Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Najua watu kibao waliosoma hii thread wamepitia app zao kuangalia salio la account zao??🤣🤣🤣Ni Mengi Mungu ametenda kwangu ila kwa hil tukio huw nawaza na kushkuru mpaka kesho. Kuna siku nilipigika yaani niliwamba na na kuchakaa sina pesa kabisa. Na wakati huo kodi ya kijiofisi changu na sehem ninayoishi zimebakiza siku moja ziishe, ukichek harakat zangu sina hata dalili ya kupata pesa nilipe kodi wenye nyumba tayari washaanza kunipigia simu, huyu wa Ofsi ambapo nilikuwa nalipa 210,000/= kwa miez mitatu anadai anaomba niwaishe kodi maana mtoto katimuliwa ada shuleni hvyo siku mbili zijazo anatakiwa kurud shule maana kule shule kuna zoez la ujazaji fomu flan zitafanyika siku hiyo maana alikuwa darasa la mitihani. Huyu ninapoishi yeye ni mfugani pia anadai vifaranga vya kuku tayari viko njiani vinakuja hvyo anategemea kodi yangu anunulie chakula cha kuku yeye nilikuwa nalipa 180,000/= kwa miez sita.
Ukweli nilikaa moyoni ile siku huk nikijisemeza Eeh Mungu kama upo kweli naomba uonekane sasa, niliendelea hvyo na ukweli sikuwa na tumain lolote la kibinadam maana nikiwaza kuipata hiyo pesa kwa pamoja bdo naona ni mtihani mkubwa sana nimeupata. Kama wasemavyo wengine kuwa matendo ya Mungu ni ya ajabu na hayaelezeki bas katika hili nilishindwa kueleza. Ikafika sik ya kulipa kodi na kuna kijimvua kilikuwa kinanyesha toka mida ya saa 11 alfajili na tayar saa tatu ila bado mvua inanyesha. Ikaingia namba mpya kwenye sim yangu ikawa inaita, naipokea alikuwa ni mdada akajitambulisha kuwa ni muasibu wa taasisi X na hii taasisi naifahamu maana nimewah fanya kazi kwao kwa mkataba na tayari mwaka ulikuwa umepita tangu niachane nao. Huyu mhasib aliniuliza kama mim ndiye anayenitafuta kwa kutaja majina yangu yote matatu, nikajibu kuwa mim ndimi haswaa, basi akanieleza kuwa anatambua kuw mkataba uliishia kipind flan lakin wao kuna makosa yalifanyika walikuwa wanaendelea kuniwekea mshahara wangu hivyo anaomba kama nina taarifa bas nimsaidie namna y kurudisha zile pesa, Nikil kuw sikuwa na faham chochote maana ile acount nilifungua kwa ajil ya kupokelea mshahara tu na sikuwa nimeunganisha kwa sim zangu kuw mshahara ukiingia bas niwe napata notifications flani hivyo baada ya kumaliza mkataba wangu na kupata mshahara wangu wa mwisho nilienda nikakomba wote na ATM CARD nikaitelekeza. Kwa maelezo ya yule dad nikamwambia kuw inawezekana ila naomba niende benk kuhakik maana sijui lolote, ilibid nitoke na mvua mpak bank na nikaomba statement, ni kweli nikakuta kuna tumilion kadhaa, nikampigia yule dada kumjuza kuwa ni kweli pesa ipo ila nina ombi kwake..
Ombi langu kwake lilikuw hvi. Huu ni ukwel mtupu wakati nafanya kazi kwenye taasisi ile kuna kipind ilitokea tatizo la kufanya malipo ya mishahara hivyo kuna watu wacheche mshahara haukuingia kabisaa kwa mwezi ule na mim nikiwa mmoja wa wahanga, nilifuatilia sana mpaka mwez ukapinduka ila sikuwa nimelipwa pesa yngu, mwez uliofuata ukaingia mshahara wa mwez husika na ikaendelea hvyo kwa miez mingine.. mpaka namaliza mkataba wangu niliendelea kufuatilia lakin sikupata majibu. Sasa ilipotokea hii nikaona ni sehem sahih ya kudai haki yangu. Nikamueleza kila siku kilivyotokea kule nyuma akaomba afuatilie atarud kwangu kunipa jibu. Ndugu msomaji pesa yangu wala sikuifikilia mara mbil nikaitoa na kwenda kulipa madeni yanyu ya kodi na nilifanya hvi kwa ujasili maana ile ilikuwa pesa yangu halali kabisaa na kuwa simzurum mtu, pesa yangu nilitoa na y kwao nikabakiza nikisubir maelekezo yke.
