Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mr. PATEL and Mr. Dogo,,, hawa ma Mafia wawili wali run Forest Hill Secondary. Waliowahi kupita pale wanawajua since 1990's
Kuna siku nilitoroka airport Dogo alinitafuta siku nzima shenzi type. Umemsahau mtu m-bad makusi hakuna kucheka.
 
Sa umesoma shule zooote hizo🤔🤔
 
Kakufundisha pandahill au swilla sec
 
Nalimi a.k.a kocha wa Ifunda Tech Sec School
Mwakalindile a.k.a Brigedia Ifunda Tech Sec School

Hawa jamaa, inapokuja wakati wa wao kuwa walimu wa zamu, ni kwamba assembly hakuna kuchelewa..!! Ole wako
Nalimi a.k.a kocha wa Ifunda Tech Sec School

Nikajua ni mwanajf mwenzetu Don Kisando
 
Shelimo alitukuta Pugu 2007 jamaa alikuwa mpole na msataarabu. Baadae alikuwa Afisa Elimu Temeke
RIP mkuu aliiwezea sana Pugu hata ukiwa unadrop anakupa lift hadi town suala la simu shule zote wanakataza ila kwa Mwamba alikua anataka kila mwanafunzi awe na number yake ili akipata shida ampigie.
 
Kitu nilicho kigundua ma teacher wakali kupitiliza walikuwa na matatizo haya.
1. Uelewa wao wa masomo wanayofundisha ulikuwa mdogo hivyo ku apply intimidation method kufunika kaujinga kake.

2. Walitokea familia katili walitembezewa mboko utotoni kiasi hawakuweza kujitetea sasa wamekuwa hawana namna ya kulipiza kisasi kwa watesi wao na wana substute kwa kuwatandika na kuwa wakali kwa watoto wa shule.
3. Umalaya wa walimu wana wachalaza mboko hovyox2 ili siku akitaka kupita na kitoto cha kike kiwe kioga na kukubali kwa hofu ya mboko.
4. Ugumu wa maisha au tuseme kuwa na msongo wa mawazo.
 
Waliomaliza shule juzi juzi utawajua tu
 
S/master mbugani sec nimemsahau jina alikua na roho mbaya sana yule mtu, ijumaa tulikua tunatorokaga mapema sana sasa siku hiyo tukakutana nae pale mesi yeye akiwa kwenye boda boda.

Sasa akili zetu tukawa na mawazo hajatuona, kumbe alituona akamkariri mmoja akapotezea.

J3 akaingia darasan akamuinua jamaa na kofi zito sana, "simama taja wenzako nimewakuta msituni majambazi hamtaki shule" kwanza tulimwagiwa maji tukachezea kipigo kizito kwa kuchangiwa na walimu alafu tukapewa barua mje na wazazi.

Kidogo tufukuzwe shule, tuliishia kufyatua matofari ya kutosha kama adhabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…