Tukio gani ulishawahi kufanya ukahakikisha umemfundisha mtu adabu?

Kumbe wewe ni mdada?
 
Kwa akili yangu ya kipuuzi ikanipeleka kuhisi au ni yule msanii ambaye nae kateseka sana,operesheni za kutosha mpaka India,now Amerest in peace,au nimechochora
 
WE muhuni wa kariakoo.
 
Hujawahi kufikiria kumsamehe my dear,hudhani kwamba inatosha now umsamehe
Umesoma vizuri nilichoandika??????
Umewahi kutoka kwenye nyumba yako ukiwa na nguo tu????
Umewahi kupoteza pesa zote kila ulichonacho????
Umewahi kudharaulika wewe??????
Hicho kipindi nilikuwa na connection kuliko unavyofikiria siwezi kuandika tu hapa.
Nilishamsamehe na sina namna ya kumsaidia.
Huko aliko ajifunze na awe mwalimu kwa wengine
 
Nilikuwa nafanya kazi kwenye kampuni moja, nilitokea kuelewana na Chief Engineer wa Meli moja kubwa ya Mizigo, tukapanga mpango wetu vizuri na chief wa kutuletea mafuta ya Diesel halafu tunayauza na kugawana pesa. Mimi nilikuwa na wateja tayari, nikamtafuta mwenzangu ambaye tunafanya kazi pamoja na yeye alikuwa anasimamia boat, kwa maana ya Captain wa boat na crew wake, hawa mwanzoni hatukuwaambia kitu lakini baadaye ikabidi niwaingize kwenye mpango kazi, wakienda melini wanapakia pipa 20-30,zikifika nafaulisha mpaka kwa mteja, mzigo ukiwa mkubwa kuna kusubiri kwa siku kadhaa kabla ya kulipwa.

Mwanzoni mawasiliano ya pesa nilikuwa nafanya mwenyewe, nachukua pesa namgawia kila mtu mgawo wake na ilikuwa cool. Siku moja sikuwepo nikaomba mwenzangu msimamizi wa boat akachukue ile pesa!
Alipochukua ile pesa akaona nyingi akaizima yote peke yake, matokeo yake nillingia gharama.Kwa hasira niliiua ile biashara tukose wote,tulikuwa tunaishi nyumba moja na mshikaji, nikahama na nyumba na sikuongea naye kwa miaka kadhaa, Sasa Manager wetu alikuwa mmoja, aligundua Mimi na jamaa hatuongei lakini sababu hakuijua, Siku alipokuja kusikia ilikuwa imepita miaka alishangaa sana na hakuamini mchezo ulivyokuwa, na kwa sasa jamaa ni Marehemu(apumzike kwa Amani), Baada ya Miaka nilimsamehe baada ya kuhama kampuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…