Toka siku amenipigia sim na kusema ngoja afuatilie zilipita siku mbil kimya, ikaj y tatu mara week ikabid nimpigie, nilimpigia sana na sim haikupokelewa nilipiga tena na tena takribani miez mitatu ila sim hazipokelewi, natuma text kuomba kupewa muongozo namna y kurejesha hzo pesa ila sikupata majibu yoyote chanya.. Hvyo baada ya takribani miez sita kupita bila majibu niliamua kuzitumia zile pesa na sasa ni miaka mitatu sijawah pokea sim yka. Hili tukio huw linakumbusha juu ya uwepo wa Mungu na naamin Mungu yupo.
Huyo ambaye yupo ambaye hana mwanzo wala mwisho na ambaye ni Muweza wa vyote vilivyopo ni nani?hapo umepatia mkuu maana hata maandiko ya kale yanakubali binaadam ni aidha ataziona neema za Muumba na kushukuru ama ataona vinginevyo atakufuru. Lakini haibadili kitu juu ya uwepo wake.. chagua chochote kinachokuudhi na useme kimetokea kwakua hakuna Muumba wake kisha unijijibu mwenyewe kimetokanaje sasa kisha ukipata kilipotokea jiulize tena nani yupo nyuma ya jibu ulopata, Yupo ambae hana mwanzo wala mwisho Mwenye kuweza vyote ili vyote viwepo.
Dereva alikuwa tatizo. Pole sanaNimeponea kifo mara kadhaa kwenye ajali . Ya kwanza niligongwa na bike ya wajeda nadhani nikiwa mdogo sana mwanzoni mwa miaka ya 2000 thanks god niliponea. Nyingine nikiwa dom tuliigonga semi trailer kwa nyuma pale kwenye mataa ya jamhuri tukiwa kwenye harrier. Ashukuriwe mungu ile trailer pale nyuma ilikuwa na ngao hivi la sivyo tulikuwa tunakusanywa kule chini ya tairi za semi. Tulitoka safe. Lakini nasikitika kusema the same guy alekuwa anaendesha haikupita miezi mitatu mbele alisababisha ajali tena iliyogharimu maisha ya mama na watoto 2 . Mmoja amekuwa crippled. It was sad kwa kweli.
ulimwengu ni vitu vingi ikiwemo hata wewe,muda,nishati na katani kwenye mipaka ya shambani hapo inabadili nini sasa kwamba vimetengenezwa vyote pamojaHuyo ambaye yupo ambaye hana mwanzo wala mwisho na ambaye ni Muweza wa vyote vilivyopo ni nani?
Kwa nini unadhani lazima iwe nani, na isiwe nini?
Huoni una lazimisha swali liwe lina onesha uwepo wa mtu fulani ambaye una ulizia ni nani,
Licha ya kwamba inaweza kuwa ni kitu, ambacho ni nini, badala ya ni nani ambaye ni mtu,
Ambacho kitu hicho ni ulimwengu wenyewe kuwepo tangu mwanzo na hata milele.
Huwezi kuamini, ila ni kweli huko kwenye Serikali Kuu sina yoyote naemjua wala anaenijua, na jina letu la ukoo ni yale rare sana na la kawaida lakini ombi langu lilijibiwa ndipo nilipoamini kweli wakati wa Mungu ndio wakati SahihiMkuu kweli haukua na connection? Au Surname yako ni famous, hongera lkn
Hakika ni Kubwa mno, daima ntamshukuru kwa matendo makuu aliyonitendea.Hii ni kubwa sana, Shukuru sana Mungu Mkuu.
Ujanijibu swali langu nimekuuliza wewe una akili?Hivi niki kwambia wewe Lidafo haupo, utakubali kwamba wewe haupo?
Uta kataa kwe vile unajiona na kujishuhudia kwamba Upo.
Sasa hapa tayari upo angalau kwa namna fulani, una onekana, una sikika na una shikika.
Kwa namna zote tatu, upo.
Upepo hauonekani ila upo kwa kusikika na angalau kwa namna moja ya kusikika, tunatambua kwamba Upepo upo.
Sasa Mungu Yupo kwa namna gani?
Unathibitishaje Mungu yupo na si mawazo yako tu ya kufikirika?
Weeeeee Bado hujakutana na msala Kila mtu anakukimbia weeeeee acha kabisa Mungu yuko jamaniHonestly binafsi bado sijamuona.
nimeomba sana katika maisha yangu ila haikusaidia kutatua matatizo yangu. Nilichokuja kugundua Maisha ni effect after effect.
Ukiwa na shida usikimbilie kuomba, shirikisha watu utapata msaada.
kuamini kwamba mungu anasaidia,
for me is just betting.
Mimi ndio nimekuuliza swali how come unaniuliza tena mimi swali.Akili kama ipo, ipoje?
Thibitisha Akili ipo.
Kama msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika then its better kuamini kuliko kutokuamini .Tangu mwanzo pale, Nilikwambia kwamba,
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika.
