Tujikumbushe: Bibi Titi alivyomwaga fedha kumuua Nyerere

Tujikumbushe: Bibi Titi alivyomwaga fedha kumuua Nyerere

Status
Not open for further replies.
“Leballo alikutana na Bibi Titi nyumbani kwake tarehe Juni 23 na mama huyo alimweleza alikuwa amekwenda Nairobi kwa muda wa siku nne na kwamba alimpigia simu Kambona kutoka Nairobi na kumtaka atume shilingi milioni moja (1,000,000/-) kwa ajili ya mapinduzi katika muda wa wiki mbili.

“Titi akampa Leballo shilingi 400/- na kusema kwamba alikuwa amepokea shilingi 2,000/- kutoka kwa Kambona, 1,000/- za Chacha kwa matumizi madogo madogo. Titi alimwambia Leballo atampa shilingi 600/- baada ya siku chache na alifanya vile tarehe 26, Juni”. Fedha hizo zilitolewa mahakamani kama ushahidi kamili.

.....ufisadi nchi hii ulianza zamani, kachukua 1m akadai kapewa 2,000/=.....duu, hii ni balaa...

JUMAMOSI Agosti 1, 1970 Mahakama Kuu ya Tanzania iliambiwa na mkurugenzi wa mashitaka jinsi Bibi Titi Mohamed alivyogharamia mapinduzi ya kumuua Julius Nyerere na kuiangusha serikali yake.

Mahakama iliambiwa kuwa Bibi Titi katika siku isiyojulikana aliitisha mkutano na katika kikao hicho, Michael Kamaliza alimshauri mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Leballo aende London kwa Oscar Kambona kumwomba atume fedha zaidi ili kufanikisha mpango wao wa mapinduzi.

Kamaliza alimtaka Chipaka amwandikie barua Kambona na kumtumia noti ya shilingi 10/- ili Kambona aitie saini ije isaidie katika kuwashawishi wabunge na baadhi ya mawaziri kumuunga mkono Kambona.

Noti hiyo pia ilikuwa isaidie katika kuchangisha fedha za mapinduzi na kuwashawishi watumishi wa TANU na NUTA kuipinga serikali.

Mkurugenzi wa mashitaka alisema; "Kamaliza alimwambia Leballo kuwa hakukuwa na shaka wafanyakazi wa Tanzania wangeliunga mkono mpango wa mapinduzi kwa sababu Rais alikuwa amemwondoa (Kamaliza) kutoka NUTA kinyume cha matakwa ya wafanyakazi.

"Leballo alikutana na Bibi Titi nyumbani kwake tarehe Juni 23 na mama huyo alimweleza alikuwa amekwenda Nairobi kwa muda wa siku nne na kwamba alimpigia simu Kambona kutoka Nairobi na kumtaka atume shilingi milioni moja (1,000,000/-) kwa ajili ya mapinduzi katika muda wa wiki mbili.

"Titi akampa Leballo shilingi 400/- na kusema kwamba alikuwa amepokea shilingi 2,000/- kutoka kwa Kambona, 1,000/- za Chacha kwa matumizi madogo madogo. Titi alimwambia Leballo atampa shilingi 600/- baada ya siku chache na alifanya vile tarehe 26, Juni". Fedha hizo zilitolewa mahakamani kama ushahidi kamili.

"Tarehe 28 Juni, Chacha alipanga kukutana na Leballo tarehe 30 Juni ili amjulishe Leballo kwa Meja Herman.

"Chacha na Luteni Kanali Marwa walikwenda nyumbani kwa Leballo tarehe 30 Juni saa 3 usiku. Chacha na Leballo walikwenda katika chumba cha kulala na kumwacha Luteni Kanali Marwa sebuleni.

"Huko chumbani Chacha alimwambia Leballo kwamba alikuwa tayari kuipindua serikali kama angelipwa shilingi 20,000,000 na akamtaka Leballo amwambie Kambona atume fedha hizo kwa haraka.

"Leballo na Chacha walikutana tena tarehe 3 Julai huko makao makuu ya Jeshi kwa maombi ya Chacha. Chacha alimwambia Leballo kwamba alikuwa amesikitishwa na ukawiaji wa fedha.

