Tukio gani limewahi kukutokea mpaka ukajisemea kweli Mungu yupo?

Katika dunia tunapitia mambo mengi ya huzuni na furaha, ya amani na magomvi vipi katika maisha yako jambo gani limewahi kutokea na ukajisemea kweli Mungu yupo.

Binafsi ni jinsi nilivyo faulu kidato cha sita yaani daah!

Nikikumbuka naishia kusema kweli Mungu yupo na anatenda maana nilijua nikijitahidi sana ntakuwa na division 3 ila asilimia kubwa nilijua hii ni division 4 lakini matokeo yalivyokuja daah! Sikuamini niliishia kusema kweli Mungu yupo kwani nilifaulu vizuri.

Vipi wewe kwa upande wako please share experience.

ANGALIZO: Wale wazee wa Mungu hayupo tafadhali hii sio thread ya ubishani juu ya uwepo wa Mungu so pita kimya kimya tu.
Mkuu,

Hapo hata wasahihishaji wakikosea na kukupa matokeo mazuri ya mtu mwingine tu, tayari kwako ishatosha kuthibitisha Mungu yupo?
 
Hicho kinachokupa kiburi ni uzima ulionao,lakini ipo siku utalia na utatamani siku zirudi nyuma lakini utakuwa umechelewa.
 
Hujajibu swali langu la wasahihishaji kukosea kutoa majibu.

Pia, tuseme ulichoandika ni kweli, siku moja nitalia na kujuta.

ikiwa kweli nitalia na kutamani siku zirudi nyuma, ulimwengu ambao unaruhusu watu kulia na kutamani siku zirudi nyuma kwa namna hiyo, ni ulimwengu ambao unathibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Ulimwengu ambao Mungu huyo yupo, hauna kilio wala kutamani vitu visivyowezekana. Kwa sababu Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na kilio na majuto ni contradiction.

Kwa kuangalia mambo juu juu tu, unaweza kuona una hoja ya kuukubali uwepo wa Mungu.

Lakini, kwa mtu anayeangalia mantiki kwa kina, hata kama unachosema kitatokea, kitatokea kweli, kutokea kwa hicho kitu kutazidi kuthibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote hayupo.
 
Mi kila nikiangalia angani, hasa usiku. Huwa nasema Mungu yupo.
Hii ni imani, ni haki ya kila mtu kuamini atakavyo.

Lakini hakuna factual and logical evidence hapo ku connect anga linavyoonekana na Mungu kuwapo.

Watu tunapenda kutoa majibu rahisi kwa maswali magumu ambayo hatujui majibu yake.

Unaangalia angani usiku.

Unaona nyota nyingi, mwezi, pretty cool.

Unajiuliza, hizi nyota zimekaaje huko juu bila kudondoka? Zimetokeaje?

Unasema sijui. Sasa hapa ndipo tatizo linapoanzia.

Wenzetu wakifika "Sijui", wanafanya utafiti kujua nyota zinaanzaje, kwa nini zinakaa juu hazidondoki chini, wanajua gravity, wanajua light ina kasi gani, wanajua space, wanajua kwa nini nyota zinang'aa, wanajua hesabu za nuclear fusion zinazotokea katika nyota, wanajua elements zinavyokuwa formed kwenye nyota, wanajua umbali kwenda kwenye nyota in light years, nyota hii ina element gani kwa kuangalia mwanga wa nyota. Wanajua nyota hii imekuwa formed miaka mingapi iliyopita, na itaishi miaka mingapi ijayo kabla haijasambaratika.

Wanasoma kwelikweli kutafuta majibu, kwa fact, kwa logic.

Na hata wasipopata majibu yote leo, wana a self correcting process that converges to the correct answers as time goes. Science.

Sisi wengi tunaangalia nyota na kuishia kwenye jibu la Mungu yupo.

Tumemaliza mchezo hapo.
 
2017 nilichomwa visu saba nikiwa eneo hatari zaidi duniani delft ndani ya capetown..lakini sikufa mungu ni mkubwa.
 
Hujajibu swali langu la wasahihishaji kukosea kutoa majibu.

Pia, tuseme ulichoandika ni kweli, siku moja nitalia na kujuta.

ikiwa kweli nitalia na kutamani siku zirudi nyuma, ulimwengu ambao unaruhusu watu kulia na kutamani siku zirudi nyuma kwa namna hiyo, ni ulimwengu ambao unathibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Ulimwengu ambao Mungu huyo yupo, hauna kilio wala kutamani vitu visivyowezekana. Kwa sababu Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na kilio na majuto ni contradiction.