Ukisha pata proofs, evidences na uthibitisho wowote ule kuhusu kitu fulani, Hiyo inakuwa si imani tena bali ni ukweli.
Labda nikupe mfano...
Mwanafunzi akifanya mtihani na akaweka lengo la kupata Alama "A" Hapa anakuwa na imani kwamba mtihani huu anaweza akapata alama "A" kwa vile, Hana uhakika wa jinsi gani majibu ya mtihani yatakuja.
Pengine anaweza kupata alama "B" kwa vile hakuwa na uhakika.
Ila mwanafunzi huyu huyu baada ya kurudishiwa mtihani na akawa amepata alama "A" Hapa Haitaji awe na imani kujua kwamba amepata alama "A" kwa vile ni ukweli na anaona kabisa, ushahidi upo kwamba ana alama "A"
Kwa hiyo imani ina endana na kutokua na uhakika juu ya jambo fulani.
Hata kusema Mungu yupo bila uthibitisho wa kuonekana angalau kwa namna fulani ni mawazo ya kufikirika tu.
That is another topic, Na inahitaji uwe na elimu ya thiolojia kujua why religion contradict .
Ila kwa ufupi ni kuwa pamoja na ku contradict kwa imani lakini imani zote hazipingi juu ya uwepo wa Mungu na hapa na maanisha abrahamic religion i.e Islam, Christian and Jewish. Zote zinakubali juu ya uwepo wa mungu
SafiNilikuta msg za mapenz anachat na rafiki yangu akaninyakua cm akafuta ushahidi akakataa hana mahusiano nae, Mungu alivyomkuu baada ya wiki 1, wakajirecord wanaongea mambo ya mapenz na jinsi mechi ilivyokua na hawakujua kama cm inarecord....nikaja sikiliza kilakitu
Hasaidii sababu hayupo, wanaopata hivyo vitu wanavyodhan ni sababu ya kuomba ni uongo bali ni matokeo ya wao kuvifanyia juhudi+pia misaada ya watu wengine... Mungu hana muda na shida za watuHonestly binafsi bado sijamuona.
nimeomba sana katika maisha yangu ila haikusaidia kutatua matatizo yangu. Nilichokuja kugundua Maisha ni effect after effect.
Ukiwa na shida usikimbilie kuomba, shirikisha watu utapata msaada.
kuamini kwamba mungu anasaidia,
for me is just betting.
Swali lako ni swali la pili baada ya mtu kuwa na majibu ya swali la kwanza.kama zinakubali juu ya uwepo wake,kwa nini zinamtafuta kwa namna tofauti huku kila mmoja akimuona mwenzake kakosea?
Samahani wewe ni dini gani?Mungu yupo aisee ! Ila anajua kututesa Sana huko aliko .
Nakubalii , ila utendaji wake binafsi siulewi kiaina.
Kuna wakati nikiwa napangalama na mishe zangu Mambo hayaendi [emoji16] ila anagalau nakua na amani.
Ila nikijifungamanisha na imani Mambo Ni tofauti Sana . (Ndio kabisa Yana stop)
Nauliza, ndugu washuhuda, ninyi mnaombaje mpaka mnashuhudia na imani zenu kuongezeka na kumfurahia katika majira yote, mkikosa sawa mkipata sawaa.
Mbaya zaidi, ata ndugu , Wanakomaa na Mungu lakini wapii
Umasikini juu ya umasikini [emoji16] , wazee wamezeeka wanategemea Watoto na Watoto nao wapi umasikini hata kusaidiana tu shida .
Kunatukio moja, lilitokea , Ni baya Kila mtu alilia kivyakee [emoji16].
Naulizaa Mungu huyu hamuoni anaupendeleoo ?
(Japo imani inanifundisha Hana upendeleo)
Ilaa inakuajee jamani wengine tunakaribia kuzeeka hatuna hizo shuhuda ?
Zinatoke Ni mbaya mbaya mbayaa .
Watetezi wa Mungu naombeni miongozo .
Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
uyu n mm aseeeKatika dunia tunapitia mambo mengi ya huzuni na furaha, ya amani na magomvi vipi katika maisha yako jambo gani limewahi kutokea na ukajisemea kweli Mungu yupo.
Binafsi ni jinsi nilivyo faulu kidato cha sita yaani daah!
Nikikumbuka naishia kusema kweli Mungu yupo na anatenda maana nilijua nikijitahidi sana ntakuwa na division 3 ila asilimia kubwa nilijua hii ni division 4 lakini matokeo yalivyokuja daah! Sikuamini niliishia kusema kweli Mungu yupo kwani nilifaulu vizuri.
Vipi wewe kwa upande wako please share experience.
ANGALIZO: Wale wazee wa Mungu hayupo tafadhali hii sio thread ya ubishani juu ya uwepo wa Mungu so pita kimya kimya tu.