Tukio gani baya ulilowahi kukutana nalo usiku?

Hayo matukio hata jioni jioni tu
 
Usiku ni mbaya ukiwa nje ila ni mzuri ukiwa kitandani umelala
haki ya nani, me Mungu akinijaalia nikafika ndani kwangu wakati kigeni kinanipuliza najiuliza kwamba wakati huu kuna mtu anakiona cha moto
 
bahati yako una akili😁
 
Tina alifanikiwa kukimbia umbali huo kweli?
 
Tukio hili hapa

Nimelala usingizi ila ndani ya usingizi najiona nipo macho kabisa yaani nimelala ila mwili wangu upo active, najiona natembea naenda kila sehemu naongea na watu nacheka nafurahi (nafurahi kweli nacheka ila nmelala) ila kuna jambo ndani ya usingizi linatokea ghafla naona kuna mtu ananifuata kwa nia ovu nakimbia kutoka nje naingia ndani mpaka chumbani kwangu ambako niliuacha mwili wangu ukiwa umelala,

Nimeingia chumbani chumba kikawa kina giza Totoro sasa nikiwa nashangaa huyu nani alielala (kumbe ni mimi nikawa nahisi ni mtu mwingine) mara ghafla yule alikua ananikimbiza nje akawa ametokea ndani, amepitia wapi mimi sijui, nikaanza kumfukuza "toooooka" "tooooooka" akawa anakuja upande wangu ananisogelea zaidi nikawa namwambia kwa sauti zaiiiidi "tooooooka", kumbe huku nimelala ni mimi naongea nikawa nimejigeuza niinuke nimfuate, nageuka kwa nguvu niende nikamsambalatishe vuuuupu najiona ni mimi ndie ambae nilikua nimelala, kumwangalia yule mtu simuoni kuangalia saa ndio kwanza saa 5 usiku

Sikulala tena hadi Swaaaalah Swaaaaalah

Niishie hapa..
 
Tina alifanikiwa kukimbia umbali huo kweli?
Goodthing ni kwamba TINA alikua kwenye athlete board ya uni(mwanariadha),hatumii kilevi halafu anaumbo dogo,mpare wa milimani halafu ni chembamba
 
pole, kabla ya kulala usali
 
Ila Arusha ina mbwa jamani 🤣🤣🤣

Si koko si wakufungwa 🙌

Mpaka kuna kipndi Njiro walianza kuwaua,, wanawatupia nyama yenye sumu.
 
Always kabla ya kuangusha mwili wangu iwe usiku iwe mchana hua napiga goti chini napiga dua zangu za kutosha, natoa shukurani km zote kwa Creator & our Maker, sijawahi lala bila kusali aisee hata siku moja
sasa mbona ukawa unasema toka badala ya kukemea kwa kutumia jina la Mungu wako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…