
Na Aminii amini kapiga ngoma...
Kambona aliagiza Chipaka a Kamaliza,pindueni mkiweza nitawapeni mapesa,nikirudi safarini Uingereza!
Nani alitunga wimbo huu tuliimba tukiwa watoto?
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Nilijua nitaambulia japo kujifunza jambo, wapi! UDINI, CHUKI na USWAHILI umekujaa moyoni!
Haya tumekusoma, kimbia wahi msikitini au kijiweni mkapige DOMO maana ndo zenu!
Lupia,rafiki wa mwalimu,
Acha uongo eti alikuja kutubu weka ushahidi, kina Bibi Titi ndiyo waliomsaidia Nyerere na kumpokea TANU mpaka kuwa rais wa Tanganyika.
Hizo ni chuki za Nyerere kwa wenzake waliopigania nao uhuru kina Kambona.
Kama Kambona alikuwa anataka kumpindua Nyerere si angeweza kufanya hivyo wakati wanajeshi wameasi na Kambona alikuwa waziri wa ulinzi ndiyo aliyekwenda kumficha Nyerere huko Kigamboni.
JUMAMOSI Agosti 1, 1970 Mahakama Kuu ya Tanzania iliambiwa na mkurugenzi wa mashitaka jinsi Bibi Titi Mohamed alivyogharamia mapinduzi ya kumuua Julius Nyerere na kuiangusha serikali yake.
Mahakama iliambiwa kuwa Bibi Titi katika siku isiyojulikana aliitisha mkutano na katika kikao hicho, Michael Kamaliza alimshauri mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Leballo aende London kwa Oscar Kambona kumwomba atume fedha zaidi ili kufanikisha mpango wao wa mapinduzi.
Kamaliza alimtaka Chipaka amwandikie barua Kambona na kumtumia noti ya shilingi 10/- ili Kambona aitie saini ije isaidie katika kuwashawishi wabunge na baadhi ya mawaziri kumuunga mkono Kambona.
Noti hiyo pia ilikuwa isaidie katika kuchangisha fedha za mapinduzi na kuwashawishi watumishi wa TANU na NUTA kuipinga serikali.
Mkurugenzi wa mashitaka alisema; Kamaliza alimwambia Leballo kuwa hakukuwa na shaka wafanyakazi wa Tanzania wangeliunga mkono mpango wa mapinduzi kwa sababu Rais alikuwa amemwondoa (Kamaliza) kutoka NUTA kinyume cha matakwa ya wafanyakazi.
Leballo alikutana na Bibi Titi nyumbani kwake tarehe Juni 23 na mama huyo alimweleza alikuwa amekwenda Nairobi kwa muda wa siku nne na kwamba alimpigia simu Kambona kutoka Nairobi na kumtaka atume shilingi milioni moja (1,000,000/-) kwa ajili ya mapinduzi katika muda wa wiki mbili.
Titi akampa Leballo shilingi 400/- na kusema kwamba alikuwa amepokea shilingi 2,000/- kutoka kwa Kambona, 1,000/- za Chacha kwa matumizi madogo madogo. Titi alimwambia Leballo atampa shilingi 600/- baada ya siku chache na alifanya vile tarehe 26, Juni. Fedha hizo zilitolewa mahakamani kama ushahidi kamili.
Tarehe 28 Juni, Chacha alipanga kukutana na Leballo tarehe 30 Juni ili amjulishe Leballo kwa Meja Herman.
Chacha na Luteni Kanali Marwa walikwenda nyumbani kwa Leballo tarehe 30 Juni saa 3 usiku. Chacha na Leballo walikwenda katika chumba cha kulala na kumwacha Luteni Kanali Marwa sebuleni.
Huko chumbani Chacha alimwambia Leballo kwamba alikuwa tayari kuipindua serikali kama angelipwa shilingi 20,000,000 na akamtaka Leballo amwambie Kambona atume fedha hizo kwa haraka.
Leballo na Chacha walikutana tena tarehe 3 Julai huko makao makuu ya Jeshi kwa maombi ya Chacha. Chacha alimwambia Leballo kwamba alikuwa amesikitishwa na ukawiaji wa fedha.
Akamtaka Leballo aende huko Lugalo barracks katika bwalo la maafisa ambapo Kapteni Lifa Chipaka atamtambulisha kwa Meja Herman.
Leballo alikwenda kule, akamkuta Kapteni Lifa anamsubiri. Kapteni Lifa alimwambia Leballo kwamba hakuwa anamwamini Meja Herman katika mpango wa mapinduzi kwa sababu alikuwa chotara kutoka Iringa na kwamba yeye angempa orodha ya maofisa ikiwa pamoja na jina la mtu mmoja kutoka kisiwani. Kutoka kwenye orodha hiyo mtu wa kuongoza mapinduzi angechaguliwa. Baadaye Kapteni Lifa alimfahamisha Leballo kwa Meja Herman.
Baada ya mkutano huo Leballo alionana na John Chipaka na Kamaliza wakiwa pamoja katika ofisi ya shirika la wafanyakazi la NUTA. Wote walizungumza na kumtaka Leballo aende London kwa Kambona kumtaka atume fedha zaidi.
Kama saa kumi na robo alasiri siku hiyo Leballo aliitwa tena kwenye ofisi hiyo. Aliwenda na kumkuta Kamaliza peke yake. Kamaliza alimwambia kwamba alikuwa amemtuma mtu mmoja kwa Kambona U That akalete fedha.
Kamaliza akamwambia Leballo kwamba yeye alipendelea Meja Herman aongoze mapinduzi kuliko Chacha.
Washitakiwa saba ambao wamekana mashitaka matatu ya uhaini na moja kuficha siri ya uhaini ni Gray Likungu Mattaka, John Dustan Lifa Chipaka, Bibi Titi Mohammed, Michael Marshal Mowbrya, William Makori Chacha na Alfred Philip Millinga.
My take:
Kwa anaeijua historia vizuri ya BIBI TITI atujuze hapa
I try to answer the likes of you with silence and indifference...it works better,I assure you,than anger and silly argument/s!
Ahsanta.