Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Maiko Katembo alikuwa na kipindi chake pia cha mkoa kwa mkoa. Alikuwa na mbwembwe nyingi ili wasikilizaji wampende maana alijua ngoma za makabila hazina wapenzi sana!!Ama kweli siku zimesonga mbele!!!
 
kipindi hiki ndio hamjataja "mashairi" msomaji Athuman Khalfan saa nane nane mchana!

Nilikuwa sikipendi... kikiisha hicho kipindi kinakuja kipindi cha ombi lako ambacho baade kilibadilishwa jina na kuwa chaguo la msikilizaji
 
Bila kusahau wakati wa Taarifa ya Habari saa saba Mchana Taarifa ya Kiongozi kuachishwa Kazi kwa Manufaa ya Umma hilo Lilieleweka Vizuri sana Na Watumishi kuwa Na Maadili na Nidhamu
 
Malenga wetu, du sikuwahi kukipenda hichi kipindi lakini ajabu nilikuwa napenda sana kusoma mashairi kwenye gazeti la uhuru walikuwa wanatabia ya kujibizana ana kama taarabu ya sasa.
 
Betty Chalamila sasa ni DC Betty Mkwasa,sambamba na Halima Kiemba, Shaaban Kisu nk. Ni wengi

[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji2] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

 
Nakumbuka kipindi cha kuripoti matukio,kilikua ni usiku kama sikosei ilikuwa saa 3 usiku,kuna Mwandishi mmoja alikuwa akiitwa Tumbo Risasi,nilikuwa namkubali sana
 
Nilikua napenda vipindi vyote kasoro malenga wetu kina mzee Andanenga. Nilivyovipenda zaidi ni mama na mwana, hisio sijui pitio la muziki, club raha leo show, pagu na pwaguzi, mazungumzo baada ya habari. Yule dada alikua akitunga hadithi kwa kutumia nyimbo ka ustadi mkubwa sana. Nakumbuka zaidi kipindi cha "ukulima wa kisasa". Kutokana na utoto nilikua sisikii vizuri baadhi ya maneno nikawa naimba "mwananchi mkulima alikakayoo, mwananchi mkulima alikakayooo..". Siku moja mamangu mdogo akaniskia naimba akacheka hadi machozi, ndo kuniambia ni "mwananchi mkulima wa kisasa yooo..
 
Duh....wee mkali..... umeukumbuka hadi wimbo wa sakina?
Nimesoma maneno tu sauti ikaja....Big up...you made my morning
nimefurahi zaidi kama nawe bado unakumbuka hizo vitu....enzi hizo ndo nimetoka kupima mkono kama ukipitia utosini unaweza kugusa sikio ili nijihakikishie kuanza std one.
 
Your correct. Nakumbuka nilivyunja mlango wa redio upande wa kuwekea kanda......niliweka kanda, kumbe haijakaa vizuri mie nikang'ang'aniza kufunga mlango, kutahamaki mlango umevunjika, kipigo nilichokipata kutoka kwa mother sitakaa nisahau
dah!Aisee ile milango kumbe tulivunja wengi!Nami nilikuwa naforce kanda ya Chaka chaka mlango ulipovunjika mdingi akanipa kisago.
 
Dada Sango upo wapi nakukumbuka Dom wakati mmehamishiwa kule na mmeo. Sauti ya Sango na Ahamed ilikuwa inakosha jamani. Dada Sango kama upo humu ni PM tujuzane ya zama zile.
Dada Sango Kipozi, wakati huo akiitwa Sango Othman Tuwa, alikuwa shule ni kwetu Muhimbili Mwaka 1975, kwenye kipindi cha watoto, Mimi ndio nilikuwa staa niliyesoma historia ya shule na kujibu maswalu Mengine. Nilkuwa std.VI
 
Kweli mkuu,uwezekano wa madogo wa leo kuelimika kupitia vyombo vya habari ni mdogo,nakumbuka wakati ule kulikuwa na vipindi maalum vya masomo kwa shule za msingi muda wa asubuhi,kama hukwenda shule siku hiyo ukizama humo unapata faida,siku hizi tunasikiliza JAHAZI.
 
Dada Sango Kipozi, wakati huo akiitwa Sango Othman Tuwa, alikuwa shule ni kwetu Muhimbili Mwaka 1975, kwenye kipindi cha watoto, Mimi ndio nilikuwa staa niliyesoma historia ya shule na kujibu maswalu Mengine. Nilkuwa std.VI
Mbona raha, mimi dada Sango nimekutana naye nikiwa nafanya kazi shirika la kigenin na yeye yupo RTD Dodoma pamoja na mme wake. Jamani sauti zao mpaka kesho zinasika. Dada Sango kumbuka ofisi opposit na manispaa ya Dom enzi zile niikuwa mdogo wako sisemi zaidi. Ukienda moja kwa moja unafika kwako na ofisi ya RTD Dom.
 

Kweli ndugu.....siku hizi mtangazaji maarufu ni yule anayeonesha umahiri wa kuhamasisha ngono......na ndio maana akili za vijana wetu zimeelekea kwenye ngono tu.....kwa kuwa ni mambo yanayosikika mara kwa mara na kuhamasishwa na vyombo vya habari......
Ki kiukweli tunajenga taifa la vijana wavivu wanaowaza ngono na starehe pasipo kuvuja jasho....,,
 
Siyo kweli. Amin alipigwa moja kwa moja toka vita ilivyoanza, japo kulikuwa na majibizano hapo Lukaya na mahali panaitwa Luweero na Kapeeka. Wakati wote huo, Ben Kuko alikuwa ni burudani tosha kwa ripoti zilizokuwa zibawakejeli askari wa Amin, unaweza kumlinganusha na Jerry Muro lakini kwa sauti ya Hemedi Kivuyo anapokuwa anainanga timu yenu iliyofungwa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…