Hapa patam sasa mumenigusa penyewe,mimi ni mmoja kati ya mteja mzuri toka kaanza kule makumbusho,alikua na package mbovu sana ila juice super A+..hata ofisini ilikua ndogo na mbaya.
Now ana grow, which ni kitu kizuri..ukitafuta uko juu zaidi ya miaka 3 ama minne nilikua msifiaji sana wa perfumes zake..
Ila kwenye ukweli lazima tuseme, marketing strategies zake A, branding and package A+..
Juice ni takataka, sitakaa ni nunue tena kwake, sasa hivi bei kafikisha 55k chupa kubwa hio sio shida,je kilichopo ndani kinastahili?sisi hatuna shida na hio package yake, je juice ina quality ile ile, na hii kuua quality ya bidhaa ndio inaua sana biashara za wabongo wengi, wakiwa juu wanachakachua sana wapate faida kubwa ila wanasahau ukimkimbiza mteja leo, kumrudisha ni ngumu sana.
Hizi chupa zangu mbili za mwisho naona kabisaa hii dhulma, amenidhulumu..
Ya kwanza nilisema labda bahati mbaya(aventus), ya pili nikasema nibadilishe nichukue black opium nayo ovyo.
Msiseme sikuwaambia..
Tujuzane machimbo mapya ya pima pima.