Tukiacha ushabiki wa kivyama na Unafiki, Hoja ya Spika haijajibiwa

CCM wanaongoza kwa kuwakumbatia maskini ambao maisha yao yanategemea kwa sehemu kubwa, kujipendekeza kwa viongozi wa chama hasa Mwenyekiti na Katibu.
Wanaiona CCM kama bahari na wao ni samaki. Kwamba hawawezi kupumua licha ya kuishi nje ya CCM.
Kwanini wanaishia kumdhalilisha Speaker Ndugai badala ya kuweka hoja zote mbili mezani?
 
Na hoja ya Ndugai ni ya msingi kwa sababu:
1. Sio uongo kwamba kuna nchi zimezidiwa na mikopo.
Mfano, jirani yetu Zambia tayari ni International defaulter. Na tayari kwenye management na bodi za mashirika yake matatu, kuna raia wa kigeni ili kurejesha mkopo wao kwa kusimamia mapato na matumizi ya hayo mashirika.
Sri Lanka pia waliachia bandari kwa mchina baada ya kuzidiwa na mkopo.
Mkopo wa Ujenzi wa Reli unawatesa jirani zetu wa Kaskazini.
2. Kutoa tahadhari juu ya mikopo, sio jambo baya hata kidogo. Ni kujibizana na kueleweshana.
Kudhalilishana, kuona kwamba watu wanataka kiti 2025; ni hofu tu ya madaraka na hofu ya kupoteza kitumbua. Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake hasa kwa swala la kitaifa kama hilo.
3. Wananchi wana haki ya kusikilizwa. Ni jambo la ajabu kuwasikiliza wale waliokuzunguka tu. Waliokuzunguka hawawezi kumwambia SSH ukweli. Ni kama ambavyo hawakumwambia JK ukweli juu ya Richmond Dowans na Escrow.
Hawakumwambia Mkapa ukweli juu ya EPA, Radar, Meremeta, Kagoda na Alex Stewarts.
 
Mkuu Stuxnet , thanks for this.
Huko nyuma niliwahi kuuliza
P
 
BAVICHA nao ni kama wamekua wajinga, sijui uelewa mdogo sijui ujinga, sijui ni stress
 
Acha matusi, nami nasema Kichaa uchwara pekee ndiye atampinga Ndugai maana ibara ya 18 ya Katiba inampa Uhuru wa kutoa maoni yake.
 

Kwahiyo nyie mpo kufuata upepo wa wajinga? Kama mlivyofanya kipindi cha Lowasa? Mwenye akili atafurahia kuona tuna Rais anayeweka wazi mikopo na matumizi yake.
 
Kwa akili yako ndogo na pumba ulizozoea kupost unadhani Ndugai hajui nakisi ya bajeti inapatikana vipi? Hoja ilukuwa kama kuna tozo zinazojenga madarasa kwa nini tukope? Tumia akili acha kujibu ishu kwa chuki.
 
What goes around comes around. Lisu naye Alisema wakitumaliza sisi itafuata zamu yao. Wahenga nao Ukila nyama ya binadamu huwezi wacha. Hata kama jobo anahoja kwenye hili ndio muda wa kulipia aliyotenda bungeni. Mungu hajawahi kulala ataendelea kutulipia hapa hapa mpk wasiojulikana pia.
 
Kwa akili yako ndogo na pumba ulizozoea kupost unadhani Ndugai hajui nakisi ya bajeti inapatikana vipi? Hoja ilukuwa kama kuna tozo zinazojenga madarasa kwa nini tukope? Tumia akili acha kujibu ishu kwa chuki.

Ni kweli kabisa usemayo, lakini Ndugai kakanusha kuwa hiyo sio hoja yake bali ni clip ya kutengeneza, kibaya zaidi kaomba msamaha kuhusu hoja hiyo. Hapo unatetea nini?
 
Kuomba msamaha kwake hakuondoi hoja aliyoiweka mezani

Ni hoja gani mahdusi aliyoiweka mezani? Ni mkopo huu wa Covid 19 stimulus package au mikopo yote? Kama yote, alikua wapi siku zote?
Inaleta ukakasi kidogo kuwa mkopo wa Covid19 uwe ni chanzo cha Nchi kuuzwa, wakati kuna mikopo kibao haikuhojiwa, ukakasi uko hapo
 
Shida ni approach yake. Hauwezi kupitisha jambo na kulibariki bungeni ukatoka nje kulikosoa, haiendi namna hiyo.
Bungeni unaweza kuwa na msimano tofauti na wenzako lakini hoja ikapitishwa kwa sababu wabunge wengi wanaiunga mkono. Hivyo kupitishwa hona sio sababu ya wasioitaka hoja hiyo kutoipinga nje ya bunge. Inawezekana Ndugai binafsi hakukubaliana na hoja hiyo ya mikopo kama kweli ilupita bungeni.
 
Shida ni approach yake. Hauwezi kupitisha jambo na kulibariki bungeni ukatoka nje kulikosoa, haiendi namna hiyo.
Msikilize vizuri ndugai jinsi vitu vya ajabu vinavyopitishwa bungeni, ndio utaelewa
 
Anajua huwa ni budget ya uongo yaan ni ilimradi liende tu, kwan ni mwaka gani hiyo bajeti iliwahi kutekelezwa?
 

Kama ni kweli kutokubaliana na mikopo ilikua ndio hoja yake, kwanini aombe radhi kwamba alieleweka vibaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…