Kwa kuangalia mambo juu juu tu, unaweza kuona una hoja ya kuukubali uwepo wa Mungu.

Lakini, kwa mtu anayeangalia mantiki kwa kina, hata kama unachosema kitatokea, kitatokea kweli, kutokea kwa hicho kitu kutazidi kuthibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote hayupo.
Kwa level uliyofikia ni kazi bure kukuelimisha maana upo katika kiwango cha juu zaidi cha upagani,kwasasa ni Mungu tu( ambaye unasema hayupo)ndio wa kuingilia kati ili uokolewe.
 
Kwanza kabisa, inaonekana una elimu finyu.

Upagani si kutoamini uwepo wa Mungu.

Upagani, jina ambalo watu walioelimika wa keo wanalikwepa sana, na ukilitumia leo unajionesha ulivyokuwa nyuma, ni jina ambalo watu wenye akili za kikoloni waliojiona wao ndio wanamjua zaidi Mungu, hususan Wazungu wakristo, walilitaja wakikusudia kuwaita watu walioamini dini nyingi tofauti na zao.

Kwa hivyo, watu walioamini dininza asiki za Africa, Asia, Amerika etc, waliitwa wapagani na wazungu wakristo.

Mtu asiyeamini uwepo wa Mungu si mpagani. Kwa sababu kuna watu wengi walioamini Mungu/miungu ya asiki waliitwa wapagani.

Hiyo ni kuhusu upagani.

Nitakuja kwenye hoja yako nyingine ya "ni kazi bure kukuelimisha".
 
Kwa level uliyofikia ni kazi bure kukuelimisha maana upo katika kiwango cha juu zaidi cha upagani,kwasasa ni Mungu tu( ambaye unasema hayupo)ndio wa kuingilia kati ili uokolewe.
Hiyo hoja ya "ni kazi bure kukuelimisha" kiukweli imetajwa hata kwenye Quran.

Kuna mstari kwenye Quran unasema, kuna watu msisumbuke kuwaelimisha, maana Allah mwenyewe ameifanya mioyo yao kuwa mizito, amewaziba macho na masikio wasimjue. Na atawaadhibu kwa adhabu kali.

Sasa, ulimwengu ambao inawezekana ikawa ni kazi bure kumuelimisha mtu kuhusu uwepo wa Mungu, ni ulimwengu unaothibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, asingewaziba watu macho na masikio wasimjue, asingewafanya mioyo yao iwe mizito wasimjue, kisha akawaadhibu kwa kutomjua. That is a contradiction.

Mungu angekuwepo, kila mtu angemjua, kila mtu angemjua bila utata, na kila mtu angemjua Mungu huyo huyo mmoja.

Uwepo wa ubishani mwingi kuhusu uwepo wa Mungu ni uthibitisho kwamba Mungu hayupo.

Mungu huyu hayupo, ndiyo maana hata wewe umeshindwa kumtetea, umeiacha hiyo kazi aifanye mwenyewe.

Na hawezi kuifanya.

Kwa sababu hayupo.

Kama unabisha, thibitisha yupo, na ondoa matatizo ya kimantiki katika dhana ya kuwepo kwake.
 
Hii ni imani, ni haki ya kila mtu kuamini atakavyo.

Lakini hakuna factual and logical evidence hapo ku connect anga linavyoonekana na Mungu kuwapo.

Watu tunapenda kutoa majibu rahisi kwa maswali magumu ambayo hatujui majibu yake.

Unaangalia angani usiku.

Unaona nyota nyingi, mwezi, pretty cool.

Unajiuliza, hizi nyota zimekaaje huko juu bila kudondoka? Zimetokeaje?

Unasema sijui. Sasa hapa ndipo tatizo linapoanzia.

Wenzetu wakifika "Sijui", wanafanya utafiti kujua nyota zinaanzaje, kwa nini zinakaa juu hazidondoki chini, wanajua gravity, wanajua light ina kasi gani, wanajua space, wanajua kwa nini nyota zinang'aa, wanajua hesabu za nuclear fusion zinazotokea katika nyota, wanajua elements zinavyokuwa formed kwenye nyota, wanajua umbali kwenda kwenye nyota in light years, nyota hii ina element gani kwa kuangalia mwanga wa nyota. Wanajua nyota hii imekuwa formed miaka mingapi iliyopita, na itaishi miaka mingapi ijayo kabla haijasambaratika.

Wanasoma kwelikweli kutafuta majibu, kwa fact, kwa logic.

