Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 15,052
- 36,866
- Thread starter
- #101
Mamie nimesoma mpaka tumbo limevurugika aiseeeh 😩Mi Kuna mtu aliniletea shida sana kuanzia kazini, familia mpaka biashara.
Mtu huyu alisababisha Mimi na familia yangu tuanze from the scratch.
Nitaelezea huku nachana page kuepusha mambo Mengine.
Maisha yalikuwa mazuri tu katika mji mmoja wa mpakani,,, niseme kiufupi familia ilikuwa na uwezo imejiimalisha kibiashara na kiuchumi katika umri ule mdogo wa kati.
Huyu best na mume wake tuliwapokea.
Sasa katika kazi na biashara.
Shost nilimfundisha baadhi ya vitu visivyohitaji mtaji makubwa kwenye magari lakini unaweza ingiza pesa zaidi ya elfu 30 kwa siku.
Sasa kwa wakati huo haya magari ya transit yalikuwa yakifika hapo ilikuwa ni lazima yaripoti kwenye ofisi yetu na tunawapatia pesa ya kuvukia.
Hili dili tukipata kupitia ofisi yetu ya kuuza spare. Ambapo matajiri walisikia sifa na utendaji wa kazi na walikuja kuomba tuwe partner.
Basi kupitia hapo tuliweza kupata gari sitaitaja kwa ajiri ya patrol.
Kisa chenyewe.
Babaa Ismail mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi.
Tulifanikisha kufanya dili moja hapo kwenye mgodi mmoja mkubwa na kuweza kubadili kontena halisi na kuweka ziro contena.
Bwanae rafiki yangu yule alijua baadhi ya details alipiga simu na kumueleza yule muhindi aisee!!!!!¡.
Nakumbuka mwarabu alifika alfajiri....... Weweee sijawahi kukamatwa vileeee!!!!!!
Yaaani!¡! Haitaki maelezo wala kesi anahitaji fidia yake ... Na kumbuka hapo Kuna baadhi ya truck zilishawahi kufika huko na mchanga wa kujengea nyumba😂😂😂
Bwana nyumba iliuzwa,,, viwanja viliuzwa,,pikipiki, gari wajomba walituchangia ndio kidogo mwarabu kukaa mezani na kuandika mkataba.
Shost anajidai kunipa pole mamaayo zake msengerama yule.
Kenge akasema anahitaji kumpuzisha kichwa......
Alienda kulima mpunga huko mpanda mi nilibaki kumbuka ofisi spare zoote ziliuzwa!!!!!
Nilianza moja kutumia uzoefu na vijana pia Kuna madereva waliipenda sana ile movie ilivyoenda walikuwa wanaotumia sana vijana wangu wakihitaji huduma ya grisi.
Mbwa yule nilichomfanya.
Nilienda kushtaki kwa bibi yangu.
Aliniagiza nipate utumbo uliolala kwenye butcher yaani uliobaki na maini yaliyooza.
Tulimu ozesha tumbo akiwa hai n
Aisee yule dada sikutaka afe nilitaka apitie nilichopitia .
mimi mtu akinikosea pakubwa siwezi kumuacha hata kidogo.
Kiufupi yule mpaka Leo anaumwa ni miaka kumi sasa!!!! Hospitali zote na hapo jirani kafika na hajapata tiba.. kwa waganga wamemlia pesa mpka kaoka kwa manabii wote kafika unaowasikia lakini Bado.
Operation kafanyiwa za kutosha na bado na akifanyiwa wanatoka wadi
Nilihitaji ateseke na kudhalilika kama alivyotesa familia yangu.
Maisha na mwarabu
Mwarabu alirogwa na kesi iliishia hapo,, baba Ismail na sisi ilibidi tutulie kabisa kuepusha viashiria vyovyote vile. Baada ya miaka miwili inshu yetu tukaimalizia.
NB;
Kuhusu bibi yangu mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi alishafariki miaka sita sasa. Na sina connection yoyote ya mganga.
Maelezo kidogo.
Watakao guna hapa ni aidha waache unafki au Bado hayajawakuta.
Pia Kuna wengine maisha kwao ni soft hawajawahi kukutana na misuko suko.
Africa ili uweze kumiliki ulichonacho ni lazima uwe bandidu,, katili, roho mbaya.
Usivyomiliki hivyo utaishia kupata mafanikio ya kawaida sana.
Mimi jamani nikikutana na misukosuko mikali kama hii nitaweza. Nafikiri naweza kujitundika kitanzi tu, sina roho ngumu hivi!
Nimeshakutwa na matukio ya hela na kibiashara mara mbili na mara zote nimeachilia bila ugomvi na moja ikanicost urafiki ambao uliniuma kuliko hata hizo hela (hela nilimuachia na urafiki bado ukafa 😪)