Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Dah mwl mpande alikuwa noma Sana...asubuhi mchakamchaka ole wako akukute umelala bwenini
 
Muttakyamirwa aka SUPER COMMANDO
Mwamfupe aka UNYAMAUNYAMA

Hawa wehu walipatikana MAZENGO TECH SEC SCHOOL.
Wiki ya zamu zao tulikuwa tunaiona shule ya moto kama jehanamu vile.

Bila kumsahau mwl Mshumbuzi huyu alikuwa boya sana kwenye kipindi chake cha kingereza, ilikuwa akikukuta umezubaa tu anakuvuta shavu unanaswa bonge la bao mpaka unaona nyotanyota!

Nakumbuka alikuwa anakuja na novel flan yenye story ya mabala the farmer na ... The bus driver!
Yule fara alikuwa anatugawa kwenye magroup halafu anatuchanganya na watoto wa kike day scholer. Sasa sisi watu wa boarding tulikuwa wakaksi tunajiita wagumu hatushobokei mademu.

Mara paaap mshumbuzi huyu hapa akukute huoneshi ushirikiano kwa mademu anakuvuta shavu mkono wa kulia then upande mwingne anakushushia wepa la shoto matata sana tena mbele ya mademu maneeena zake mshumbuz...!
 
Hahahaha asbh tulikuwa tunaita kombolela kutukimbiza wachelewaji. Mgimwa hakuwa mnoko kivile.
Mkuu kumbe nawe ulisoma Mkwawa? Mkwawa ilikuwa balaa, hiyo kombolela isikie tu, mimi niliwahi jikuta nimekubwa na kombolela walimu wanne waliingia bwenini na viboko vya kutosha saa 1 asubuhi sisi tukiwa bado tunaoga tulikuwa washkaji kama 5 hivi , basi jamaa walitembeza bakora ivo ivo bila kujali mpo uchi, ilibidi tukimbie na kupanda juu ya dari la bweni hapo tukiwa na mataulo tu. jamaa walitusihi tushuke tuyamalize lakini tuligoma , tuliwapa sharti moja zito waondoke au tujirushe chini nje ya bweni tupasuke au tufe kabisa maana palikuwa parefu. Basi dogo mmoja alijirusha kweli ile kumchungulia dogo alitapakaa tamu kama kapigwa ngumi Sugunyo ya bmandoga, taya na meno vilikuwa vinadam, including pua, ilibidi walimu waache hiyo tabia ya kufanya kombolela baads ya hapo. tulikuwa tukiishi maisha mazuri tu, hata ukichelewa pared hakuna kombolela.
 
Masatu alinifundisha English one,Mgimwa Geography 2.Mgimwa alikua best sana.Kipindi hicho ni kijana wa miaka 17 hata sijaanza kuchakata mbususu.Umenikumbusha mbali enzi hizo Mkuu ni Mr Mbao
Mbao alikuwa na pigo kama za kiongozi flani mkubwa wa kiserikali.
 
Da! umetaja mwl Mpande umenikumbusha mbali saaana kwa kwa dada Asha!!!
 
Galanos Galaxy Msocha na mchaka mchaka yule Mzee alikuwa akinifatilia Sana kidogo nimpe za uso,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…