Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Number 7 Kipingu yupi?Kama Co.Idd Kipingu wa Makongo hapo atolewe Maana hajawahi hata kumfinya mtu ukiachilia mbali kumchapa mtu!labda afande Miraji ndio alikuwa anatusumbua
 
Hatari sana..jamaa alikua mnoko kweli..nakumbuka ule wimbo wa mchakamchaka "man to man man to man....kipara chake kina magamba[emoji28][emoji28]...

Na Brother Lyimo (RIP) Majengo Sec jaman..that man duh! alikua anainyoosha shule si kidogo.
Na mwalimu Andrew Katto vp na upunga wake?
 
Hapo sawa. Hivi yule Babu wa wali (Mzee Ugegede) mchambuko bado yupo kweli...Mzee alikua anaupika wali kiufundi aisee. Sufuria kubwa ila wali unaiva safi kabisa. Hata kabichi na nyama alipika vizuri sana. Pia ugali safi kabisa.

Kiufupi Mzee alikua fundi wa mapishi na aliipenda kazi yake.
Karume ni Dom 31 to 40. Sikumaanisha dom 10. Nilificha tu, kiukweli nilikuwa Dom 34.
 
Kulikuwa na mwl. anaitwa Mrisho-alikuwa second master Moshi Tech. The man was neat and handsome. Mkewe (also beautiful) alikuwa nurse pale dispensary ya shule. Mrisho alikuja kupata ugonjwa wa akili, nilimkuta Mirembe hospital miaka ya 90. Mwenye habari zake zaidi p'se.
 
Nimeandika huu uzi baada ya kuwakumbuka waalimu wangu hasa wale wakuu wa miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni waliokuwa wakali sana wasiotaka masikhara kiasi cha kuweza kujulikana hadi mkoa mzima na kanda. Wafuatao walivuma sana kanda ya kaskazini;

1. Mwalimu Kibatala - Shule ya sekondari Karatu, Arusha.
2. Mwalimu Shayo - Shule ya Sekondari Arusha.
3. Mwalimu wa malezi Ilboru sec, jina limenitoka ila ana jina la kimasai. Waliosoma 1998 - 2001 wanaweza kumkumbuka.
4. Mwalimu Teti - Tanga technical Secondary school. Huyu mkuu wa shule ilikuwa sio poa...
5. Mwalimu Mpande - Moshi Technical Secondary School. Huyu mwalimu kwenye umisetta alikuwa tishio. Ukileta zako ni kibano unakula.
6. Munga - Kaloleni sec, Arusha.
7. Kipingu -
8. Mwalimu Masatu na Mgimwa - Mkwawa High School (complex)
Ongezeeni majina mengine tujikumbushe enzi za u-teenage.
Kuna thread humu ulishaanzishwa.
 
Mwalimu Bokasa Arusha sec school 1980
Mwalim Mrema Arusha Meru secondary school 1981
Mwalimu Tibikunda Bichwa Mzumbe high school 1984
Mwalim mkuu Nguema Mzumbe high school 1984
 
Back
Top Bottom