ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,728
- 34,860
Hongera sana umepata mume....Mwaka fulani nimetoka mbeya na Mr saa saba za usiku, Kufika maeneo fulani karibu na morogoro kuna kona fulani hivi ya kishkaji, sijui Mr alikua na nini kichwani hakuangalia mita kadhaa mbele, mi nimelala zangu nakula usingizi kwa raha zangu, gafla nikahisi kama gari imepaki gafla, nikasikia ananiambia amka amka! Kufungua macho naona malori mawili yamepaki pembeni ya njia mbele ya malori kuna gari dogo nayo imepaki halafu kuna bongee la gogo katikati ya barabarani Mr akanambia kuna tukio la utekaji hapa either linaendelea ama kimeisha muda si mrefu,Salaleee usingizi ulinitoka wote, nikakwambia Mr turudi tulikotoka akanambia No, kwenye matukio kama Haya huwa haturudi nyuma. Nilipaniki nusu nimnase kibao nikamwambia sa tusirudi nyuma tubaki hapa watushike na sisi? Akasema anavoona yeye lile tukio limeshaisha na wenye magari haya either wamepaniki wamekimbilia vichakani ama watekaji wamewachukua wameondoka nao... nililoa jasho hadi pichu, mi kwa akili yangu nilikua nafikiri wamewakusanya wenye magari wako nao mahala wanatuangalia na watajitokeza sio muda kutuchua na sisi Ndio maana nilikua namsisitiza Mr turudi tulikotoka ye anamsisitiza hakuna kurudi . Akanambia ye anashuka ajaribu kutoa gogo tupate pakupenya, hivo mi nishike wheel ikitokea wakajitokeza wakamkamata mi nirudishe gari reverse vyovyote vile bora nipate ajali ila wasinikamate nikiwa mzima anasisitiza maana wanaweza kunibaka. Haya mabishano yote yalifanyika kwa dakika kadhaa... mwisho kishingo upande nikamkubalia ashuke. Akashuka nikakamata usukani, nikafunga belt nikajiandaa huku natetemeka hakuna mfano. Ile ameshuka tu akakamata gogo naona ni zitooo hata haliwezi akatokea kijana porini amepigwa vibaya sana kumbe alikua mmoja wa madereva waliotekwa, kidogo wengine wakajitokeza wakawa wanaelezana kilichotokea, mwisho wakakubaliana watembee kwa kuongozana hadi wakutane na Barrie ya mapolisi watoe taarifa. Wale madereva na makonda wao walikuwa wamepigwa sana wanavuja tu damu, nakumbuka mmoja sikio la kulia lilikua limelegea kama linataka kudondoka na kwa wakati huo niliona kama hasens chochote zaidi ya kuona tu midamu inamvuja. Basi ndo hivo tukaondoka kwa kuongozana tulifika Barrie ya polisi karibu kabisa na moro tukawaacha sie tukasepa zetu, tumbo liliniuma siku hiyo sitasahau sijui ni sababu ya uoga.
Eti ngoja msafara ufike salama[emoji23][emoji16][emoji23][emoji16][emoji16][emoji23][emoji16][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
Tulidili na 'don' wao baada ya kumtaja... Tulimwambia pesa iliyochukuliwa tarehe fulani irudi na ya usumbufu... Hakua hata na maneno, fedha akarudisha..
