Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Rugalema a.k.a Kitanta - Kahororo sec (Bukoba)
Kiniga - Adolec sec (Karagwe/Kyerwa)
Sozi - Sahare sec (Tanga)
Mhagama - Kilosa sec/Kizu boys (Kilosa)
Mjuni/Israel Mkongo - Tambaza sec (Dar)
 
Mwalimu Odelli huyu mwamba alikua anafundisha Mafulala sec school
Watoto wa Swax wenyewe wanapenda kuiita shule yao Mafu Camp.
 
Mkuu Isack Malisa alikuwa mkuu shule gani? Mi nilimkuta Moshi tech. 1981 - 1984. The man was very smart. Nasikia alikuja kumuoa madam Oberlin wa biology. Waalimu wetu Hawa walitu-shape vizuri, Mungu awabariki, awarehemu waliotangulia. Kina Mpande, Nzohi, Kasenge, headmaster Malale etc.
Malisa alikuwa headmaster Moshi Technical kuanzia 1998, alipokea usukani kutoka kwa Kimario ambaye naye alipokea kutoka kwa Malale. Ni kweli mke wake alikuwa madam Orbelin. Nzohi alikuwa Mwalimu wa physics Pugu secondary kwenye miaka ya 2000’s hivi! Kwa sasa sijui yeye yupo wapi au kama yupo hai. Mpande nimeona wadau wakisema yupo anaishi pale Moshi mjini
 
🙏
 
Mkuu ulikuwa from four ipi? Form four 1 ya kina Peter Ngalya, 2 ya kina Anjela Joseph, 3 ya kina ya Yule kiranja masai, 4, ya kina Hamida aka jamaa wa Fitter and Turner, 5 ya kina Ronald Estomih aka mjomba au 6 ya kina McDonald?
Hivi Fred Dominick yuko wapi? Alikuwa hatari sana form I hadi III
 
Mkuu Isack Malisa alikuwa mkuu shule gani? Mi nilimkuta Moshi tech. 1981 - 1984. The man was very smart. Nasikia alikuja kumuoa madam Oberlin wa biology. Waalimu wetu Hawa walitu-shape vizuri, Mungu awabariki, awarehemu waliotangulia. Kina Mpande, Nzohi, Kasenge, headmaster Malale etc.
Shkamoo
 
Mr. Mshana Academic Master waliosoma Mbezi wanamjua huyu Mzee alikua mkali km pilipili na Mara ya mwisho naenda nilisikia alifariki kwa Kisukari, R.I.P ulale unapostahiri mwalimu
Hii "alale anapostahili" tunatumia kwa watu waliokuwa waovu wakati wa uhai wao.. sasa hadi kwa mwalimu naona sio poa boss.
 
Mkuu Isack Malisa alikuwa mkuu shule gani? Mi nilimkuta Moshi tech. 1981 - 1984. The man was very smart. Nasikia alikuja kumuoa madam Oberlin wa biology. Waalimu wetu Hawa walitu-shape vizuri, Mungu awabariki, awarehemu waliotangulia. Kina Mpande, Nzohi, Kasenge, headmaster Malale etc.
Duh, malisa hadi 2007 nilimuacha pale Technical
 
Walimu wakali hawamalizagi ualimu wao kwa amani, sijui kwa nini?
Wengi hufa vifo vibaya pia km maradhi ya moyo na kisukari au hupitia mateso tu km msongo wa mawazo,
Hii "alale anapostahili" tunatumia kwa watu waliokuwa waovu wakati wa uhai wao.. sasa hadi kwa mwalimu naona sio poa boss.
Kuna siku alinifanyia kitu kimoja sisahau maisha yangu yote, ndio maana nasema alale anapostahili
 
Man to man Ifunda tech. Huyu jamaa alikua mnoko mpaka basi yaani hata kama amevaa suit Kali Yuko radhi alale kwenye tope akikuvizia. Alimkimbiza jamaa Hadi kwenye madimbwi ya maji machafu alipomkamata akawa anampitisha Kila darasa anamtangaza. Kuna kipindi watu walichoka nae wakamuibukia usiku wakachoma nyumba bahati nzuri majirani(walimu wenzake) waliwahi kutoa msaada. Dah yule mkurya ni noma asee ila atatukumbuka sana mm na wanangu (swege na Joshua) kwa matukio tuliyomtendea.
 
Kuna mwamba anaitwa Morega Simon Mongate a.k.a double M, alikuwa mkuu wa Ndanda high school, Masasi sasa hivi nasikia amekuwa afisa elimu Kagera huko

Huyu mwamba alikuwa anaogopwa Hadi na staff wenzake, alikuwa anapenda usafi balaa yaani Bora ukutwe bweni umedodge kipindi kuliko ukutwe haujasafisha eneo lako la usafi

Mwalimu akimkuta darasani anafundisha wakat darasa likiwa chafu alikuwa anamuokotesha makaratasi huku wanafunzi wanaangalia

Usiombe ukamatwe na simu au local
Ndanda mwaka gani mkuu nimepita hapo
 
Nalimi a.k.a kocha wa Ifunda Tech Sec School
Mwakalindile a.k.a Brigedia Ifunda Tech Sec School

Hawa jamaa, inapokuja wakati wa wao kuwa walimu wa zamu, ni kwamba assembly hakuna kuchelewa..!! Ole wako
Dah umenikumbusha hao wazee ni noma Kuna mtu anaaitwa Hardson Lwago .. Mwenyewe anajiita mtoto wa kiume mgumu Lwago anakwmbia siku ukiona amevaa Buti ujue ni siku ya kuua kenge. Kuna kipengele yy anachapa pale pale alipochapa fimbo ya kwanza, zote zinatua sehemu moja.
 
Back
Top Bottom