Tukiwa kwenye zinaa na starehe wanaume hatutaki mtuletee mamimba yenu. Huo ni ukatili kwa wanaume

Tukiwa kwenye zinaa na starehe wanaume hatutaki mtuletee mamimba yenu. Huo ni ukatili kwa wanaume

Hii matumizi yake yapo je?
Wewe mtoto wa Mjini utaweza kunywa Majivu. Anatumia mwanamke, Baada ya kutoka kushiriki tendo chukua majivu weka kwenye kikombe cha maji masafi subiri kama nusu saa ivi alafu kunywa hayo maji yenye majivu. Kunywa maji hayo ndani ya masaa 24 baada ya kutoka kwenye tendo.

Usukumani vijijini kwa asilimia kubwa wanatumia hiyo njia, na mimi wife anatumia njia hiyo ya Uzazi wa Mpango.
 
Hata mfoke hadi koo liwakauke hicho unachokitaka kitawezekana tu kwa wewe kutumia condom tu babangu.

Hata sisi sometimes hatutaki kubeba mamimba yenu na mabichwa yenu mabaya, tunajikuta tu kwa bahati mbaya tushanasa damu zenu chafu.

Wengi wenu hamtaki condom na hata tukifuata kalenda bado tunaweza pata limimba,hata tukitumia vidonge bado unaweza jikuta ushanasa limimba la "hovyo"😃 ila kwa vile tuna huruma hatutoi.Tunazaa damu zenu chafu na kuzipenda.

Nyie wanaume msijione keki sana.Hata sisi kuna wanaume hatutaki kuwazalia.

Usitufokee kabisa.
Hili ni suala la pande zote mbili.
Usisukumie wanawake zigo la misumari.

Unataka uinjoy bila condom jiandae kwa limimba la kutegeshewa au la ajali.


Mnatukera sana mnavyotuharibia maisha yetu
 
6A1D4D9F-2687-4A81-B137-2436FB44A787.jpeg

😎
 
Kinga muhimu, ikipasuka vaa nyingine.
 
Umetoa boko Brother yaani hovyo kabisa kama ni wali basi umetoa boko leo

Hoja zangu 👇

1.Jukumu la kuzuia au kupanga kuleta mtoto duniani ni la mwanamke pekee au ni jukumu lako na mwanamke husika?

2. Unalala na mwanamke usie na mipango nae ya baadae kwanini usivae condom ?
Au ukivaa unasema sio tamu?
au ukivaa ukuni unazima?
Kwanini usivae condom?

3. Wewe kama mwanaume ukiwa kwenye tendo akili hua zina hama kiasi huwezi kuchomoa ukamwaga njee
Au huna uwezo huo unakua unatetema kama mayele?

4. Haya yote hayo yamekushinda sawa
Afta sex hujui kama kuna dawa za kuzuia uwezekano wa uja uzito kutunga ndani ya masaa 24 mpka 72 kwanini ukimaliza ku sex na huyo mwanamke wako usifanye utararibu wa kumpatia dawa ameze ili kunusuru mimba hiyo usioitaka

Baadhi yenu wanaume mnachekesha sana na hiyo mimba utampatia mtu asie smart kicwani saivi kubeba mimba ni kuchagua hakuna cha ajali wala nini

A. Mwanaume ukiona umebebesha mimba na ukaanza kulaumu wewe utakua mpumbavu

B. Mwanamke ukibeba mimba ukaanza kulaumu wewe ni mpumbavu pia

Hapo kutakua na wapumbavu wawili waliotanguliza hisia mbele kuliko akili


NB : nipo on kwa battle ila uje na hoja za mashiko🫴
Kinadharia. Ila kiuhalisia mwenye maamuzi ya mwisho kuhusu mimba ipatikane au isipatikane ni mwanamke.
 
TUKIWA KWENYE ZINAA NA STAREHE WANAUME HATUTAKI MTULETEE MAMIMBA YENU. HUO NI UKATILI KWA WANAUME.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Msitake kutuharibia Maisha sisi.
Serikali sasa inayohaja ya kufikiria kuunda sheria ya kukomesha ukatili huu wa kijinsia kwa wanaume. Unabebaje Mimba ya mwanaume bila ridhaa yake? Tena mtu sio mume wako. Unaakili sawasawa wewe.