Hizi likes zote umezitoa wapi...ilhali ilikimbilia juu ya kenchi huku ukimuacha mkeo na mwanao wawe asusa....???Walituvamia 2016 Sept ,majambazi zaidi ya kumi walivamia nyumba nne usiku mmoja na ya kwetu ilikuwa ya pili ,walivyunja mlango wa chumba na ule wa mbao ndani ya sec Ila walitumbukia sebuleni maana nyumba yenyewe ilikuwa ujenzi haujaisha , hata milango haikuwa stable Sana ,wakapiga paaaa moja tu ,nikashituka nikachukua panga nikalikwaruzaa ukutani nikiwa kuchumbani paraaaaaa paraaa "nikawambia mkiingia tu tutaonyeshana kazi" wakaema we tulia "tunakuja'
Aisee kishindo Chao Kuna friji lilikuwa kwenye korido walilidondosha kulee vyakula hukooo mayai hukooo yaani ,umeme wakakata wakawa ma matochi makali balaaa ,Sasa mi kuona vile nikapanda juu kwenye makenchi maana palikuwa wazi ..wakazama chumbani wakamkuta wife kakaa tu kitandani hajui afanye Nini mi nipo kwa juu tu naangalia ,maana nilivyowachimba mkwara wangenishilka wasingeniacha hai...wakamwambia wife tunataka pesa akasema Hana chochote wakamwambia lete pochi ya kazini akawapa ,akawapa simu zake zote ,pochi ilikuwa na elfu tano ,wakasema unatuchezea wakaenda chumbani kwa mtoto wakamchukua wakamleta kwa wife , mbele yake wakamwekea panga mtoto shingoni wakasema tunahesabu Hadi kumi ...
Wakaanza walivyofika tano nikawambia chukue suruali Ina pesa hapo kwenye kochi wakachukua kulikuwa na laki mle ...basi majirani wakawa wameshutuka wakapiga filimbi wakasepa ,wakaenda kuvamia nyumba zingine 2 ...toka kilindi hicho huwa sila hata Sasa hivi nasikilizia kimtindo ....na nimefuga mbwa wa kunishtua
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimecheka sana aisee....ww muoga sana unakimbia huku unalia.....ulishindwaje kumkabili mwizi mmoja!!?Mi nakumbuka wakati nipo Chuo,siku moja natoka kupiga bia zangu baa ya jirani tu kama meter 500 toka getho, ilikuwa majira ya saa 6 usiku, napita karibu na kapori nikasikia mtu ananiita oyo nisubiri kugeuka nyuma nikamuona yupo Kama hatua 15 toka nilipo,nikamuuliza wewe nani ghafla akaanza nikimbiza,nilikimbia mbio kama filbert bai hakunishika, alirusha mawe Sana akanikosa.Ile nafika getho get la kuingilia limefungwa kucheki nyuma anakuja basi nikaamua kukimbia huku nazunguka nyumba nikapiga kelele kuwambia washkaji huko ndani oyooo fungueni fasta nakimbizwa na mwizi jamaa kusikia ivo akasepa.mi nikaingia ndani.
Ndiyo mkuu wangu, hiyo ilikuwa ni volvo, siku hyo waliokuwa wametangulia mbele walikula kichapo balaa...
Hatari Faya Hahahaaa!!!
Ww jamaa nimecheka sana aiseeNakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mi mwenyewe nilijiuliza ilo swali how
Una bahati sana....Tulidili na 'don' wao baada ya kumtaja... Tulimwambia pesa iliyochukuliwa tarehe fulani irudi na ya usumbufu... Hakua hata na maneno, fedha akarudisha..
hahahahahaMimi hata sio barabarani wala nini ila nilikua na jambazi ndani ya nyumba niliyembatiza jina la MKE WANGU sikuamini siku nimerudi nyumbani nakuta nyumba nyeupe peeee kama nilivyokabidhiwa na Faza house Nilikoma mimi..Sema hawa majambazi wa style hii wamenkosa saivi tangu niamue kuwa PADRI
Daa imenichukua dakika kadhaa kukuelewa,kumbe huyo mama hakuwa sehem ya majambazi?,inaonekana majambazi yalikuwa yametoka kufanya tukio sehemu nyingineMwaka 2007 asubuhi tukiwa kwenye daladala kufika buguruni mama mmoja kabaini simu yake imechomolewa na kibaka na anauhakika kibaka hajashuka akauwasha moto kuwa aliyeiba simu hajashuka akamwambia dereva tafadhali twende polisi akajitokeza Kaka mmoja akamwambia yule mama simu yako ni Aina gani na ni Sh.ngapi mama kajibu Nokia elfu sabini
Kaka akazama mfukoni akatoa laki moja tusiende polisi maana anaharaka saa hiyo tumekaribia mataa Buguruni gari ya Gongolamboto hiyo.