Akamtaka Leballo aende huko Lugalo barracks katika bwalo la maafisa ambapo Kapteni Lifa Chipaka atamtambulisha kwa Meja Herman.

"Leballo alikwenda kule, akamkuta Kapteni Lifa anamsubiri. Kapteni Lifa alimwambia Leballo kwamba hakuwa anamwamini Meja Herman katika mpango wa mapinduzi kwa sababu alikuwa chotara kutoka Iringa na kwamba yeye angempa orodha ya maofisa ikiwa pamoja na jina la mtu mmoja kutoka kisiwani. Kutoka kwenye orodha hiyo mtu wa kuongoza mapinduzi angechaguliwa. Baadaye Kapteni Lifa alimfahamisha Leballo kwa Meja Herman.

"Baada ya mkutano huo Leballo alionana na John Chipaka na Kamaliza wakiwa pamoja katika ofisi ya shirika la wafanyakazi la NUTA. Wote walizungumza na kumtaka Leballo aende London kwa Kambona kumtaka atume fedha zaidi.

"Kama saa kumi na robo alasiri siku hiyo Leballo aliitwa tena kwenye ofisi hiyo. Aliwenda na kumkuta Kamaliza peke yake. Kamaliza alimwambia kwamba alikuwa amemtuma mtu mmoja kwa Kambona "U That" akalete fedha.

"Kamaliza akamwambia Leballo kwamba yeye alipendelea Meja Herman aongoze mapinduzi kuliko Chacha".

Washitakiwa saba ambao wamekana mashitaka matatu ya uhaini na moja kuficha siri ya uhaini ni Gray Likungu Mattaka, John Dustan Lifa Chipaka, Bibi Titi Mohammed, Michael Marshal Mowbrya, William Makori Chacha na Alfred Philip Millinga.

My take:
Kwa anaeijua historia vizuri ya BIBI TITI atujuze hapa
Huyu mama alikuwa na moyo wa Gobachev.Ukomunisti wa nyerer ulikuwa kero kwa umma wa kitanzania kupita hata kutawaliwa na mtu kama mabutu seseseco. kama Bibititi mwamadi angefanikiwa mwaka 1970 basi haya yafuatayo yangetokea:

1-Ujamaa na kujitegemea(ukomunisti kufutika nchini
2-wanamuziki wangerudishiwa hati miliki na kujikluta matajiri sana
3-kiwanda cha santuri kingejengwa hapa nchini.
4-kingereza kingerudi mashuleni ya msingi.
5-Operesheni vijiji isingetokea
6-Mfale wa soka duniani angekuja hapa Tanzania
7-Yanga na simba zisingemekuga na kuzaa Pani na Nyota nyekundu
8-Tambwe Leya na Nabi Kamal wasingefukuzwa mwaka 1976.
9-Kombe la dunia 1970 tungeliona Live kwa TV na pele tungemshuhudia akicheza
10-Tusingevunja uhusiano wa kibalozi na Israel kuwaridhisha waarabu.
11-Kamata kamata ya vijana mitaani na kuwapeleka geza Ulole isingetokea kamwe.
12- Jiji la Dar Es Salaam lingekuwa linazoa takataka barabarani
13- Mtaa wa Independence ungebakia kama ulivyo na wala usingepewa kwa chizi na mhuni kama samora machel
14- Kusingekuwa na Palestina day-sherehe ya kutukana wayahudi.
15- Marehemu maulidi dilunga angekuwa mtanzania wa kwanza kuwa mchezaji wa soka la kulipwa mwaka 1970!

16-matembezi ya mshikamano yasingekuwepo wala ujamaa dina kila ijumaa pale CCM kivukoni.
17- kusingekuwa na kurudia rudia darasa la saba kwa watoto wa wakulima.
18- Pesa za umma na misaada ya sweeden isingetumika kujenga ukumbi wa mikutano chimwaga kwa mabilion ya pesa.
19- Tungekuwa na TV tangia mwaka 1970
20- Tungekuwa tunaongea kiingereza kama kenya na Uganda.

sasa wewe piga mahesabu baada ya Bibi titi kushindwa hayo niliyotaja ndiyo yaliyotukuta watanzania.
 