Acheni kuharibu future ya wanaume. Mnawaumiza wanaume. Mnawakatili wanaume.

Hakuna jambo linakata na linawakera wanaume wengi kama umletee Habari za mimba zako za kipumbavu, mimba ya zinaa wakati hamkukubaliana hivyo.

Mtibeli nimekutongoza. Nimekufuata. Nimeomba mzigo. Hupajui kwetu. Sipajui kwenu. Hujui majina yangu yote. Hunijui sikujui na sinahaja wala sitaki kukujua. Sitaki kujuana na wewe.

Nimeomba mchezo, tufanye michezo ya kuzimu, uasherati na uzinzi. Wewe unajibebesha mimba kama chizi.

Unabebaje sasa. Unataka mtoto wa kuzimu sio? Unataka mtoto wa offside sio?

Hakuna mwanaume anayetaka watoto wa hivyo wewe. Acheni kutuumiza wajinga nyie.

Lazima wanawake mjue. Hakuna ukatili unaoweza kuufanya kwa mwanaume kama umbebee mimba alafu hajakuambia.
Mtu hakupendi unambebeaje mimba? Alikuomba?

Ni ukatili mkubwa kubeba mtoto tumboni ambaye Baba yake hukumwomba ridhaa. Unamkosea hata Mtoto.

Wanaume wengi huishia kulalamika moyoni. Hawasemi lakini wengi unapowapa taarifa umebeba mimba na wewe sio mkewe, hakupendi wanajisikia vibaya. Wanaumia. Wanakerwa. Ni Habari mbaya sana hiyo.

Sisi wanaume tunajua hakunaga mwanamke anayebeba mimba kwa bahati mbaya. Hasa wanawake wakubwa kiumri

Tena wengine elimu mnayo kabisa. Unaanzaje kubeba mimba na hajakuoa au hamfahamiani vizuri.

Alafu jitu linakuambia, alinipa mimba akanikimbia, alikuomba mjinga wewe?
Ni mumeo huyo mpuuzi wewe?

Wewe ndiye unajua siku zako za hatari.
Wewe ndiye unabeba mimba,
Wewe ndiye utakayezaa kwa uchungu.
Mtu anakubebeshaje mimba kama kweli zinakutosha?

Binti za Tibeli hawabebi mimba kipuuzi hivyo.
Kubeba mimba bila ridhaa bila kuolewa kwa binti za kitibeli huo ni uhuni, dhulma na utapeli kwa mwanaume na mtoto utakayemzaa.

Mwanaume anachukia mimba ambayo inabebwa na mwanamke ambaye hakutaka Amzalie.
Fikiria umebeba mimba alafu mwanaume anaiombea hiyo mimba isiwepo. Fikiria.
Anatamani hata zingerudi dakika ile afute hilo tukio ili hiyo mimba isiwepo ambayo ni mtoto uliyemzaa.

Najaribu kusema ukweli upi. Ni kwamba wanaume hatutaki mamimba yenu mnayoyabeba bila ridhaa zetu. Hatuyataki.

Haijalishi mtaukubali au kuupinga ukweli huu kwa kiwango gani.
Haijalishi mtatuona vipi lakini huo ndio ukweli.

Wanaume wenye ujasiri ndio watakuambia kabisa hilo mimba ulilobeba aidha ulitoe au utajua pakulipeleka.

Hayo yakusema sijui mtoto atakuja kuwa waziri au Rais au sijui kitu gani huo ni utetezi wa kishenzi na kikatili.

Ngono ni starehe sio kwaajili ya kubeba mimba pekee.
Mwenzako kaja kwa starehe wewe unamletea mamimba yako hapa. Hapana huo ni ushenzi na malipo lazima utayapata. Kikawaida ukweli unatoa malipo ya haki.

Ooh! Mtibeli kama ninyi wanaume hamtaki kuzaa na wanawake si mbaki kwa wake zenu. Ooh! Si mtumie kondomu. Blah blah blah!

