Tukio la kupotea kwa watu wengi hapa duniani kwa wakati mmoja limekaribia sana kutokea

Tukio la kupotea kwa watu wengi hapa duniani kwa wakati mmoja limekaribia sana kutokea

Ile siku ambapo watu wengi watapotea kwa wakati mmoja duniani kote imekaribia sana. Inaelezwa kwamba taifa fulani lilipochipuka na kukua basi ni ishara. Pia tukio hilo litatokea ndani ya miaka 100 ya taifa hilo, ambayo ni kizazi kimoja.

Aidha, wengi pia watakufa siku hiyo kwasababu baadhi ya watakaopotea watakuwa wakiendesha vyombo vya moto vitakavyopata ajali baada ya wao kupotea ghafla wakati vikiwa kwenye mwendo mkali. Siku hiyo itatisha na itakuwa mwanzo wa mapigo yatakayofuata.

Kwa hiyo itakuwa ni lini?
 
Ninaamini uwepo wa Mungu, ninaamini uwepo wa siku ya hukumu... Lakini sikubaliani na mnavyopagawa na tafsiri ya Kitabu cha Daniel na Ufunuo. Uishi Ukristu wako vema. Inatosha.
Haya ameyasema Yesu Kristo kwenye Mathayo sura ya 24.
 
Hakuna anayefahamu siku wala saa lakini Yesu Kristo alitaja dalili zitakazokuwepo. Unaweza kuzisoma kwenye mathayo sura ya 24 kwenye biblia takatifu.
Yesu nae alisema haijui hiyo siku, anaeijua ni Mungu tu. Sasa nyie mnaopiga ramli humu ina maana mnajua kuliko Yesu?
 
Mungu anaujua mwisho kwasababu yeye leo hii tayari anaona matukio ya mwaka 2030, 2050, 2100 nk. Anakuona utakavyokuwa unafanya maamuzi.

Kwahiyo ni sahihi kumuomba atupe kufanya maamuzi sahihi.

Mkuu kwa kifupi ni kwamba, kutokana na maelezo yako, wewe kama uliumbwa kwenda motoni, utaenda motoni! No amount of prayers will save you. Mungu yeye alishachagua watu wake kabla hata hajawaumba, na wewe kama sio mmoja wao, imekula kwako.
 
Hahahahah movie zinakuchanganya




Anyway kwa kuwa tuko jukwaa takatifu tuendelee kuheshima hoja



Na Mimi nina suala langu wanasema ipo siku umeme utakatika ghafla na internet duniani kote je ni kweli na nini kitasababisha power ku off ghafla
Mwaka 2000 ulipokuwa unaingia walisema hivyo na watu kwa woga wao sijui ujinga waliweka stock ya maji mengi sana majumbani kwao na toilet paper ndio ilikuwa inaongoza kwa vitu walivyosomba madukani
Wakati huo niko hapa kwa wazungu ndio walikuwa wanafanya haya

Nikawa najiuliza hawa watu kama wanaamini 2000 ndio mwisho wa Dunia toilet paper na maji wanaenda nazo wapi?
 
Watu wengi waliopo makanisani wataachwa, siku hizi wanawaza hela tu.
Kwani wewe huwazi hela? Bando unaloChat hapa umepiga mzinga mahali?Unanikumbusha Ile story ya Sabato masalia waliotaka kwenda kuhubiri marekani bila passport, visa wala pesa wakaishia Segerea ." Pesa ni suluhisho la mambo yote" , Mhubiri 10:19. Kutafuta pesa kwa njia halali haituzuii kuingia mbinguni🤔
 
Back
Top Bottom