Mkuu Ben Saanane,

Nakuomba ukisome upya hicho kitabu, kisha soma marejeo ya mapito ya siasa za Mwalimu Nyerere, na mwisho soma mapito ya siasa za Tanganyika na Tanzania,

Mkuu Mag3 umenikumbusha jambo muhimu na la kilele cha helima za Mwalimu Nyerere,

Niliwahi kulisema siku moja hapa lakini wazito wa akili na mioyo waliinuka na kuweka kikinza
 
Naendelea kusoma kitabu cha The Dark Side of Nyerere.Kitabu hiki kilipigwa marufuku Nchini.Lakini iliniongezea kiu kukisoma

Hadi Muda Huu Kambona amesahaulika kwenye Historia.Ipo siku atarudi kwenye Historia ya Nchi hii.

Nilitegemea Barack Obama Road iwe Kambona Road au Shanty Town Moshi iwe Oscar Kambona Streat.Osterbay iitwe Oscar Kambona Streat.Taifa haliwezi kurithi maadui wa mtu mmoja.Ni ujinga na Uzuzu.Ni laana.Tutende haki

Mwanasiasa umkanye huyu panya buku atakuharibia kanyageni.
 
Last edited by a moderator:
kinamama kilikuwa taabu...NYERERE MUNGU AMWEKE PEMA... aliwajuwa sana hawa wanywa gahawa.Walikuwa busy kugombea rushwa za mzungu....km walivyorithishana hadi leo simba na yanga, ushuru wa masoko, misikiti kupinduliwa..hawakuwa na haja ya uhuru....walikuwa wakitaka bure ya mzungu, East Africa Muslim Welfare, kuchinja kwa Wakristu a kupiga ramli..

Bibi titi alikuw ana vikao kibao, leo katumwa na wanaojiita waislam wakipanga mpindua Nyerere, wakaimkaririsha mistari m ili yao ya ubishi, akifika kwa Nyerere ynakuwa uchafu yote na kujikuta akitakiwa eleza vikao vilikuwa vya nini.Hii ndio ilikuwa tabi aya waislam enzi ya uhuru...

Ndio wali mblack maila Nyerere hadi akaamua taifisha mashule ili kukata kiu n atamaa ya hawa jamaa wanaopenda issue zote za kubeba ndizi zilisvurugike kwa sababua ya uhuru.

Mheshimiwa jaribu kustabirize your mind usiwe kipofu. Watu watakudharau sana.
 
Acha uongo eti alikuja kutubu weka ushahidi, kina Bibi Titi ndiyo waliomsaidia Nyerere na kumpokea TANU mpaka kuwa rais wa Tanganyika.

Hizo ni chuki za Nyerere kwa wenzake waliopigania nao uhuru kina Kambona.

Kama Kambona alikuwa anataka kumpindua Nyerere si angeweza kufanya hivyo wakati wanajeshi wameasi na Kambona alikuwa waziri wa ulinzi ndiyo aliyekwenda kumficha Nyerere huko Kigamboni.

Mh Ritz,tunapenda sana kugeuza mambo,tatizo mnachanganya Udini,mtihani mkubwa ambao watu hatuutambui ni kwamba zama za mwanzo baada ya Uhuru karibu nchi zote za kiafrika zilipitia katika hali ya baadhi ya watu kutamani madaraka zaid ya waliyonayo,hivyo basi kwetu tulianza na Africanisation ya jeshini baadaye wakina Kambona and likes,kikubwa katika yote Nyerere was very strong and indeed brave leader,haliweza kudeal na mazingira hayo na ni ukweli ulio wazi hakuna kiongozi alyependa kuyaachia madaraka kipindi hicho,tuwe wakwel,Zanzibar Karume aliua,Kenya vilevile,Uganda ndo usiseme,hii ni mifano ya karibu tu.
Ni ukweli ulio wazi ukiondoa hilo la uanarakati la chin kwa chin la waislamu la kujiona kwamba walichangia sana kwenye uhuru wa nchi,na kuhitaji makubwa zaid,hapana shaka baadhi ya elite leaders wa wakati huo kama wakina Kambona waliona ni nafasi nzuri ya kutwaa madaraka.Bahati nzuri Nyerere was very clean.
Labda nimalize kwa kuuliza je kama hayo hayakuwepo katika Nyakati
hizo,maana yake ni nchi ilikuwa inaenda smooth,sasa nini kilitokea katika mpaka kufikia Nyerere kutomsamehe Kambona mpaka kufa kwake?
NB,Nyerere hakutonywa na Kambona kuhusu mahasi nakukimbilia Kigamboni.
 
