Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Baba yangu mzazi, mzee isaki alikuwa mlinzi kanisani. Ule ulinzi kwamba siyo mgambo wala askari ni raia tu, miaka ya nyuma uaminifu wako ulikubeba.

kazi hiyo aliifanya zaidi ya miaka arobaini. Akamwambia mchungaji wa lile kanisa, nguvu zimeisha nataka nipumzike, mchungaji hakuona kama serious issue, ikabidi mzee aendelee na kazi huku anangojea aletewe mtu wa kumwachia kazi.

Mwaka 2001, pasaka jtatu kuamkia jnne, waliingia wezi,

Wakamuulia baba yangu, ndani ya kanisa, pale madhabahuni damu yake ilijaa pale hadi tunaenda kwenye ibada ya mazishi iko pale, ilikuwa huzuni kubwa. mzee alikuwa mpole sana.

Walikamatwa vijana ila mama akasema sitaki kesi, mzee wangu wameshamuuwa, waachieni Mungu anajua.

Walikufa vijana wengi pale kwetu wakiweweseka tulimuuwa yule mzee kanisani. Wengine hadi wazazi wao na ndugu zao walikufa.

Wezi hawafai.

So sad.

R.I.P. Paradise Baba na Mama!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh pole. Sasa iyo mikoba ya mama hujairithi tumalize hawa vibaka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni Jambazi?
 
Hii inatisha aisee. Mimi majambazi siwaamini kabisa, ndio maana nadhani sipendi ku surrender, bora nife napambana kuliko niuawe nikiwa nimenyosha mikono juu ya kusalimu amri. I will surely fight to my last breath, siwezi surrender mbele ya ISIS wakati najua watanichinja huku wananirekodi na camera. Nitasurrender kama ni ambush kali ambayo sikustuka tangu wanavunja mlango. Mwenyesi MUNGU anihifadhi na shari zote hizi, maana sio mchezo yakikukuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo walewale tu wewe jambaz wa kike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wajinga wanateka magari,wanakusanya kila chenye thamani.Kuna njia tukipita lazima uwe na balance siyo chini ya elfu 50.Utachezea vitasa mpaka ukome kusafiri.Kuna siku wametuweka kwenye target kumbe sisi tupo kwenye kamsafara (tuliambatana na wazee wa Mabaka mabaka).Waliyeyuka kama upepo,halafu wajinga watakuwa hadi mauchawi wanatumia hawa.
 
Noma sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
@mamndenyi pole sana
 
Hapo walifanya makosa. Na wezi mkiwaogopa namna hiyo ndiyo wanazidi kuonea mtaa. Mimi jirani aliibiwa ikabidi nikae kimya kwa sababu sikuwa na namna. Ilikuwa hivi: Nilikuwa nimepanga nyumba moja haina uzio wowote kwa nje. Kati ya nyumba niliyokuwa nakaa na huyo jirani aliyeibiwa kulikuwa na uwanja ambao haujajengwa. Basi siku moja usiku kama saa 8 hivi tukasikia mlio wa risasi kwa yule jirani. Kuchungulia nje tukaona pikipiki mbili jamaa wawili wana makoti marefu na bunduki. Ile nashangaa nafikiria labda ni askari mke wangu akawaulizia nyie ni akina nani? (walikuwa wamepaki pikipiki zao karibu kabisa na dirisha la chumbani kwetu). Wakamwambia mama kaa kimya hatujakufuata wewe la sivyo unatafuta shari. Mimi kimyaa, jasho linanitoka. Kumbe kule kwa jirani kulikuwa na wengine wawili ndiyo walikwenda kuvamia. Mara wakarudi na kupakizana, haoo wakaondoka. Kusema ukweli ilibidi nikae tu kimya kwani hata ningejitutumua hizi nyumba za uswahili dirisha lina nyavu, mtu akiwa nje akipiga tochi ndani anawaona wote mliopo ndani. Hata akiamua kulenga ndani akapiga risasi anaweza kuwamaliza familia nzima. Baadae kabisa ndiyo majira wanatoka lakini wezi walikuwa wameshaondoka na fedha.
 
Ni ngumu hata kufikiria, yaani bora uumwe ufe kuliko kufa kifo cha kikatili cha kuchinjwa na binadamu mwenzio
 
Mh hii chai aisee mbuzi anaruka nusu SAA zima kachinjwa, Mara radi Mara visu vya moyo
 
Dah hadi nimesisimka. Pole sana dada yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…