Na hata wasipopata majibu yote leo, wana a self correcting process that converges to the correct answers as time goes. Science.

Sisi wengi tunaangalia nyota na kuishia kwenye jibu la Mungu yupo.

Tumemaliza mchezo hapo.
Kina ninavyozidi kufahamu habari za nyota, galaxies na ulimwengu kwa undani ndivyo ninavyozidi kuamini kuwa Mungu yupo(Nikimaanisha nguvu inayojitambua iliyopanga na kutengeneza vitu hivyo) Kadri ninavyovichunguza ndivyo ninavyoona kuwa kuna uwezekano mdogo sana kwamba vikitokea bila kupangwa.
 
Kuamini si issue. Unaruhusiwa kuamini, uongo, ukweli. Ni haki yako ya kikatiba.

Ila, hujaweka ushahidi wala uthibitisho kuifanya imani yako hiyo ipate hadhi ya kuwa ukweli.

Hata mini naweza kusema kila ninavyoangalia habari hizo napata Imani kuwa babu yangu mzaa mama ndiye aliyeviumba vyote hivyo.

Hilo halifanyi imani hiyo iwe ukweli.

Kama unataka twende kwenye ukweli, thibitisha mambo.

Kama unataka imani tu, unaruhusiwa kuamini chochote.

The appearance of created order does not mean the order is created.

Inawezekana your window of observation of the universe give you that illusion of created order.

Kuna bwana mmoja mvuvi. Alikuwa anatafuta size ya samaki wadogo kabisa katika sehemu ile ya bahari.

Akatumia nyavu ya matundu ya ukubwa wa unit 1.

Akashindwa kukamata samaki wadogo kuliko wa ukubwa wa unit 1 (kwa sababu walipenya katika nyavu, hawakushikwa)

Akaishia kuhitimisha kuwa samaki wadogo kabisa katika bahari ile ni wa ukubwa wa unit 1.

KWa sababu hakuweza kukamata wadogo zaidi.

Kumbe hakujua kuwa conclusion yake ilitokana na nyavu aliyotumia tu.

Na wewe umefanya kosa lile lile la yule mvuvi.
 
Inahitajika imani tu. Kama wewe umeona nafsi yako imeridhika na ushahidi unaaonyesha kuwa babu yako aliumba ulimwengu unaruhusiwa kuamini hivyo. Kwangu mimi mpangilio wa ulimwengu unatosha kuniaminisha kuwa kuna aliyeuumbwa na haukotokea hivi hivi bila kupangwa.
 
Lakini mimi siongelei imani.

Nishasema imani unaruhusiwa kuamini lolote, ukweli au uongo.

Imani ni haki yako ya kikatiba, ni human right yako, ipo katika Universal Declarationnof Human Rights tangu December 10 1948.

Na mimi si mtu wa imani, lakini natetea haki ya kila mtu kuamini anavyotaka, au kutoamini kama mimi.

Miminsiongelei imani.

Naongelea ukweli uko wapi.

Ukweli ni zaidi ya imani.

Unaelewa tofauti?
 
Sawa mkuu naona Kina Kiranga wanabishana na hoja
 
Mungu yupo, ghafla tu nguvu za kiume ziliisha Kila nikiamka asubuhi bwana mkubwa amelala tu, mchana Hadi jioni hakuna mabadiliko yeyote.

Nilienda hospital nyingi bila kupata ufumbuzi wa tatizo langu, nikaenda kwa waganga napo nikaishi kulishwa madawa ambayo yakasababisha masikio yangu kuziba kwasababu ya kutumia mitishamba kwa wingi.

Hatimaye nikaamua kuegemea kwenye kumuomba Mungu tu, nikaanza kushirikiana na mwenzi wangu kwenye maombi, usiku wa manane tunaamka kuomba. Machine haisimami kabsa Wala siwezi kula mema ya nchi ambayo hapo awali nilikuwa nakula.

Tukasema basi ngoja tumlilie Mungu, kama zamani alifanya na Sasa atafanya. Ndugu zangu Mungu ni mwema Hali ikaanza kurudi taratibu, hadi muda huu Hali yangu ni tishio kabisa.

Katika harakati za kutafuta Tiba nimekuja kugundua Kuna wanaume wengi sana wenye haya matatizo ya kutosimamisha, nilienda kwa Mganga nikakuta vijana kama 7 Hivi wanaishi hapo kwa ajili ya kutibiwa.

Nikaingia mitandaoni Kila Kona kilio Cha kutosimamisha.
 
Back
Top Bottom