Mkiambiwa msome historia ya nchi yenu hamtaki, mmekalia siasa tu za maji taka!

Kwanza msome Bibi Titi Mohamed ni nani? Tewa Said Tewa ni nani? na EAMWS ni kitu gani?

Ukifahamu yote hayo bila shaka utajua chuki ya Mwl. Nyerere kwa Biti Titi ilitokana na nini/au ilianzia wapi? mpaka kubambikiwa hiyo kesi iliyokua haina kichwa wala Miguu!

Nendene mkasome nyie watu Nyakageni ichenjezya Mag3 Mama JJ asigwa Nicholas Yericko Nyerere ili mpate faida.

Mkitaka darsa niko tayari kuwafundisha nyote bure bila hata ya senti kutoka kwenu!
 
Mkuu acha mihemko ya Kidini,Kwa nini mnapenda kujifaragua na mambo hayo,chuki ipi unayoizungumzia.Mambo yapo wazi,Nyerere hakuwa na uwezo wa Kimungu kufanya mambo yote bila kushirikisha watu,ni matumain yangu baadhi ya watu wapo mpaka Leo wakati wa Sakata lile,kwa nini basi msifanye utafiti wa kutosha na kuacha hayo mnayoyaamin?Je c kweli hawa watu walikuwa na tamaa?Mpaka mwaka 67,Kati ya Nyerere na hao watu Wako ni nani alikuwa na Mali zaid,maana hili lipo wazi.Ni kweli harakati za uhuru zilikuwa engineered na waislamu,sasa udhani haikuwepo hali ya kutaharuki baada ya uhuru kwamba nchi sasa imeanza kushikwa na wagalatia ambao ndo walikuwa elite?sasa katika mikinzano hiyo kwa akili yako unadhani watu wenye tamaa kama Kambona ambaye mpaka mwaka 1967 Ana nyumba tatu hawakutaka kutumia hali hiyo na hasa ukitilia maanani kwamba cku zote aliamin alipaswa kuwa waziri mkuu,kushika hatamu,na Afrika kote walikuwa wanapindua viongozi wao wa mwanzoni.Ukweli utabaki ukweli,Nina hakika kwa kuelewa mambo haya kamwe Mwl hakutaka kuongelea sana maasi yote,hilo la 64,hata hayo ya hao wakina Bibi Titi mpaka kifo chake,aliwapa nafasi wote na hasa walioshiriki waseme ukweli na nyie wanaharakati wa dini zenu mtie pilipili,lakin ukweli utajulikana cku moja.
RIP Nyerere with your colleague Kawawa.
 
Last edited by a moderator:
bila Nyerere kufanya hayo hii inchi ingekuwa pango la magaidi, shamba la wanyang'anyi. ukabila,ukanda, udini tuuonao sasa,maskini kupita maelezo last nchi ingegawanyika vipande..............udini si mzuri uukristo umeletwa na wazung na uislam umeletwa na waarabu pls watz wenzangu tusikubali kutumiwa, wametupa elimu lakini hatujui kuitumia mungu ibariki tz
 
Mkuu acha mihemko ya Kidini

Wapi nimetaja dini kwenye bandiko langu?

chuki ipi unayoizungumzia.Mambo yapo wazi,Nyerere hakuwa na uwezo wa Kimungu kufanya mambo yote bila kushirikisha watu

Mkuu, kasome ili ujue hao aliokua nao katika harakati za uhuru wa Tanganyika ni wa kina nani na nini kilitokea baadae? hiyo ni kwa faida yako, ukipenda uje wafahamishe wenzio.

