Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine


Mwalimu Ndutila Mbalizi Secondary School huyu alikuwa nyoko nyoko ya hatari, na Mwalimu Adimeli mkali wa kiswali shule fulani nimeshau ila bangi alikuwa anavuta huyu mwamba, mwanae kama yupo ataonekana kwenye comment
 
Mwalimu wangu wa nidham alikuwa anafundisha physics alafu anakigugumizi ,, somo gumu mwalim mkali basi tabu tupu
 
Daah! Umenikumbusha mbali sana Mkuu,huyo Mwl.Masatu wa Mkwawa ni alikuwa mbabe kweli kweli , alikuwa Mwalimu wangu wa bweni la Shaban Robert East ,siku 1 usiku saa 7 natoka prepo nilikuwa na kiradio changu kidogo, vile naingi bwenini, nikisikiliza miziki ya juma nature mara pap nasikia Sauti mtu nyuma yangu ananiuliza wewe kwanini unapiga kelele wenzio wamepumzika si nikachukulia ni wanafunzi wananiletea utani, nikamjibu acha ufala. Basi nilikoswa na ngumi kama ya mandonga, Ile kugeuka kweli teacher huyo, nikazama uvunguni mwa kitanda, alipiga mateke mbao za kitanda mpaka saa 8 ila sikutoka. Saa nane na dakika kadhaa nikaibuka kutoka chimbo nikaenda kulala.
 
Hahahaha asbh tulikuwa tunaita kombolela kutukimbiza wachelewaji. Mgimwa hakuwa mnoko kivile.
 
Huyu Limbu aliishi nyegez kona?
 
😁😁😁 Huyu mwalimu mpande alikuwa mwamba sana. Siku ya kwanza ndio naingia form one alinikurupusha pale Karume House Dorm 33, mpaka nikakimbia mchakamchaka na kandambili. Mzee wa "Ee bwana, unajifanya mjanja, together you stand alone you gooo😁😁😁".
 
Masatu alinifundisha English one,Mgimwa Geography 2.Mgimwa alikua best sana.Kipindi hicho ni kijana wa miaka 17 hata sijaanza kuchakata mbususu.Umenikumbusha mbali enzi hizo Mkuu ni Mr Mbao
 
Ilikuwa ukimzingua mwl.Masatu anakupa makofi ya chapchap hadi uone nyotanyota!Shaban Robert East enzi hizo.Na mwl.Mgimwa katika malezi akiwa na "Miss Tanzania"!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…