Tukutane hapa ambao ndoa zao zimekufa ila tumebaki kulea tu watoto

Tukutane hapa ambao ndoa zao zimekufa ila tumebaki kulea tu watoto

Ndoa sio nyepesi, acheni ujinga wa kukimbia wajibu.

Mnadhani sisi wazee tuliishi bila changamoto na mama zenu?, jibu ni HAPANA ila tulikabiliana na yote mwisho tukavuka.

Acheni kuishi nyie vijana maisha ya maigizo ndipo mtaziweza ndoa, mkihendekeza maisha ya uanaharakati yaani baba ndevu, mama ndevu sijui na mtoto ndevu matokeo yake ndio hayo.

Ishini maisha halisia ya kiAfrika, hakika ndoa zitadumu, vinginevyo mtaishia kulia lia kila siku.
 
Ndoa haina MUNGU MUUMBAJI au haina shetani kama msingi wake, unategemea nini?

Unategemea nini?

Hata biashara uwekeze MTAJI WA KUTOSHA kama haina MSINGI WA KIROHO itakufa na utaichukia tu...

Umeoa lakini kuna shangaz yako hajapenda, kuna mchepuko wako nao unataka ukumiliki, kuna ex wako alijua utamuoa sasa umemuoa huyo mzuri kumzidi, na kuendelea...

Ndoa ni kama shamba linalohitaji uangalizi wa kila muda...
 
Honestly Taasisi ya ndoa Kama imefika mwisho wengi tumebaki kulea watoto tu katika ndoa zetu.
Maneno tunayotamkiana ni zaidi ya Vita.

Guyz things are not easy. Kukaa alone ni Bora Sana kwa zama hizi.
Usijali mkuu hakuna ndoa ya kizazi cha sasa itadumu mimi sio mchawi lakini[emoji847]
 
Ndoa sio lelemama, usiishi kihuni kwenye ndoa, pia usiishi kama mfungwa kwenye ndoa, uvumilivu uwepo na uaminifu ni silaha nzito, gubu ni baya hupunguza upendo na upendo ukipungua kifuatacho ni matukio,

Elimu juu ya masuala ya ndoa itolewe kwa pande zote hasa Wanaume wa siku hizi wanaingia ndoani kibubu bubu, wakikutana na changamoto kidogo tu wanakimbilia mtandaoni kuomba ushauri.
 
Kwa hiyo hizo changamoto nyie wanawake ndiyo mnazileta sio?
Ndiyo maana wanaume wanakimbia
 
kitu napenda ni mwanaume asimame kama mwanaume, yani akiniambia jambo kwa sauti ya mamlaka natii bila shuruti, mwanaume aniongoze despite ninampita vitu vingapi still nitataka awe kiongozi kwangu sasa mwanaume unashindwaje na ndoa yako? au ndio kina nyinyi mnaopenda matako makubwa mnaoa kichwa kichwa? take time msome mwanamke unayetaka kuingia naye ndoani, msikurupuke heri uchelewe kuoa uoe mtu sahihi kuliko uwahi kuoa kwa mihemko ndoa sio rahisi na ndoa sio kwa kila mtu.
 
Back
Top Bottom