.Ni kweli harakati za uhuru zilikuwa engineered na waislamu

Ahsante, kwakuwapa faida wana JF wasiolijua hilo ambalo umeandika!
 
kambona hakuwa muislamu na barabara za dar Es Salaam nyingi ziligawiwa kwa kufuatia dini ya mtu. kama wangefuata ukweli mtu kama Lupia angepewa barabara ya msimbazi!!

Ndugu yangu, mbona tena unaleta khadith za kitoto na kutaka kuiharibu hii thread...jaribu kujitofautisha na hao mbumbumbu wengine!

Mbona hata Waislam unaowataja/unaowashutumu nao pia wanalalama pita kiasi yakuwa hizo mitaa/Barabara takriban zoote wamepewa maluuni wengine tu wasiokua hata na history,asili au hata kujitolea muhanga na hilo jiji au nchi/Taifa letu!?

Unafahamu yakuwa mitaa michache mno hapo D'Salaam hiyo mnayodai ati ina majina ya Waislam; ilipewa majina hayo baada ya msukosuko na lawama nyingi toka kwa Waislam na wapenda haki wengineo hapo nchini!? Hii ilikua khasa kipindi cha Alhaj Hassan Mwinyi na Kitwana Kondo.

Ikumbukwe zaidi,yakuwa hao unaowaona ati ni Waislam... asilan hawakupewa majina ya hiyo mitaa sababu ya Uislam wao...hasha abadan!

Hao walikua ndo Vinara,Wanaharakati,Wafadhili na Wahenga wakuu wa kupigania ukombozi/harakati za kutupatia huo "Uhuru" wetu.

Zaidi ya hilo,takriban woote kati yao hiyo D'salaam/Mzizima ni kwao au ni kwenye asili yao...kwa hiyo hawakuwa ati ni wageni hapo kama wengineo wengi tu!...

Hata hivyo wengi mno kati yao wamesahaulika kwa makusudi kwenye hiyo "Official History" ya nchi hiyo kama alivyoitaka yule Nyerere!

Nafikri pia unashuhudia hata leo wakijaribu kutajwa kiduchu tu humu mitandaoni-Jf na kwingineko,basi hutokea Wajaaluta kadhaa kuwakashifu hao Mashujaa wetu,Wanaharakati na Wakombozi wa huo "Uhuru" wetu!?

Nakhis ni uzuri ifike wakti baadhi ya jamaa zetu wengi mpunguze jazba na mihemuko ya kidini japo kiduchu na kuzipisha hizo Ilm na busara zenu kufanza shugulize japo thuluthi...na hii ni kwa faida yetu soote na Taifa letu changa!

D'salaam,ni mmojawapo wa mikoa michache saana kama sio pekee hapo Tanganyika usokua na ubaguzi kwa watu woote...embu kachungulie huko mikoani kuna mitaa mingapi yenye majina ya watu wenye asili au kutoka D'salaam/Mzizima!?

Nyerere alichukua ile ilokua Independence Avenue nafikiri ndo akaipa jina la yule Mmakonde Terrorist wake...ambae bila ya shaka kama angalikuwapo mpaka leo basi wale washenzi/Politicians wa Western World labda nae pia wangemwita pale Dan Hague/The Hague akajibu charges - Crimes against humanity!? Kwi! Kwi! Kwi!

Kuna wakti nilitoa maoni na sababu/history kiduchu humu Jf,kupinga yule mpuuzi Mwai Kibaki kupewa jina la mmoja wa mitaa/barabara zetu maarufu hapo Mzizima/D'Salaam...matokeo yake nilishambuliwa vibaya mno tena bila hata ya mantik yoyote ile!?

Ahsanta sana.
 
Al akhy gombesugu,

Karibu kaka tupate nasaha zako japo kiduchu kwa muda huu ulojaliwa kuwa hapa!
 
Last edited by a moderator:
hao waliomkaribsha nyerere kwenye mji,kwanini wao walikaa mda wote huo bila kupata uhuru mpaka alipokuja nyerere..

Kiukweli waislam mna akili flani hivi za ajabu sana ambazo mnarithishana kizazi hadi kizazi..