Wewe uliona wapi Malaya akabeba mimba?
Unapofanya umalaya usisahau malaya hatakiwi kubeba mimba.
Anayestahili kubeba mimba ni Mke, mwanamke aliyeolewa.

Kwa nini utese mtoto kisa ujinga wako?
Niliwaambia sisi wanaume hatunaga shida na watoto. Na watoto sio big deal kwetu. Tena hao watoto wanaokuja bila ridhaa ndio kabisa hawagusi hata mshipa wa akili.

Binti na dada zangu, msiwe wajinga. Msipende kujibebesha misalaba ya kijinga. Msipende kuwatesa watoto wenu.

Yaani kweli unabeba mimba kwa mwanaume hajakuoa?
Unabeba mimba kwa mwanaume humjui, umekutana naye tuu kwenye daladala huko, mmepelekana kwenye madanguro huko, unajibebesha mimba.
Acheni kutesa watoto kisaikolojia.

Baba hawezi kukataa watoto aliowazaa kwa hiyari yake.
Baba hawezi kataa watoto waliozaliwa na mwanamke aliyempenda. Huyo Baba hayupo.

Lakini Baba hujisikia vibaya na hasira mtoto kuzaliwa na mama asiyewahi kumfikiria atambebea mimba Tena kihunihuni katika matendo ya kihuni.

Mwanaume anaweza kulea hata mtoto asiyewake kwa mwanamke anayempenda.
Ila wanaume hupata ukakasi kulea mtoto aliyezaliwa na mwanamke asiyempenda.

Muelewe hilo. Mkichukia shauri yenu.
Kuzaa sio jambo la kujitokea sadaka na kujiamulia amulia tuu. Ni jambo linalohitaji mambo makuu yafuatayo;
a) Upendo
Upendo wa pande zote mbili mwanaume na mwanamke.
Mtoto ambaye amezaliwa kwenye upendo ataishi maisha mazuri sana. Hawezi fanyiwa ukatili.
Lakini mtoto ambaye amezaliwa mzazi mmoja hana upendo au wote walikutana kwenye tamaa tayari huo ni ukatili kwa watoto

b) Ridhaa na Makubaliano.
Sio unajibebea tuu kama lijinga. Au mwanaume atumie nguvu kukubebesha mimba. Huo ni ushenzi.
Mimba na watoto wanatakiwa wazaliwe kwa ridhaa na makubaliano ya wazi kati ya mwanamke na mwanaume.

c) Utayari.
Haya mnapendana, ridhaa ipo yaani wote mnatamani na kupenda mpate mtoto pamoja lakini utayari hamna.
Utayari unatokana na factors mbalimbali. Kuna mambo ya kiuchumi, mazingira, Mila na desturi.
Mtu hajakutambulisha hata kwenu au kwao anakubebeshaje mimba. Ni kwamba bado hana utayari.
Utayari wa malezi.

Sasa mtu anabeba mimba ya Mume wa mtu. Shenzi! Huyu anatakiwa ashtakiwe kabisa.

Msiwe mnaoneana haya kwa mambo ya hovyo kama haya. Ndio yanaleta matatizo.

Ooh! Wewe unajijua ni mume wa mtu why utafute wanawake wengine. Natafuta malaya huko nje. Ili nifanye umalaya(starehe).
Na sio uniletee watoto.

Pesa yako nilikulipa. Nilikupa pesa ya kazi uliyoifanya, kazi ya umalaya, kunipa starehe.
Mimi sio mumeo, sio kaka sio Baba hukushangaa hela niliyokupa ilikuwa ya nini? Ilikuwa business.

Wewe kama mume wa mtu anakufuata na unampenda.
Zungumza naye kwamba unataka kikao na mkewe.
Mjadiliane mkikubaliana sawa. Msipokubaliana sawa. Unapita kushoto.

Sasa unajua mwanaume anamke. Anakupangia nyumba(danguro) ya kufanyia ufuska wenu.
Hataki mkewe ajue. Mpaka hapo huelewi nini mbuzi wewe. Kwamba wewe ni malaya tuu. Upo kama bidhaa ya magendo.
Unakubalije kuwa bidhaa ya magendo?
Hujipendi? Hujithamini? Umejikosea nini mpaka ujidharau kiasi hicho? Mpaka unaruhusu mwanaume akudharau kiasi hicho kweli binti yangu, kweli?

