Tukio gani limewahi kukutokea mpaka ukajisemea kweli Mungu yupo?

 
Daah aisee kweli Mungu yupo mkuu...!!
 
Kama tulivyokuwa tofauti kimtazamo, maumbile, Rangi n.k basi na akili, itikadi na uelewa wa mambo tunatofautiana pia.
Umechagua upande wako wa kutokuamini katika Mungu That's up to you.
But my advice try to research more and more usiishie kujifungia kwenye cage ya science tu, In this world there is thousand of knowledge and good enough all of them zinaishia ku prove Uwepo wa mungu na kutukuza matendo yake makuu.
Have a good jorney when you're ready to find the truth of God existence.
 
Kuna kipindi nilikuwa napitia madeni na pia majukumu kibao aisee kuna sehemu nilikuwa naombaga Kazi bila kuchokaaa na nilishasahau kama walitoa tangazo nikaomba.. Aisee Mungu yupo na Anaishiii ile Kazi sikuipata kwa akili zanguu kabisaa He is the Lord of Miracle tukumbuke kutoa sadaka na kushukuru kila tunapofanikisha ndugu zangu maana Tukiwa tunapitia Magumu huwa tunaweza sana nadhirii ila tukishapata tunasahau viapo na nadhiri hasa za kumtolea Mungu...!! Jumapili njema wakuu.
 

Kwa hiyo ulipata kazi ki masiala
 
Nilikutwa na mke wa jamaa kwenye nyumba ya jamaa, yule Yezebeli alinijaza kuwa anakaa mwenyeww kumbe jamaa alikua peace keeping Sudani


Jinsi nilivyopona kuanzie ile siku ukiniambia Jehovah Nisi hayupo nakuona bonge la zuzu
 
Aisee M
ngu yupo bhanaaaaaa
Daah aisee kweli Mungu yupo mkuu...!!
 
Nilidondoka toka kwenye meli(man overboard) bahar ikiwa imechafuka balaa alaf wale wapuuz walikua wanajua fika kuwa uogeleaj wangu ni wa mchongo lkn wakaishia kunitupia lifering tu


Ingawaje nilitoka nikiwa hai lkn mtanange wake ulikua si wa kitoto mbiringe iliyotokea hapo viumbe hai vilivyopo pale vyote vilikimbia


Baada ya zahma ile nikawa muumin mtiifu na kila uchwao lazima nitoe sadaka na silal bila kusal na ktk begi langu la safar lazima nibebe kitabu changu cha dini
 
Hapa hakuna ulichooneshwa na Mungu sista, wanaume wote tupo hivyo hatuna mwanamke mmoja. Hata ulienae Sasa hivi anafanya kimya kimya ni vile hujajua tu.
 
Acha tu. Nakosa cha kukiongelea.
Kwa kifupi maisha yangu yote, kwa kila hatua, kwa kila pumzi, yanadhihirisha uwepo wa Mungu.
 
Hebu leta hizo source zako za knowledge zinazo prove uwepo wa Mungu.

Hukatazwi kuwa na imani yako, Lakini ukianza kusema kuna source za kuthibitisha uwepo wa Mungu uzilete hapa tuzione.
 
Siku nilipanda bodaboda mshikaji nikiwa na my young brother kutoka kariakoo kwenda mbagala mida saa Moja jion kagiza kanaingia ilikua katika early stage wa ujenzi wa mwendokasi....

Boda boda aka overtake daladala akamulikwa na gari za upande wa pili hakawa haoni vizuri mm nikiwa katikati nikawa wa kwanza kuona Yale matofari makubwa yanayo block njia likiwa limelala nikataka noruke Ile boda kushangaa lahaula uso Kwa uso...

Miujiza pikipiki ikapanda mpaka upande wa pili ikiwa na mwendokasi bila kuanguka Wala kupotezaa uelekeo ilikua ni maeneo kati ya mission na Saba Saba kwa mpili watu wote hawakuamini kilicho tokea...................

Mdogo angu Kwa kukasirika na hasira alikataa kuendelea na yule bodaboda nikamwambia MUNGU NI MWEMA KATULINDA NA HII AJARI

JESUS IS LORD
 
Je tukio hili la kufaulu kidato cha Sita lina Thibitisha vipi uwepo wa Mungu na si mawazo yako tu ya kufikirika na imani?

Je vipi kama wasahishaji wa mitihani na wapangaji wa matokeo walifanya "Standardization" ya matokeo?
 
Ajali zingine zinazo tokea na kuua Watu wengi licha ya kwamba Abiria Husali na kuomba sana Mungu awa kinge na kuwa epusha na Ajali hiyo,

Je Huyo Mungu huwa ana walinda kweli?

Ndege ya precision Air iliyozama ziwa Victoria, Abiria walio pona ni kwamba Mungu aliwalinda?

Je Abiria walio kufa, Hawakuwa wana muomba Mungu na wenyewe wapone kama wenzao?

Huyo Mungu ana walinda kweli watu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…