Na ndiyo maana mwinyi na kikwete ndo ma-rais wanaosifika kwa kupindisha nchi wakati mkapa na nyerere wanasifika kwa kunyosha nchi..

Halafu changia kwa adabu, sawa?!! kama unataka matusi nenda kule MMU kwa wenzio!

Hizo kwanini hazitakusaidia kitu bila kua na ilmu, kasome ndugu ufahamu ukweli wa mambo!
 
Al akhy gombesugu,

Karibu kaka tupate nasaha zako japo kiduchu kwa muda huu ulojaliwa kuwa hapa!

Maulana Al Tayeb!

Asalaam Alaykum, Al Akhiy.

Wallahi,ndo nachungulia hapa kiduchu naona zile "Zah'ma Wa Min'karadas" ndo zimeshaanza!ahaaa!!

Naona unavyoshusha mipini yako kwa utaratibu!ahahaa!!

Ahsanta.
 
Sikilizeni nyinyi vijana wa juzi halafu wavivu wa kusoma, kwa taarifa yenu nyerere ni mkosefu wa fadhila na mzee mshenzi hajawahi kutokea na hatatokea mzandiki kama yeye..wafuatao ndo walimkaribisha nyerere ndani ya mji huu na ndio wenye mchango mkubwa katika kuleta uhuru, abdulwahid sykes, aziz dossa, ally sykes, hassan bin ameir, john rupia,mshume kiate, suleiman takadiri, bibi titi mohammed, na kwa ufupi waislam ndo walichangia sana, na nyerere alikiri hilo wakati anawaaga wazee wa dsm mwaka 85, watu hata hamujui hotuba aliyotoa siku hiyo kazi yenu kuropoka tu...wazandiki nyie...nyere aliwatenga wote hao kwa ukosefu wa fadhila zaidi aliwatia kizuizini...kwa kuwasaidia nendeni mkasome kitabu cha mohammed said "maisha na nyakati za abdulwahid sykes" mtafaidika...

Mwonee...huna hata haya lizee lizima badala ya kutoa taarifa hii km mwanahistoria unashambilia kwa hasira na jazba!

Si-bure! Udini umekujaa kinywani na moyoni! Hapo sijaona la ajabu, wala sijashangaa maana haraka haraka tu nilichokiona ni uhafidhina wa udini ndio ulokujaa moyoni!! Na hapa napata picha clear kabisa kuwa kama nyerere alifanya haya unayotuambia BASI alikua sahihi na aliona mbali sana kuwa mlitaka kuingiza suala la UDINI katika harakati za kudai UHURU wa nchi badala ya uzalendo na utaifa kuongoza harakati hizo!

Ni Mungu wa Mbinguni atuepushe na hili balaa la udini maana inaelekea wenzetu mnataka hii nchi yenye neema asitawalike! Acheni kulalamika, fanyenikazi, acheni uvivu, fursa sawa kwa wote ipo na zaidi shirikianeni na wenzenu kujiletea maendeleo kama taifa moja na sio kukaa vijiweni kutwa nzima kupiga domo tu!
 
kinamama kilikuwa taabu...NYERERE MUNGU AMWEKE PEMA... aliwajuwa sana hawa wanywa gahawa.Walikuwa busy kugombea rushwa za mzungu....km walivyorithishana hadi leo simba na yanga, ushuru wa masoko, misikiti kupinduliwa..hawakuwa na haja ya uhuru....walikuwa wakitaka bure ya mzungu, East Africa Muslim Welfare, kuchinja kwa Wakristu a kupiga ramli..

Bibi titi alikuw ana vikao kibao, leo katumwa na wanaojiita waislam wakipanga mpindua Nyerere, wakaimkaririsha mistari m ili yao ya ubishi, akifika kwa Nyerere ynakuwa uchafu yote na kujikuta akitakiwa eleza vikao vilikuwa vya nini.Hii ndio ilikuwa tabi aya waislam enzi ya uhuru...

Ndio wali mblack maila Nyerere hadi akaamua taifisha mashule ili kukata kiu n atamaa ya hawa jamaa wanaopenda issue zote za kubeba ndizi zilisvurugike kwa sababua ya uhuru.

Nicholas, your very right Sir!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom