Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni mambo mengiUnaweza ku share Ni vitu gani ulivyoonyeshwa?
Mkuu,Katika dunia tunapitia mambo mengi ya huzuni na furaha, ya amani na magomvi vipi katika maisha yako jambo gani limewahi kutokea na ukajisemea kweli Mungu yupo.
Binafsi ni jinsi nilivyo faulu kidato cha sita yaani daah!
Nikikumbuka naishia kusema kweli Mungu yupo na anatenda maana nilijua nikijitahidi sana ntakuwa na division 3 ila asilimia kubwa nilijua hii ni division 4 lakini matokeo yalivyokuja daah! Sikuamini niliishia kusema kweli Mungu yupo kwani nilifaulu vizuri.
Vipi wewe kwa upande wako please share experience.
ANGALIZO: Wale wazee wa Mungu hayupo tafadhali hii sio thread ya ubishani juu ya uwepo wa Mungu so pita kimya kimya tu.
Hicho kinachokupa kiburi ni uzima ulionao,lakini ipo siku utalia na utatamani siku zirudi nyuma lakini utakuwa umechelewa.Mkuu,
Hapo hata wasahihishaji wakikosea na kukupa matokeo mazuri ya mtu mwingine tu, tayari kwako ishatosha kuthibitisha Mungu yupo?
Hujajibu swali langu la wasahihishaji kukosea kutoa majibu.Hicho kinachokupa kiburi ni uzima ulionao,lakini ipo siku utalia na utatamani siku zirudi nyuma lakini utakuwa umechelewa.
Hii ni imani, ni haki ya kila mtu kuamini atakavyo.Mi kila nikiangalia angani, hasa usiku. Huwa nasema Mungu yupo.
Anakupenda ,na anataka ubadilishe avatar Yako!2017 nilichomwa visu saba nikiwa eneo hatari zaidi duniani delft ndani ya capetown..lakini sikufa mungu ni mkubwa.
Kwa level uliyofikia ni kazi bure kukuelimisha maana upo katika kiwango cha juu zaidi cha upagani,kwasasa ni Mungu tu( ambaye unasema hayupo)ndio wa kuingilia kati ili uokolewe.Hujajibu swali langu la wasahihishaji kukosea kutoa majibu.
Pia, tuseme ulichoandika ni kweli, siku moja nitalia na kujuta.
ikiwa kweli nitalia na kutamani siku zirudi nyuma, ulimwengu ambao unaruhusu watu kulia na kutamani siku zirudi nyuma kwa namna hiyo, ni ulimwengu ambao unathibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Ulimwengu ambao Mungu huyo yupo, hauna kilio wala kutamani vitu visivyowezekana. Kwa sababu Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na kilio na majuto ni contradiction.
Kwa kuangalia mambo juu juu tu, unaweza kuona una hoja ya kuukubali uwepo wa Mungu.
Lakini, kwa mtu anayeangalia mantiki kwa kina, hata kama unachosema kitatokea, kitatokea kweli, kutokea kwa hicho kitu kutazidi kuthibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote hayupo.
Kwanza kabisa, inaonekana una elimu finyu.Kwa level uliyofikia ni kazi bure kukuelimisha maana upo katika kiwango cha juu zaidi cha upagani,kwasasa ni Mungu tu( ambaye unasema hayupo)ndio wa kuingilia kati ili uokolewe.
Hiyo hoja ya "ni kazi bure kukuelimisha" kiukweli imetajwa hata kwenye Quran.Kwa level uliyofikia ni kazi bure kukuelimisha maana upo katika kiwango cha juu zaidi cha upagani,kwasasa ni Mungu tu( ambaye unasema hayupo)ndio wa kuingilia kati ili uokolewe.
Kina ninavyozidi kufahamu habari za nyota, galaxies na ulimwengu kwa undani ndivyo ninavyozidi kuamini kuwa Mungu yupo(Nikimaanisha nguvu inayojitambua iliyopanga na kutengeneza vitu hivyo) Kadri ninavyovichunguza ndivyo ninavyoona kuwa kuna uwezekano mdogo sana kwamba vikitokea bila kupangwa.Hii ni imani, ni haki ya kila mtu kuamini atakavyo.
Lakini hakuna factual and logical evidence hapo ku connect anga linavyoonekana na Mungu kuwapo.
