Tukumbushane: Ulishawahi kuanzisha vagi au kuanzishiwa vagi Mtaani?

Tukumbushane: Ulishawahi kuanzisha vagi au kuanzishiwa vagi Mtaani?

Ah hayo ndo yalikuwa mambo yangu.

Nilikuwa natembea na mkia wa taa muda wote.

Kila mimi na washikaji tukienda kwenye mechi lazima nilianzishe.

Ila nilikoma pale siku moja Wamakonde waliokuwa wanakaa kama walinzi kwenye nyumba ya jirani waliponilia timing wakanipiga jiwe juu ya hicho baada ya kumvuruga kaka yao.

Kama lile jiwe lingeshuka chini kidogo ya nyusi basi leo hii ningekuwa na chongo.

Ila niliipata maana uchokozi wangu wote ulinitokea puani.
NN, kumbe na wewe mtata
 
[emoji3][emoji3][emoji3] mzee itabidi na mimi nikutafute nikuonee
Ha ha ha ha mzee haka kamwil kafaida kananipa sana point maeneo fulan naonekana mtoto mwenzao...
Nyie mnionee tu ila maeneo yangu na mie nakula Pweza gizan
 
Mmmh, hivi niliwahi kupigwa kweli mm sidhani, lbd mambo ya fumanizi fumanizi ndiyo nimebobea sana [emoji12] [emoji12]
(Joking)
Ulishawahi fumaniwa?
 
Kuna siku nilikuw nimeenda club bn..
Nikatumia bapa za kutosha mpk akili akiwa sio yangu tena. Pembeni angu kulikuw na mrembo , kama kawaida yetu nikamfata bana. Kumbe alikuw na jamaa ake
Yule jamaa ake akanikazia kidg, nikaona isiwe tabu bn nikamtia kitasa
Kumbe jamaa alikue na kundi lake kam la watu 12 iv. Wakanivamia, nahic nilikula scale kubwa zaid ambayo cjawahi kuipata tangu nianze vurugu mpk nikakata moto.
Nimekuja kustuka saa 10 alfajir nipo mtaroni tena mvua ndo ilikuw imeanza kunyesha.
Siku ile siwezi kuisahau mimi


Sent using Jamii Forums mobile app
Pole asee
 
Nilipewa pass ya kwenda kung'oa jino Mawenzi hospital, ilikuwa Ijumaa niliamua kuingia disco lakaa ya kutudi shule J'mosi. Sasa kulikuwa na wavulana wawili wananifukuzia kheri si nikawakuta wote ndani, kila mtu anataka kuwa na mimi ugomvi disco lilifungwa.

Moshi si kuwa ninajulikana vijana walitaka sana kumjua manzi aliyesababisha disco kufungwa na police kuingilia, wakati huo nilishachukua tax na kutokomea.
[emoji23][emoji23] eti disco likafungwaaa
 
Ha ha ha ha mzee haka kamwil kafaida kananipa sana point maeneo fulan naonekana mtoto mwenzao...
Nyie mnionee tu ila maeneo yangu na mie nakula Pweza gizan
Haa nyie ndiyo mnsotumaliizia watoto wetu wa la saba
 
Miaka hiyo nipo mkoani tulikuwa tunasifika sana Kwa vagi...tulijiita Red Star Camp...

Tuliuvaa mkenge siku moja Kwa Jamaa wabebs vyuma.
Mwanzo tuliwatembezea waya sana.walivyoona tumewashinda wakaongeza nguvu kwakiwaita Jamaa zao wengine.

Ebwanaee tulipigika mpaka tukapoteana kila mtu na kona yake.

Banat mbaya me nikaingia chakike ebanaee cjawahi chezea kichapo takatifu ndani ya muda mfupi kama kile....mungu you mwema,nilipata kaupenyo kadogo nilichomoka kama mshale wa Masai amwindae simba Kwa shaft la kupewa mke!!

Nilikoma.
 
Back
Top Bottom