Ni Mengi Mungu ametenda kwangu ila kwa hil tukio huw nawaza na kushkuru mpaka kesho. Kuna siku nilipigika yaani niliwamba na na kuchakaa sina pesa kabisa. Na wakati huo kodi ya kijiofisi changu na sehem ninayoishi zimebakiza siku moja ziishe, ukichek harakat zangu sina hata dalili ya kupata pesa nilipe kodi wenye nyumba tayari washaanza kunipigia simu, huyu wa Ofsi ambapo nilikuwa nalipa 210,000/= kwa miez mitatu anadai anaomba niwaishe kodi maana mtoto katimuliwa ada shuleni hvyo siku mbili zijazo anatakiwa kurud shule maana kule shule kuna zoez la ujazaji fomu flan zitafanyika siku hiyo maana alikuwa darasa la mitihani. Huyu ninapoishi yeye ni mfugani pia anadai vifaranga vya kuku tayari viko njiani vinakuja hvyo anategemea kodi yangu anunulie chakula cha kuku yeye nilikuwa nalipa 180,000/= kwa miez sita.
Ukweli nilikaa moyoni ile siku huk nikijisemeza Eeh Mungu kama upo kweli naomba uonekane sasa, niliendelea hvyo na ukweli sikuwa na tumain lolote la kibinadam maana nikiwaza kuipata hiyo pesa kwa pamoja bdo naona ni mtihani mkubwa sana nimeupata. Kama wasemavyo wengine kuwa matendo ya Mungu ni ya ajabu na hayaelezeki bas katika hili nilishindwa kueleza. Ikafika sik ya kulipa kodi na kuna kijimvua kilikuwa kinanyesha toka mida ya saa 11 alfajili na tayar saa tatu ila bado mvua inanyesha. Ikaingia namba mpya kwenye sim yangu ikawa inaita, naipokea alikuwa ni mdada akajitambulisha kuwa ni muasibu wa taasisi X na hii taasisi naifahamu maana nimewah fanya kazi kwao kwa mkataba na tayari mwaka ulikuwa umepita tangu niachane nao. Huyu mhasib aliniuliza kama mim ndiye anayenitafuta kwa kutaja majina yangu yote matatu, nikajibu kuwa mim ndimi haswaa, basi akanieleza kuwa anatambua kuw mkataba uliishia kipind flan lakin wao kuna makosa yalifanyika walikuwa wanaendelea kuniwekea mshahara wangu hivyo anaomba kama nina taarifa bas nimsaidie namna y kurudisha zile pesa, Nikil kuw sikuwa na faham chochote maana ile acount nilifungua kwa ajil ya kupokelea mshahara tu na sikuwa nimeunganisha kwa sim zangu kuw mshahara ukiingia bas niwe napata notifications flani hivyo baada ya kumaliza mkataba wangu na kupata mshahara wangu wa mwisho nilienda nikakomba wote na ATM CARD nikaitelekeza. Kwa maelezo ya yule dad nikamwambia kuw inawezekana ila naomba niende benk kuhakik maana sijui lolote, ilibid nitoke na mvua mpak bank na nikaomba statement, ni kweli nikakuta kuna tumilion kadhaa, nikampigia yule dada kumjuza kuwa ni kweli pesa ipo ila nina ombi kwake..
Ombi langu kwake lilikuw hvi. Huu ni ukwel mtupu wakati nafanya kazi kwenye taasisi ile kuna kipind ilitokea tatizo la kufanya malipo ya mishahara hivyo kuna watu wacheche mshahara haukuingia kabisaa kwa mwezi ule na mim nikiwa mmoja wa wahanga, nilifuatilia sana mpaka mwez ukapinduka ila sikuwa nimelipwa pesa yngu, mwez uliofuata ukaingia mshahara wa mwez husika na ikaendelea hvyo kwa miez mingine.. mpaka namaliza mkataba wangu niliendelea kufuatilia lakin sikupata majibu. Sasa ilipotokea hii nikaona ni sehem sahih ya kudai haki yangu. Nikamueleza kila siku kilivyotokea kule nyuma akaomba afuatilie atarud kwangu kunipa jibu. Ndugu msomaji pesa yangu wala sikuifikilia mara mbil nikaitoa na kwenda kulipa madeni yanyu ya kodi na nilifanya hvi kwa ujasili maana ile ilikuwa pesa yangu halali kabisaa na kuwa simzurum mtu, pesa yangu nilitoa na y kwao nikabakiza nikisubir maelekezo yke.
Toka siku amenipigia sim na kusema ngoja afuatilie zilipita siku mbil kimya, ikaj y tatu mara week ikabid nimpigie, nilimpigia sana na sim haikupokelewa nilipiga tena na tena takribani miez mitatu ila sim hazipokelewi, natuma text kuomba kupewa muongozo namna y kurejesha hzo pesa ila sikupata majibu yoyote chanya.. Hvyo baada ya takribani miez sita kupita bila majibu niliamua kuzitumia zile pesa na sasa ni miaka mitatu sijawah pokea sim yka. Hili tukio huw linakumbusha juu ya uwepo wa Mungu na naamin Mungu yupo.