Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda




Dah

Pesa pesa, ikiwepo shida na isipokuwepo pia ni shida
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 hapo utakimbia hadi usikie kufa
 
hahahahahahahahahahahahaaaa nimecheka mpaka mbavu zimeniuma.
 
Aisee nimecheka kinoma 😂😂😂😂
Cc kadagala1
 
Hii kali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitosahau ule mwaka tumepiga tukio NBC ubungo......pesa ya kuiba Bank tamu sana.
 
Kuna siku natoka masai club narudi home nikakutana na mateja wawili wanataka wanikabe nilipiga teke la tumbo yule mwenye panga alitoa kilio cha ajabu nikadaka yule mwingine nikamfinya nikamtia nako nikamsachi nikakuta elfu arobaini na chenji nikamuendea na yule mwingine aliyelala nikamsachi nikachukua hela na simu nikaacha amelala pale!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
No way, can't believe you!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeua aisee, nimecheka vibaya sana hapa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…