Mama kajibu sitaki laki line yangu instead majina ya wateja wangu wa samaki sitaki laki yako nataka simu yanguu twende polisi
Huyo aliyekua anataka kutoa laki alikua siti ya mbele karibu na dereva, basi Hari ziliporuhusiwa alitoa bastola akamuelekezea dereva akamwambia hatuendi polisi endesha gari kuelekea tazara bwana red Kumbe hakuwa peke yake huku kwenye siti niliyokaa Mimi Kumbe nimekaa na mwenzie naye akatoa bastola akaiinua juu akiamuru tutulie
Ulimi Wang ulikua wa moto mdomoni mpaka ninaufeel nilitetemeka Sana dereva alinyoosha mpaka Around uwanja wa taifa wakashuka jamaa wanne na Makoti makubwa wakaenda zao.
Sent using Jamii Forums mobile app
hao wa bank mliwachukulia hatua gani sasa?Nilihisi kuna mtu wa benki alinichoma, maana hakuna mtu aliyekua anajua naenda kuchukua hela pale.. Kuna jamaa zangu ni mabaka mabaka na mapolisi nikawaelezea nilivyoporwa... Wakaniambia tuandae mtego..
Baada ya wiki tatu nikarudi benki ileile kuchukua pesa.. Kweli bhana wale washenzi wakajilengesha, bila kujua 40 ndio zimefika.. Watatu walikufa palepale baada ya kupigwa risasi, wawili walikuja kufa baadae baada ya kutaja hela zinapokwenda... Hela walizochukua zilirudi na fidia juu...
Cc: Duke tuchaz, rikiboy...
Usiku una mengi, kuna wanadamu wao wamejitolea usiku kama ndio muda wao wa kutafuta chochote kitu,,, binafsi nimewai kukutana na matukio machache ya kukutana na wezi usiku.
Tukio la kwanza, nakumbuka tulikua form six miaka ya nyuma tunatoka kwenye kumbi za starehe tukiwa watatu tunarudi tuliko kua tumepanga uswahilini, njiani tulikutana na wezi wametoka kuiba samani meza, vitanda, na viti walikua wengi kiasi, jamaa walitusimamisha mmoja wao akatupiga mkwara mzito sanaa, nakumbuka walitubebesha meza, rafiki angu mmoja mwenye mwili mkubwa yeye alibebeshwa kabati, tulitembea kama kilomita mbili hivi wakatuachia, yule mwenzetu aliebeba kabati aliumwa mgongo wiki nzima.
Tukio la pili, nikiwa nakatiza mitaa ya sinza, nikakutana na kundi la vibaka wako kama sita hivi, saa sita usiku, ilikua ni ile position unakata kona unakutana na watu hawa hapa, siku sita nikapita kati kati yao maana hakukua na namna nyingine ya kukimbia, nilipigwa kabali ya hatari, huyu kashika mguu huu, mwingine kashika mguu mwingine, walinichukulia simu, waleti na viatu, tukaachana kwa mengi matusi tunatukanana.
Tatu, hii ilinikuta maeneo mapya niliyokua nimehamia, mida ya saa tano usiku nimetoka kunywa mitungi mtaa wa pili, walikuja vijana wawili kwenye boda boda na mapanga yao, mmoja nilimvamia kwa speed ya hatari nilimrukia teke moja akaanguka analia ana kufa, siku laza damu nilikimbia speed ya kufa mtu.
unaweza kushare mawili matatu kama umewai kukumbwa na mswaibu haya, then watu wakajifunza chochote na kuchukua precautions siku za mbeleni.
Naisubir thread yako mkuuNi gari Za NMB sio crdb, ilikua Saa 6 mchana.
Ngoja ntaanzisha thread yng nielezee matukio tulopiga japo kwa kifupi nilikuja kunasa maeneo ya nkuhungu Dodoma nikanusurika kuchezea moto lkn mguu walivunja na jicho wakatoa!!sshv nimekua raia Mwema na ibada nafanya Pia.
Sent using Jamii Forums mobile app