Mkuu visa ni vingi Sana hiki kimoja kiko kabisa kwenye familia yangu, hii NI kama karma fulani hivi! Baba yangu mkubwa alichepuka na mke wa jirani Yake kabisa na mwisho wa siku Yule mwanamke akashika mimba na akazaa mtoto ila ndo hivyo mumewe alimbakiwa na maisha yaliendelea. Sasa Yule mtoto ambae for now ni Kaka yangu kadri alivyokuwa anakua akazidi kufanana na mshua mpaka ikaja kujulikana kwamba huyo mtoto ni wa Fulani na mshua alipoulizwa na baba Yake ( babu yangu) akakiri kwamba ni kweli ila hajui cha kufanya maana atavuruga NDOA Yake na ya jirani Yake ila bahati mbaya kabla sekeseke halijapamba Moto mshua akafariki ghafla hivyo ni kama Ile ishu ikapoa. Badae mume wa Yule mama akashtuka na akambana mkewe mpaka akasema ukweli hivyo Jambo likawa lizo wazi kabisa kwa watu wote. Babu yangu akawaita Baba zangu waliobaki akiwemo Baba yangu akawambia inabidi wafanye utaratibu wamnunue Yule mtoto ( hapo alikuwa tayari mkubwa kama miaka 15 hivi) ila kabla hawajaliweka Sawa babu yangu nae akafariki hivyo mchakato ukakwama tena mpaka badae mtoto alipofikisha miaka 18 ndo alichukuliwa rasmi akaja kwenye familia yetu kama Kaka yetu and yes tunafanana maana sisi kwetu wengi wetu tunafanana. Mama Yake mzazi aliendelea kuishi na mumewe pamoja na yote alisamehewa ila sasa😆😆😆😆karma is a bitch Kaka yangu huyuhuyu baada ya kufika umri wa kuoa alijilipua alioa mwanamke ambae ni single mama japo alionywa Sana maana huyu binti alikuwa anajulikana ila alishupaza shingo akaoa hivyohivyo ( HISIA ZILIZIDI AKILI) na alimuoa Yule dada mtoto wake akiwa mdogo Sana jamaa akalea mpaka Dogo akakua basi wakapata na wao mtoto wao wa Kwanza ila kabla hajakua vizuri wakapata mtoto mwingine tena (walibebanisha watoto) ajabu huyu mtoto alipokua akawa anafanana Sana na first born wa yule dada aliyetoka nae kwao. Baadhi ya ndugu walianza minong'ono ila Mzee wangu alikemea vikali na akasema asije kusikia mtu anaongea chochote. Akazaliwa mtoto mwingine wa 3 sasa 😃😃😃😃nyie watoto wa kuiba wanafanana na wezi balaa nae akaja kufanana copyright na wale wengine wawili kwahiyo mtoto pekee aliyekuwa tofauti ni Yule waliyempata wa Kwanza kwenye ndoa yao. Sasa sekeseke likaja hivi juzi shangazi Yake na huyu shemeji yangu walikosana walipokuwa kwenye sherehe huko kwao na walitoleana maneno machafu Sana(familia ya huyu shemeji yangu Wana uswahili Fulani hivyo kutoleana maneno machafu kwao ni kawaida) si shangazi mtu akaropoka kwamba huyu shemeji ashukuru kapata mume asiye na makuu kwa umalaya wake kamzalia watoto wote wawili nje ya ndoa ila mume haelewi analea tu na huyu akiendelea kujifanya mjuaji atamsema baba halisi wa wale watoto mbele ya hadhara maana anamjua😆😆😆shemeji akawa mpole bwana na akamuomba aunt Yake asiendelee kuongea ila sasa tayari Wana familia na watu wengine waliokuwepo pale walishasikia, aunt alikasirika kupita kiasi mpaka akaropoka baba halisi wa wale watoto🥺🥺🥺ni ndugu kabisa wa yule shemeji (uncle wake)aisee ikawa balaa na maneno yakafika kwetu. Bro hakumuuliza chochote zaidi alimchukua Yule mtoto wake halisi akamhamisha shule akampeleka kwa shangazi yetu (PWANI) na yeye akasepa na nguo zake tu akamwacha mwanamke pale walipokuwa wanaishi mpaka Leo, hajawahi kuongea na yeyote kuhusu hili sakata ila alimwambia tu Mzee kwamba huenda dhambi ya mama yangu na Baba yangu inanitafuna hivyo nahitaji utulivu niweze kutubu . Mpaka Leo yupo huko kanda ya ziwa na ni bachelor mpaka sasa