Alafu wewe ni bidhaa ya magendo unazaa matoto ya magendo. Hivi ziko timamu kweli.

Usikubali mtu akudharau binti yangu. Usikubali kujidharau.

Kuwa na msimamo. Mwambie mimi ninajiheshimu. Siwezi kuishi maisha ya kudharauliwa, kufanywa mchepuko sijui magendo. Hapana.

Sema wewe sio second class, wewe sio Takataka inayofichwa kwenye shimo la taka.

Huwezi ukasema unajiheshimu na unaheshima wakati umegeuzwa bidhaa ya magendo.

Na ulivyo lijinga kama sio umelaaniwa, unajigamba umepangiwa nyumba, sijui umenunuliwa gari au unajengewa.
Nyumba hata ndege wanaviota, na mchwa wana vichuguu.
Thamani yako ni kubwa.

Mwambie kama anakupendi nini kinamzuia usiwe mkewe? Sheria zinaruhusu. Fungeni ndoa ya kimila. Kaongee na mke mwenzako. Wekeni mambo sawa.

Mheshimu mke uliyemkuta. Sio uanze kujilinganisha hapa. Wewe ni wapili mheshimu wakwanza ili ndoa na familia yenu iwe imara.

Sisi Watibeli hatuoi Wake Wengi. Ingawaje sheria zetu zinaturuhusu kufanya hivyo ikibidi. Ikitokea tumeoa Wake wengi mke wa kwanza atabaki kuwa mama wa boma. Chagua namba moja. Lazima umheshimu utake usitake.

Nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Mwenye masikio na asikie,
Mimi nimetoka zangu kutafuta ladha mpya wewe unanibebea mimba we fala nini?
 
..Maturity ya Uhanga,Mfumo na Ushuhuda wa Madhara ya wazi na vitendo vya kuyaona Laivu home/Mtaani/-Yeye mwenyewe..,(Rafiki/Dada,nk).

Humushauri kitu.
Nimewahi kukutana nao kwenye project ya kuhusiana na Maisha yao..
Daah!?Wengi ni Watendwa wa matukio yenye kutisha na alishaganda na kuamua.

Anakupa Ushuhuda wa kisa/Mkasa na kupaba order uite Kiongozi wa Dini yoyote aamue..
Noted
 
Kinadharia. Ila kiuhalisia mwenye maamuzi ya mwisho kuhusu mimba ipatikane au isipatikane ni mwanamke.
Wenye maamzi ni wote wawili mwambie mwanamke mapema
Kua haupo tayari kua baba

mshirikiane kuepka mimba bila mipango

akijifanya kicwa ngumu muache atajua mwenyewe

Ila swala la kupanga uzazi usiamuachie peke ake
 
Nimependa hapo ulipowakumbusha wapumbavu wakiume na wakike mambo zao za kupeana mimba bila mipango,mbeba mimba na mbebeshaji mimba wote mataahira Tu!
Kabisa mbebesha mimba na mbebaji na baadae kuanza kujifanya et ni bahati mbaya wanachekesha
Hawa wapumbavu wawili😁😁
 
Wewe mtoto wa Mjini utaweza kunywa Majivu. Anatumia mwanamke, Baada ya kutoka kushiriki tendo chukua majivu weka kwenye kikombe cha maji masafi subiri kama nusu saa ivi alafu kunywa hayo maji yenye majivu. Kunywa maji hayo ndani ya masaa 24 baada ya kutoka kwenye tendo.

Usukumani vijijini kwa asilimia kubwa wanatumia hiyo njia, na mimi wife anatumia njia hiyo ya Uzazi wa Mpango.
Sawa hivi hakuna madhara kumbuka baadhi ya miti ni sumu
 
Mwenye wajibu na uwezo mkubwa zaidi wa kupanga mimba ni mwanamke.
SAsa mtu anayetaka kukutegeshea mimba atajikinga?Si ww mwanaume ndo ujikinge?
Kila jinsia ina wajibu wa kujikinga na mimba isiyoitaka.
 
Back
Top Bottom