Watu tunapenda kutoa majibu rahisi kwa maswali magumu ambayo hatujui majibu yake.
Unaangalia angani usiku.
Unaona nyota nyingi, mwezi, pretty cool.
Unajiuliza, hizi nyota zimekaaje huko juu bila kudondoka? Zimetokeaje?
Unasema sijui. Sasa hapa ndipo tatizo linapoanzia.
Wenzetu wakifika "Sijui", wanafanya utafiti kujua nyota zinaanzaje, kwa nini zinakaa juu hazidondoki chini, wanajua gravity, wanajua light ina kasi gani, wanajua space, wanajua kwa nini nyota zinang'aa, wanajua hesabu za nuclear fusion zinazotokea katika nyota, wanajua elements zinavyokuwa formed kwenye nyota, wanajua umbali kwenda kwenye nyota in light years, nyota hii ina element gani kwa kuangalia mwanga wa nyota. Wanajua nyota hii imekuwa formed miaka mingapi iliyopita, na itaishi miaka mingapi ijayo kabla haijasambaratika.
Wanasoma kwelikweli kutafuta majibu, kwa fact, kwa logic.
Na hata wasipopata majibu yote leo, wana a self correcting process that converges to the correct answers as time goes. Science.
Sisi wengi tunaangalia nyota na kuishia kwenye jibu la Mungu yupo.
Tumemaliza mchezo hapo.
Mungu anaangalia moyo sio avatarAnakupenda ,na anataka ubadilishe avatar Yako!
Kuamini si issue. Unaruhusiwa kuamini, uongo, ukweli. Ni haki yako ya kikatiba.Kina ninavyozidi kufahamu habari za nyota, galaxies na ulimwengu kwa undani ndivyo ninavyozidi kuamini kuwa Mungu yupo(Nikimaanisha nguvu inayojitambua iliyopanga na kutengeneza vitu hivyo) Kadri ninavyovichunguza ndivyo ninavyoona kuwa kuna uwezekano mdogo sana kwamba vikitokea bila kupangwa.
Inahitajika imani tu. Kama wewe umeona nafsi yako imeridhika na ushahidi unaaonyesha kuwa babu yako aliumba ulimwengu unaruhusiwa kuamini hivyo. Kwangu mimi mpangilio wa ulimwengu unatosha kuniaminisha kuwa kuna aliyeuumbwa na haukotokea hivi hivi bila kupangwa.Kuamini si issue. Unaruhusiwa kuamini, uongo, ukweli. Ni haki yako ya kikatiba.
Ila, hujaweka ushahidi wala uthibitisho kuifanya imani yako hiyo ipate hadhi ya kuwa ukweli.
Hata mini naweza kusema kila ninavyoangalia habari hizo napata Imani kuwa babu yangu mzaa mama ndiye aliyeviumba vyote hivyo.
Hilo halifanyi imani hiyo iwe ukweli.
Kama unataka twende kwenye ukweli, thibitisha mambo.
Kama unataka imani tu, unaruhusiwa kuamini chochote.
The appearance of created order does not mean the order is created.
Inawezekana your window of observation of the universe give you that illusion of created order.
Kuna bwana mmoja mvuvi. Alikuwa anatafuta size ya samaki wadogo kabisa katika sehemu ile ya bahari.
Akatumia nyavu ya matundu ya ukubwa wa unit 1.
Akashindwa kukamata samaki wadogo kuliko wa ukubwa wa unit 1 (kwa sababu walipenya katika nyavu, hawakushikwa)
Akaishia kuhitimisha kuwa samaki wadogo kabisa katika bahari ile ni wa ukubwa wa unit 1.
KWa sababu hakuweza kukamata wadogo zaidi.
Kumbe hakujua kuwa conclusion yake ilitokana na nyavu aliyotumia tu.
Na wewe umefanya kosa lile lile la yule mvuvi.
Lakini mimi siongelei imani.Inahitajika imani tu. Kama wewe umeona nafsi yako imeridhika na ushahidi unaaonyesha kuwa babu yako aliumba ulimwengu unaruhusiwa kuamini hivyo. Kwangu mimi mpangilio wa ulimwengu unatosha kuniaminisha kuwa kuna aliyeuumbwa na haukotokea hivi hivi bila kupangwa.