Tujikumbushe Big Dogg Pose (BDP Kamili)

Tujikumbushe Big Dogg Pose (BDP Kamili)

Ndio video ya kwanza ya kibongo kali na kiwango . walitengenezewa na mjerumani.
Umenifanya niende youtube kuiangalia daah na ile style ya kugongesha miguu ilitamba sana
 
Mimi nimeutafuta ule wa Pig black unaitwa nini mnataka mazeeeeee.Sijaupata mpk leo
 
Wazee wa pafu kun ya pafu kuja mba? [emoji23][emoji23][emoji23] umenikumbusha mbali sana.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nimekumbuka huu mstar afu wanavuta fegi
 
Nina albam zao zote mbili za cassete hao jamaa nilikuwa nawaelewa kinomaaaa,
Aisee emb nifanyie mpango wa wimbo wao wa "kitambo kidog" nadhani utakuwa kwenye albamu yao ya kwanza.
 
BDP ni ma bloo zangu na majiran zangu hapa kino kwakwel baadhi ya member wa group hali zao mbaya haswa DREZ yan ni kama kadata anakunywa mpaka gongo amekongoroka sana,meno ya show ya mbele 5 hamna,anaongea mwenyewe tu muda mwingi...Isssa yuko kigambon alihama kabisa Kinondon shamba,Computer aliondokaga muda sana kino sijui alipo
Daah nikisikia habari kama hizi huwa nasikitika sana.
Wakati wanatoa wimbo wa "kitambo kidogo" na "rudi mpenzi" nilikuwa primary nakumbuka.
Aboubakar Sadiq akiplay kwenye redio nawahi kuzirekodi na matangazo humo humo.
Nikaziandika kwenye kidaftari changu. Yaani ile unaplay kidogo unaandika mstari mmoja then unaplay tena unaandika mstari unaofuta hadi wimbo wa dk 6 unaisha. Na kuna maneno mengine unakuta huwa hayasikiki vizuri basi unaandika hivyo hivyo tu.
Ukiuotea wimbo kwenye gazeti la Ijumaa sijui Tabasamu hapo ndo umetupa garasa.

BDP KAMILI.
 
BDP ni ma bloo zangu na majiran zangu hapa kino kwakwel baadhi ya member wa group hali zao mbaya haswa DREZ yan ni kama kadata anakunywa mpaka gongo amekongoroka sana,meno ya show ya mbele 5 hamna,anaongea mwenyewe tu muda mwingi...Isssa yuko kigambon alihama kabisa Kinondon shamba,Computer aliondokaga muda sana kino sijui alipo
Computer nilimuona maeneo ya kimara bucha
 
"wanagwaya gwaya wamekanyaga miwaya"

nakumbuka mashairi kama hayo ya BDP ila sikumbuki wimbo uliitwaje
Huu mstari si ulikuwa wa D Chief kwenye Yamenikuta ya GWM ft Sugu? Haikuwa kwenye ngoma za BDP.

Ova
 
FAGIO LA CHUMA crew na wenyewe wako wapi kwa sasa,one of my favorite group enzi hizo walikuwa na flow Kali sana.hakika zamani kulikuwa na vipaji
 
Ma jobless ilishutiwa kinondoni shamba na leaders...video iko youtube
Nakumbuka,hawa wana enzi zile tuliwabeba sana
Kuna siku nlikuwa kwenye garage ya masubaru mitaa ya ada estate
Drez alipita nkaonana naye alikuwa ameathirika sana na pombe

Ova
 
Back
Top Bottom